Gari ya Lissu iliyopigwa risasi, isibadilishwe muonekano, ikae ilivyo, ipelekwe katika kila mikutano ya siasa kukumbusha madhila ya Hayati Magufuli

Gari ya Lissu iliyopigwa risasi, isibadilishwe muonekano, ikae ilivyo, ipelekwe katika kila mikutano ya siasa kukumbusha madhila ya Hayati Magufuli

Watanzania wengi ni matomaso, ukiwasimulia tu hivi hivi, hawaamini. Nashauri gari ya TAL isibadilishwe muonekano wake baada ya kupigwa risasi, matundu ya risasi yabaki, gari itengenezwe injini tu na sehemu muhimu, ila sehemu zenye matundu ya risasi zibaki.

Hii itafanya watu wakifika katika mikutano ya hadhara, kwanza wapate somo lwa kuliangalia gari, kisha watajikumbusha madhira ya awamu ya tano. Gari hiyo itembezwe mitaa yote ambako mikutano inatarajiwa kufanyika, wananchi wayaone matundu ya risasi, halafu waamue wenyewe kuhusu awamu ya tano, na walinganishe na awamu ya SSH ambayo Lissu anazurura huku na kule akimtukana kwa uzanzibari wake

Pili, Lissu asipande gari hilo, kwa kuwa tayari lomeshaingia nuksi, ni sawa na jeneza.
Hoja ya kipumbavu ya mwaka...
Kwamba hamna hoja za kuwasilisha kwa wananchi??
Kwamba mpinzani sio samia bali ni magufuli??
WHat a lame dude!!
Sababu mojawapo upinzani unazidi kupotea licha ya kwamba kuna fursa ni mawazo kama haya... hii inatoka kwa wafuasi wengi wa upinzani mpaka viongozi... mentality ya kuwa defeated...
MKitumia hoja ya kumchafua magufuli ni mnamfanyia kampeni sisiemu...
 
kwamba kila aliyeuawa kipindi cha utawala wa jpm bas jpm ndo alikuwa anahusika ?
Wanaombebesha madhambi JPM ni wale waliokuwa wakwepa kodi enzi za utawala wa JPM, walipigwa kote kote kwa sababu JPM hakucheka na wezi ama wakwepa kodi.

Baada ya kufa kwa JPM mama akawarudishia ulaji wao hao wakwepa kodi, na ndio wanakula mema yote ya nchi hii na kodi hawalipi.

Na ndio hao hao wanaoimba mapambio eti JPM alikuwa muuaji.

Wasilolijua hao wahuni ni hili za siku zao kuhesabiwa.
 
Hoja ya kipumbavu ya mwaka...
Kwamba hamna hoja za kuwasilisha kwa wananchi??
Kwamba mpinzani sio samia bali ni magufuli??
WHat a lame dude!!
Sababu mojawapo upinzani unazidi kupotea licha ya kwamba kuna fursa ni mawazo kama haya... hii inatoka kwa wafuasi wengi wa upinzani mpaka viongozi... mentality ya kuwa defeated...
MKitumia hoja ya kumchafua magufuli ni mnamfanyia kampeni sisiemu...
Mbona umepandwa jazba kama umeibiwa shilingi mia na kondakta wa daladala?Umeambiwa kwamba wawe na paredi ya kutembeza gari tu bila kuongea hoja?Tulia na ufikirie.
 
Sasa mbona unaikimbia hoja? Umeulizwa kwamba viongozi wa Sasa wamemuua nani?
unaitaj maombi asee , mambo yote haya yaliyotokea ndan ya miaka 3 bado unataka kufungulia macho ? wasanii kukimbia nchi , wakosoaji kuvuliwa nyadhifa zao , wengine kupewa kesi za uhaini ( kifungo cha maisha au kunyongwa kabisa ) , wamasai kuuliwa kisa wanapigania ardhi zao , kufunguliwa maji ya bwawa la umeme yalioua makumi ya watu ili tu kuonesha JP alijenga bwawa nje ya ubora , Kupora machinga biashara zao ilihali watu wanaiba 42B bado wanaombwa kujiuzuru na hawafanyi hivyo , mfumuko wa bei za vitu , mlipuko wa panya road walioua makumi ya watu , uporaji wa maeneo ya watu na ugawaji wa maliasilI za nchi kwa mikataba mibovu , rushwa imelithiri hasa vituo vya polisi na vituo vya afya , upigaji wa kodi zetu yaan kidaraja cha 20M wanatumia 200M yaan chumba cha mlinzi cha 5M wanatumia 11M yaan kidimbwi cha kuchimba kwa 600K wanasema wamejenga kwa 600M halaf hakijasakafiwa

Kiufupi ndan ya miaka hii 3 tumeona uborongaji mwingi sana yakiwemo mauaji pia ya direct na indirect
 
Kwani mimi ukisema kuwa ni Msukuma nao ni ukabila?
Kuna haja gan ya kumtambua mtu kwa kabila lake ? je kabila lake linahusiana vipi na matendo yake ? je ni kwel Tanzania kuna wahutu ? je huoni umefikia hatua ya kumvua uraia ? je ukishitakiwa utasema wanatumia madaraka yao ?
 
Kwa umbumbumbu huu ndiyo maana vijana tutabaki kuwa watazamaji tu.
Umbumbumbu ni jadi ya wabongo, wewe ukiwa miongoni mwao wabongo mbumbumbu nenda ukamsabahi robot Eunice pale bungeni mbumbumbu wa haja wewe.
Wazee wataendelea kukalia viti vya uongozi.
Unataka kusema hata kikwete jr ni mzee? Acha ufala ndugu
Vijana wengi ni weupe kichwani.

Unaambiwa tetea hoja yako huwezi.
Hao vijana weupe kichwani imekuwaje wakawa madarakani, mtu kama Nape ni mweupe kabisa kichwani Ila anatembelea V8 huku akisalimiana na Eunice pale bungeni 😂😂

Wewe ni mfu unaye tembea
 
Attachments

  • 1715969438082.jpg
    1715969438082.jpg
    395.5 KB · Views: 1
unaitaj maombi asee , mambo yote haya yaliyotokea ndan ya miaka 3 bado unataka kufungulia macho ? wasanii kukimbia nchi , wakosoaji kuvuliwa nyadhifa zao , wengine kupewa kesi za uhaini ( kifungo cha maisha au kunyongwa kabisa ) , wamasai kuuliwa kisa wanapigania ardhi zao , kufunguliwa maji ya bwawa la umeme yalioua makumi ya watu ili tu kuonesha JP alijenga bwawa nje ya ubora , Kupora machinga biashara zao ilihali watu wanaiba 42B bado wanaombwa kujiuzuru na hawafanyi hivyo , mfumuko wa bei za vitu , mlipuko wa panya road walioua makumi ya watu , uporaji wa maeneo ya watu na ugawaji wa maliasilI za nchi kwa mikataba mibovu , rushwa imelithiri hasa vituo vya polisi na vituo vya afya , upigaji wa kodi zetu yaan kidaraja cha 20M wanatumia 200M yaan chumba cha mlinzi cha 5M wanatumia 11M yaan kidimbwi cha kuchimba kwa 600K wanasema wamejenga kwa 600M halaf hakijasakafiwa

Kiufupi ndan ya miaka hii 3 tumeona uborongaji mwingi sana yakiwemo mauaji pia ya direct na indirect
Chiembe hebu njoo usome huu uozo wa unaodai hawajawahi kuwa makatili
 
Matukio ya mauaji dhidi ya wakosoaji wa Serikali, yalimharibia sana marehemu. Huyu amekwishatangulia mbele za haki, na hukumu au msamaha wake siyo wa Ulimwengu huu, bali wa aliyemuumba.

Tunachotakiwa kuhoji zaidi ni hawa tulio nao hai mpaka sasa, na Serikali ya awamu ya 6 haijawahi kuwafanya chochote kuhusiana na uovu walioutenda.

Aliyepanga na kusimamia tukio lile yupo hai. Awamu ya sita kama kweli inauchukia uovu kwa nini huyu bwana hajakamatwa na kufikishwa kwenye vyombo vya sheria? Kumzawadia ukuu wa mkoa si ina maana hata awamu hii inaunga mkono uovu aliotendewa Lisu na wengineo? Yule ambaye alikuwa ndiyo mkono wa uovu wa Bashite, bado yupo hai, na kule Lindi akamwua mfanyabiashara ndugu yake PM, kwa sasa yupo jela lakini kama awamu hii ni ya watu wema, mbona hajawahi kushitakiwa kwa uovu alioute da dhidi ya Lisu? Kuwezesha uovu au kuficha taarifa za uovu, ni kosa la jinai. Mbona Kalemani aliyeondoa camera za CCTV, hajawahi kuhojiwa wala kushtakiwa kwa kushiriki kuficha taarifa za uovu?

Ni ngumu sana kudai au kuamini kuwa awamu hii ni ya haki, labda tuseme tu kuwa ina uafadhali.
 
Wanaombebesha madhambi JPM ni wale waliokuwa wakwepa kodi enzi za utawala wa JPM, walipigwa kote kote kwa sababu JPM hakucheka na wezi ama wakwepa kodi.

Baada ya kufa kwa JPM mama akawarudishia ulaji wao hao wakwepa kodi, na ndio wanakula mema yote ya nchi hii na kodi hawalipi.

Na ndio hao hao wanaoimba mapambio eti JPM alikuwa muuaji.

Wasilolijua hao wahuni ni hili za siku zao kuhesabiwa.
Huyo mtu wenu alikuwa muuaji kwa asili ya kabila lao la wahutu. Tunashuru tu kuwa corona ilitusaidia watanzania kuliondoa lile jinamizi.
 
Back
Top Bottom