Gari yangu inakimbia sana!

Gari yangu inakimbia sana!

Kuna project naisimamia pale Kibaha Mailimoja. Kwahiyo route za kutoka Makongo Juu kwenda Kibaha na kurudi daily hazikatiki. Zile njia sita kutoka Kimara hadi Mailimoja zimenipa nafasi kujua kumbe gari yangu inakimbia mazee.

Gari yenyewe ujue ni gari gani basi?

Ni Passo Racy, 1290CC. Ni ya mwaka 2007.

Kwa data nilizonazo (kwa kipindi cha miezi mitatu), nimegundua yafuatayo:

A: Gari nazozionea road, nawakimbiza nawaachia vumbi:
  • IST zote
  • Sienta, Raum, Runx, Allex, Swift, Nadia, Voltz (tuseme babywoka zote za Toyota)
  • Premio na mwenzie Allion
  • Nissan Dualis na X-trail
  • Rumion
  • RAV4 zote (isipokua lile toleo jipya linatumiwa na gari za serikali na ile Hybrid)

B: Gari ambazo nimeshindwa kufukuzana nazo:
  • Subaru Forester (model karibu zote)
  • Ford Ranger (hii gari noma)
  • Toyota Hilux
  • Landcruiser (VX na jamii yake)
  • ALPHARD (toleo jipya)
  • Toyota Fortune
  • Discovery
  • BMW (japo kuna baadhi navimbiana nao)
  • Toyota Crown
  • Brevis
C: Gari nazokwenda nazo ugoko kwa ugoko:
  • Harrier na Vanguard
  • Range Rover
  • Subaru Impreza

Sasa hivi focus yangu nijipime na kina Audi, Benz, Volkswagen and the like. Tatizo European cars nazokutana nazo barabarani ni chache sana. Halafu huwa nakutana nazo mida ambayo sipo kwenye kuanzisha ligi.

Changamoto nayopata ni gari inachelewa kuchanganya. Hasa pale taa zikiruhusu ndio wengi wanaponipiga bao. Lakini ikishachanganya nawapoteza karibu wote (ukitoa hao wa kwenye kundi B).

View attachment 2738606
Kuna Mwenzio huku nae alikua anaamini gari lake Toyota Noah ndio mambo yote na alikua mbishi sana lakini siku alipopigwa tukio na Audi Q7 ndo alijua kumbe anaendesha jenereta lenye matairi.[emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Mkuu hilo jina lako linaonesha wewe ni mnazi wa Werrason kama mimi.
ile live performance ya zenith 2002 ndo ilinifanya nianze kuchimba na kumfuatilia jamaa ailiuwasha sana akiwa na kundi lake lenye wababe kama, baby ndombe, aimelia lias,heritier watanabe, ferre gola,kabose bulembi, jdt mulopwe ,bill clinton,celeo scram, ali mbonda (tumba),kapaya flamme(solo gitar), papy kakol (drums)
 
BMW (japo kuna baadhi navimbiana nao)
Kwanini Toyota huwa mnataja model ila other mnataja maker tu ? Au hamjui bmw nao Wana vigari vya under 1300cc


Unavosema Alphard toleo jipya kwani ya zamani unaweza fatana nayo ?
Nikwambie tu hako ka gari chako kanaliwa vizuri na 1NZ ikiwa kwenye body lolote, iwe premio, IST, rumion nk
 


Anacho hicho kigari toka 2020 ..alisema January ananunua Forester kashindwa Sasa kaamua kuja isifia
 
Back
Top Bottom