Reginald L. Ishala
JF-Expert Member
- Jun 18, 2011
- 3,810
- 6,789
Madaraka na utamu wake
Follow along with the video below to see how to install our site as a web app on your home screen.
Note: This feature may not be available in some browsers.
Jones...Sijawawahi kuona mwalimu anayefundisha mambo kwa bias. Usifundishe kinachokufurahisha wewe fundisha kinachofanya jamii ielewe kwa mapana yake.
Islamic slavery and colonial mentality. Ukiwa mwafrika unawezaje kujidai na imani yacwadhalimu wa kiarabu na kizungu. Si haba kuona watu hawana majina ya kilugha eti na wao wana makabila duuh.GAUDENSIA KABAKA MWENYEKITI WA UWT?
Mwenyekiti wa UWT Gaudensia Kabaka ndiye aliyehusika kuwafukuza Waislam 11 Chuo Kikuu cha Dodoma na kusimamisha ujenzi wa msikiti hapo chuoni ambao ujenzi wake ulishaidhinishwa.
Leo yupo katika sherehe za kumuenzi Bi. Titi Mohamed.
Huyu ndiye kiongozi aliyewafukuza wajukuu wa Bi. Titi hapo chuoni na kuzuia ujenzi wa msikiti.
Kwa yale aliyopigania Bi. Titi Mohamed na wanawake wote katika TANU ya enzi zile huu ni msiba mkubwa.
Huyu Mama hastahili kuongoza wala kunasibishwa na umoja huu ulioasisiwa na mama zetu akina Bi. Titi, Bi. Hawa bint Maftah, Bi. Zarula bint Abdulrahman kwa kuwataja wachache.
Angalieni picha hiyo ya kwanza hapo chini pcha iliyopigwa na Mohamed Shebe ya mkutano wa TANU 1955 wakati wazee wetu wanautafuta uhuru wa Tanganyika.
Angalia huo umma Viwanja Vya Mnazi Mmoja na tazama hiyo sehemu nyeusi.
Hayo ni mabaibui ya bibi. mama, na shangazi zetu wamekuja kuujaza uwanja na kumtia nguvu Mwalimu Nyerere.
Mama zetu wameitika mwito wa "kuno kuno."
Hapo ndipo walipokuwa wakiimba nyimbo za lelemama kuhamsisha wakiimba."
Muheshimiwa nakupenda sana....Insha Allah Mungu yupo Tanganyika tutajitawala.''
Tujitawale halafu iwe nini?
Gaudensia anyanyase Waislam, Gaudensia avunje misikiti yetu?
Gaudensia awafukuze chuoni wajukuu wa hawa wanawake unaowaona hapo chini kwenye picha?
Picha ya pili hao wote mbele hapo wanaongoza maandamano ya akina mama mimi mama zangu.
Hao ndiyo msingi wa UWT.
Yupo Bi. Mwamvua bint Mrisho (Mama Daisy), Bi. Titi Mohamed na Bi. Zainab Tewa.
Mapinduzi ya harakati za uhuru, za siasa na utawala baada ya uhuru, a.k.a usaliti sasa swali kwa nini mwinyi au kikwete hawajapigania na kuwezesha hili la uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika, maisha baada ya Azimio la Arusha 67, CCM 77 na Muungano 64. Kama kuna hofu ya inflamatory instigations basi mambo yaachwe sirini au yawasilishwa by impartiality.Jones...
Umekuwa mwepesi wa kulaumu.
Wapi ilipo bias?
Nashangaa kuwa hushangai imekuwaje mtu kama Abdul Sykes na udugu na urafiki huu na mchango wake kwa Nyerere hatajwi katika historia si ya Nyerere wala ya TANU?
Unadhani mimi nafurahi kutukanwa na kukejeliwa hapa?
Mimi nakupeni historia iliyofutwa na ikapotea kabisa.
Haya ninayokusomesha wewe ulikuwa ukiyajua?
Picha za 1955 za Bi. Chiku, Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee unajua nilikozipata?
Hizi picha nimezitoa kwa Jim Bailey ziko katika Jim Bailey Collection Johannesburg.
Huyu Jim Bailey ndiye owner wa jarida la Drum lilikuwa gazeti maarufu sana katika 1950s.
Ally Sykes ndiye aliyenijulisha kwa Jim Bailey.
Ukiondoa hii historia katika historia ya Tanganyika hakuna tena kitu.
Galileo...Mapinduzi ya harakati za uhuru, za siasa na utawala baada ya uhuru, a.k.a usaliti sasa swali kwa nini mwinyi au kikwete hawajapigania na kuwezesha hili la uandishi wa historia ya uhuru wa Tanganyika, maisha baada ya Azimio la Arusha 67, CCM 77 na Muungano 64. Kama kuna hofu ya inflamatory instigations basi mambo yaachwe sirini au yawasilishwa by impartiality.
Nimefanya provocation mtambuka kwa ajili ya fikra tu. Kuna mengi zaidi.Galileo...
Ikiwa umenikusudia mimi swali hilo basi mimi siwezi kuwajibia hao uliowataja.
Galileo...Nimefanya provocation mtambuka kwa ajili ya fikra tu. Kuna mengi zaidi.
Mzee Ajitafakari Upya
Yuko sahihi acha kua na fikra nyepesiMzee Ajitafakari Upya
Watanzania tulio wengi hatuna utaratibu wa kuchimbua mambo tupo mstari wa mbele kukosoa matokeo ya waliosema wengine
Hii nchi ukiisoma historia yake kama wewe ni muislamu utabaki unaumia roho tu ila kama wewe ni mkrsto hutaumia chochote zaidi ya hapo utaona walioandika ni wabaguzi wa kidini
Yuko sahihi acha kua na fikra nyepesi
Lombo,Salamu,
Hivi karibuni Uongozi wa JF ulimpa tuzo mwandishi Mohamed Said ambaye ni maarufu Sana hapa JF kwa kuandika Historia ya TANU ,Tanganyikana Zanzibar.
Mzee Mohamed amekuwa akiandika historia hii kwa kile ambacho amekuwa akibainisha kuwa Historia ya TANU na Tanganyika imekuwa ikipotoshwa makusudi kwa kutowataja baadhi ya Waasisi ambao yeye anawaita wazee wake.
Bila woga wala hofu Mzee Mohamed amekuwa akieleza kuwa Historia hiyo imefutwa kwa kuwa hao Wazee ni Waislam.
Na katika maandishi hayo pia Mzee Mohamed ameeleza jinsi Waislam walivyodidimizwa Kielimu ambapo ameeleza kuwa ni kundi dogo tu la Waislam,wamekuwa\walikuwa wanachaguliwa kujiunga na Sekondari(yeye ameita 20:80)
Mzee huyu amediriki kuelezea (kwa Lugha ya kebehi) jinsi Mwalimu Nyerere alivosaidiwa ' na hao Wazee wake wakati anadai Uhuru. Kwa maneno mengine Nyerere hakulipa fadhira
Kimsingi ameandika mengi katika Uzi wake wa mwisho ambao umezua mjadala mkubwa ameeleza inakuwaje Mwenyekiti wa UWT, Mama G. Kabaka alipewa nafasi hiyo ,ilhali alishiriki kuwanyanyasa Waislam alipokuwa Mwenyekiti wa Baraza la Chuo Cha Dodoma kwa kukataa kujengwa kwa Msikiti eneo la Chuo.
Hizi no shutuma nzito kwa Serikali, CCM na Mama Kabaka Mwenyewe. Shutuma hizi zingetolewa na layman' zingewezwa kupuuzwa. Lakini zinapotolewa na Msomi,Inatia mashaka. Ilhali anaelewa kabisa namna Maamuzi ya Taasisi kama UDOM wanavyotolewa.
Lengo lake Nini!
Inawezekana Kuna kasoro katika Historia ya TANU, lakini kwa namna anavyoeleza Ndg Said kwa misingi ya Ubaguzi wa Kidini inakera.
Turudi kwenye mada, hivi Uonhozi wa JamiiForums haukuona Viashiria vya Ubaguzi vilivyomo kwenye simulizi zake hadi wakafumba macho Hadi kumpa Tuzo!? Au Viashiria hivi ni vidogo kulinganisha na Elimu anayoitoa kwa Jamii?
Mimi kwangu Viashiria hivi ni sumu katika Jamii.
Rejea mjadala katika Uzi wake kuhusu Mama Gaudensia Kabala katika jukwaa la Historia.
Ahsante sana.As long hajavunja sheria za nchi sio tatizo. Mzee Said anareclaim the forgotten/deleted history