Gaudensia Kabaka Mwenyekiti wa UWT?

Sijawawahi kuona mwalimu anayefundisha mambo kwa bias. Usifundishe kinachokufurahisha wewe fundisha kinachofanya jamii ielewe kwa mapana yake.
Jones...
Umekuwa mwepesi wa kulaumu.
Wapi ilipo bias?

Nashangaa kuwa hushangai imekuwaje mtu kama Abdul Sykes na udugu na urafiki huu na mchango wake kwa Nyerere hatajwi katika historia si ya Nyerere wala ya TANU?

Unadhani mimi nafurahi kutukanwa na kukejeliwa hapa?
Mimi nakupeni historia iliyofutwa na ikapotea kabisa.

Haya ninayokusomesha wewe ulikuwa ukiyajua?
Picha za 1955 za Bi. Chiku, Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee unajua nilikozipata?

Hizi picha nimezitoa kwa Jim Bailey ziko katika Jim Bailey Collection Johannesburg.
Huyu Jim Bailey ndiye owner wa jarida la Drum lilikuwa gazeti maarufu sana katika 1950s.

Ally Sykes ndiye aliyenijulisha kwa Jim Bailey.
Ukiondoa hii historia katika historia ya Tanganyika hakuna tena kitu.
 
Islamic slavery and colonial mentality. Ukiwa mwafrika unawezaje kujidai na imani yacwadhalimu wa kiarabu na kizungu. Si haba kuona watu hawana majina ya kilugha eti na wao wana makabila duuh.
 
Mapinduzi ya harakati za uhuru, za siasa na utawala baada ya uhuru, a.k.a usaliti sasa swali kwa nini mwinyi au kikwete hawajapigania na kuwezesha hili la uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika, maisha baada ya Azimio la Arusha 67, CCM 77 na Muungano 64. Kama kuna hofu ya inflamatory instigations basi mambo yaachwe sirini au yawasilishwa by impartiality.
 
Galileo...
Ikiwa umenikusudia mimi swali hilo basi mimi siwezi kuwajibia hao uliowataja.
 
Galileo,
Nimefanya provocation mtambuka kwa ajili ya fikra tu. Kuna mengi zaidi.
Galileo...
Nilimpa Mzee Ali Hassan Mwinyi nakala ya kitabu cha Abdul Sykes cha Kiingereza na cha Kiswahili Ukumbi wa Korea mwaka wa 2014.

 
Salamu,

Hivi karibuni Uongozi wa JF ulimpa tuzo mwandishi Mohamed Said ambaye ni maarufu Sana hapa JF kwa kuandika Historia ya TANU ,Tanganyikana Zanzibar.

Mzee Mohamed amekuwa akiandika historia hii kwa kile ambacho amekuwa akibainisha kuwa Historia ya TANU na Tanganyika imekuwa ikipotoshwa makusudi kwa kutowataja baadhi ya Waasisi ambao yeye anawaita wazee wake.

Bila woga wala hofu Mzee Mohamed amekuwa akieleza kuwa Historia hiyo imefutwa kwa kuwa hao Wazee ni Waislam.

Na katika maandishi hayo pia Mzee Mohamed ameeleza jinsi Waislam walivyodidimizwa Kielimu ambapo ameeleza kuwa ni kundi dogo tu la Waislam,wamekuwa\walikuwa wanachaguliwa kujiunga na Sekondari(yeye ameita 20:80)

Mzee huyu amediriki kuelezea (kwa Lugha ya kebehi) jinsi Mwalimu Nyerere alivosaidiwa ' na hao Wazee wake wakati anadai Uhuru. Kwa maneno mengine Nyerere hakulipa fadhira

Kimsingi ameandika mengi katika Uzi wake wa mwisho ambao umezua mjadala mkubwa ameeleza inakuwaje Mwenyekiti wa UWT, Mama G. Kabaka alipewa nafasi hiyo ,ilhali alishiriki kuwanyanyasa Waislam alipokuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Cha Dodoma kwa kukataa kujengwa kwa Msikiti eneo la Chuo.

Hizi no shutuma nzito kwa Serikali, CCM na Mama Kabaka Mwenyewe. Shutuma hizi zingetolewa na layman' zingewezwa kupuuzwa. Lakini zinapotolewa na Msomi,Inatia mashaka. Ilhali anaelewa kabisa namna Maamuzi ya Taasisi kama UDOM wanavyotolewa.

Lengo lake Nini!
Inawezekana Kuna kasoro katika Historia ya TANU, lakini kwa namna anavyoeleza Ndg Said kwa misingi ya Ubaguzi wa Kidini inakera.

Turudi kwenye mada, hivi Uonhozi wa JamiiForums haukuona Viashiria vya Ubaguzi vilivyomo kwenye simulizi zake hadi wakafumba macho Hadi kumpa Tuzo!? Au Viashiria hivi ni vidogo kulinganisha na Elimu anayoitoa kwa Jamii?

Mimi kwangu Viashiria hivi ni sumu katika Jamii.

Rejea mjadala katika Uzi wake kuhusu Mama Gaudensia Kabala katika jukwaa la Historia.
 
Watanzania tulio wengi hatuna utaratibu wa kuchimbua mambo tupo mstari wa mbele kukosoa matokeo ya walnayosema wengine

Hii nchi ukiisoma historia yake kama wewe ni muislamu utabaki unaumia roho tu ila kama wewe ni mkrsto hutaumia chochote zaidi ya hapo utaona walioandika ni wabaguzi wa kidini
 
 
Huyo mzee huwa nasoma mada zake naishia kuguna tu, inshort huyu mzee ajitafakari upya kwa kile anachoandika humu.
 
As long hajavunja sheria za nchi sio tatizo. Mzee Said anareclaim the forgotten/deleted history
 
Yuko sahihi acha kua na fikra nyepesi

Mohamed yuko sahihi kwa kumzushia mama Gaudensia Kabaka kama mweyekiti wa UDOM kuwa alitoa uamuzi peke yake kwa kuzingatia udini? Taasisi haziendeshwi hivyo, huo ni uchochezi wa muandishi.
 
Lombo,
Nakushukuru sana kwa makala hii yako.

Hakika umenisaidia pakubwa kwa kujaribu kuwagutusha wenye mamlaka. juu yetu kuhusu wajibu wao katika yale ambayo mimi nimekuwa nikiyapigania.

Nakupinga kusema kuwa nimekuwa nikiandika kwa kebehi historia ya Mwalimu Nyerere na jinsi alivyopokewa na wazee wangu.

Katika hili naomba kama unao ushahidi uweke hapa hayo maneno ya kebehi kutoka kwenye kalamu yangu.

Nataka nikusaidie uelewe vizuri historia ya elimu na matatizo yaliyowafika Waislam kuanzia mwaka wa 1961 Tanganyika ilipopata uhuru wake:

1968 EAMWS ilivunjwa na serikali ili kuondoa uwezekano wa kuendelea na mipango ya elimu na ujenzi wa Chuo Kikuu.

Miaka ya 1970s Organisation of Islamic Conference (OIC)ilitaka kujenga Chuo Kikuu Tanzania serikali ikakataa kutoa kibali.

OIC ikajenga chuo hicho Mbale Uganda.

1981 Warsha wakiwa ndani ya BAKWATA kwa kujipenyeza waligeuza baadhi ya shule za Kiislam kuwa seminari ili kuboresha shule hizo.

Serikali iliingilia mchakato huu na shule zile zikarejeshwa katika hali yake ya zamani.

Mambo hayakuishia hapo.

Vijana wa Warsha waliojipenyeza BAKWATA wakafukuzwa BAKWATA kwa amri ya serikali na kupigwa marufuku kuongoza taasisi yeyote ya Kiislam nchini.

Mlezi wa Warsha Sheikh Hussein Malik akafukuzwa nchini.

Warsha haikuvunjiks moyo wakajenga shule Masjid Quba serikali ikakataa kuipa tasjila.

Warsha wakaendesha shule hivyo hadi Prof. Malima akiwa Waziri wa Elimu alipoipa tasjila.

Mwaka wa 1987 Prof. Malima akiwa Waziri wa kwanza Muislam kuongoza Wizara ya Elimu aligundua yaliyokuwa yakifanyika ndani ya wizara hiyo na akamtaarifu Rais Ali Hassan Mwinyi.

Prof. Malima akaondolewa katika wizara hiyo baada ya kikao cha CCM Dodoma.

Miaka ya 1980s Darul Iman kutoka Saudi Arabia ilitaka kujenga shule ya ufundi Kibaha.

Kama kawaida njama zikapita.
Darul Iman wakaufuta mradi na kuondoka nchini.

Yako mengi pamoja na matatizo ya NECTA nk. nk.

Nasikitika hukuwa unayajua haya kwa hiyo hukuweza kuyafikisha kwa wahusika.

Nakubaliana na wewe kuhusu sumu kwa jamii.

Lakini sumu hii haikorogwi wala kupikwa na Waislam.

Kuhusu tuzo ya JF hili naona limekuchoma sana maana umekuwa ukilirejea.

Nina tuzo mbili kabla, hii ya JF ni ya tatu.

Hayo mengine naona niyanyamazie kwa sasa.

Ikitokea fursa In Shaa Allah tutayazungumza.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…