Kumradhi Mohamed Said, ni kweli nimeghadhibika sana na maelezo yako ya uzandiki na uchochezi kuhusu Bibi Titi, Gaudencia Kabaka na Suala la Msikiti pale UDOM!
Tunamwomba sana Mwenyezi Mungu kwamba kizazi chenye mawazo hasi na primitive kama wewe kiishe haraka katika Nchi yetu ili Taifa hili lije kupumua!
Wewe Mohamed Said ni mtu mdini , mwenye maarifa madogo sana na mwenye chuki iliyopitiliza dhidi ya Hayati Julius Kambarage Nyerere na harakati zake za kudai Uhuru wa Tanganyika.
Siku zote unataka wajinga wenzio wamwone Julius Nyerere kama mtu mshamba ambaye alifika Dar es Salaam hajui chochote na isingekuwa hao Wazee wako wa Kiislamu wa Dar es Salaam kumpokea asingekuwa chochote!
Unachosahau au ambacho hujui na hutaki kujifunza ni kwamba hata kabla ya kuja Dar es Salaam, Julius Kambarage Nyerere alikuwa ni kijana wa Chifu Burito wa Wazanaki kule Butiama na katika makuzi yake ya utoto alianza kupata hisia za uongozi kutoka kwa baba yake Chifu Burito na jinsi utawala wa kikoloni ulivyokuwa uki- operate!
Nadhani muda huo Wazee wako hao ambao mimi binafsi nawapenda na kuwaheshimu kwa mawazo yao na hawakuwa wadini na wajinga kama wewe hawakuwa na mikakati imara ya kudai Uhuru mpaka akina Dossa Azizi walipokutana na kijana mahiri na Mwalimu wa Sekondari ya St. Francis kama sikosei (Pugu Sekondari leo) Julius Kambarage Nyerere na wao kumtambulisha kwa Wazee wao.
Tambua kuwa muda huo Julius Nyerere alishatoka Makerere University Uganda, ameshasoma Tabora School ( Ambako pia nilisoma mimi Fumadilu Kalimanzila) na kuacha rekodi mbalimbali kama kijana shupavu na mwenye maono ya mbali kuhusu utawala wa kikoloni .
Wewe Said Mohamed hujui chochote zaidi ya kuokoteza "vistory" vya kwenye kahawa hapo Kariakoo na "tu- picha" twa zamani kutoka kwa familia za hao Wazee wa Kiislamu wa zamani hapo Mzizima na kuenezea UDINI WAKO!!!