Gaudensia Kabaka Mwenyekiti wa UWT?

Saint,
Suala hili si la kujadiliwa na lugha za kejeli za "lialia."

Serikali inajua tatizo hili na iko kimya.

Kwa sababu maalum.

Soma historia ya uhuru wa Tanganyika kuna mengi utajifunza.

Ndipo unaweza ukawa na maarifa ya kukusaidia kujadili.
Mzee wetu kubali kuwa hapa umekosea. Wewe ni binadamu, na kukosea ni kawaida. Ila uungwana ni kukiri kuwa umeteleza. Kwa umri wako hukutakiwa kuendekeza kauli za ubaguzi na uchochezi wa kidini namna hii.
Umefeli sana hapa mzee wetu
 
Halafu na nyie msiwe mnasema tu waislamu wamefukuzwa. Unajua vyeti vya hao jamaa vilikuwaje? Msiwe mnanunua ugomvi wa vitu msivyovijua ambavyo wahanga wanakuja kupiga kelele za uongo misikitini.

Unajua wakristo wangapi na waislamu wangapi walikuwa na vyeti fake na wakaondolewa kwenye ajira? Au kwa sababu ni chuo kikuu cha Dodoma ndio kelele kubwa? Unajua hao ndugu zako baadhi walihamia vyuo vingine wakakataliwa kwa sababu ya utata wa vyeti? Wakati mwingine tangaza dini tu.
 
Huwa napenda kufuatilia mada zako nzuri kuhusu historia ambayo huwa imejaa ukweli mwingi lakini huwa ninakwazika sana na wewe na kuwa na mashaka na credibility yako pale ambapo UNAGEUZA HARAKATI ZAKO ZA UDINI ki ukweli huwa ukifikia hapo ninakuona ni msomi ASIYE NA AKILI ZA KUZALIWA
 
Una udini balaa na unachofanya ni kujificha nyuma bibi Tit, nikukumbushe tu bibi Tit hakuwa anapigania udini Bali uhuru
Tk...
Hakika soma mchango wa masheikh waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika utajifunza mengi.

Sina sababu ya kujificha.
Jina langu liko hapa.

Uliyejificha ni wewe.
Nini kinakutisha?
 
Halafu eti Jamii Forum walimpa huyu Babu Tuzo...!
Yaani hoja ya kipuuzi kabisa...Kwani mama Kabaka ndiye mmiloki ya UDOM!
UJINGA MTUPU..
 
Mbona unaficha ukweli kwamba huyo Bi Titi alishiriki kutaka kuipindua Serikali akakamatwa na kushtakiwa kwa kosa ya uhaini na wenzie na kufungwa kabla ya kupewa msamaha na Nyerere?


Soma history vizuri..
Hawakutaka kupindua serikali ..
Walibambikiziwa kesi kwa kutofautiana na Nyerere....
Bibi Titi alipachikwa tu kwa kesi ambayo hata haijui..
 
Fuma...
Udini ni kukandamiza wale wasiokuwa imani yako na kuwanyanyua wale wa imani yako.
Unaijua hali ya Waislam wa Tanzania katika elimu?

Unaijua historia yake?
Soma historia hii utarudi hapo kujadili kwa adabu na heshima wala hutatukana.

Utatambua kuwa lipo tatizo.

Prof. Hamza Mustafa Njozi baada ya Rais Mkapa kutaka apewe ushahidi wa kisayansi Njozi aliandika kitabu, ''Mwembechai Killings...''

Yaliyomo ndani ya kitabu hiki ulitisha serikali.
Iliamua kukipiga marufuku kitabu.

Waliokipiga kitabu marufuku si Waislam kwani wanapenda tatizo hili liwe wazi na lijadiliwe kwa amani na salama ili haki itendeke.

Tatizo hili linataka ujuzi si matusi.
 
Tk...
Hakika soma mchango wa masheikh waliokuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru wa Tanganyika utajifuunza mengi.

Sina saabu ya kujificha.
Jina langu liko hapa.

Uliyejificha ni wewe.
Nini kinakutisha?
Hivi kwani so walipigania Uhuru ili iweje!
Hawaapo kwenye Taifa Huru!
Kwa ujinga Kuna watu walikiwa wanapigania Uhuru wakifikiri wanapingana na Ukristo(wa Wazungu)😂
 
Halafu eti Jamii Forum walimpa huyu Babu Tuzo...!
Yaani hoja ya kipuuzi kabisa...Kwani mama Kabaka ndiye mmiloki ya UDOM!
UJINGA MTUPU..
Lombo,
Soma kitabu cha Njozi, ''Mwembechai Killings..."

Yapo mengi ya utajifunza na utakuwa na maarifa ya kuelewa kwa nini Gaudensia Kabaka hakuwa na hofu na uamuzi wake na kwa nini BAKWATA imekuwa kimya hadi leo licha ya Waislam kuwaomba walishughulikie tatizo lile.
 
Hivi kwani so walipigania Uhuru ili iweje!
Hawaapo kwenye Taifa Huru!
Kwa ujinga Kuna watu walikiwa wanapigania Uhuru wakifikiri wanapingana na Ukristo(wa Wazungu)😂
Lombo,
Walipigania uhuru kuondoa dhulma za wakoloni.
Umesoma kitabu cha Abdul Sykes?

Kama bado soma kitabu hiki kina mengi muhimu kufahamu.
 
Kuna mambo mengine hayataki ligi. Fika Mzumbe University, pale kuna kanisa na wamepewa mpaka eneo la kujenga shule ilhali waislamu wanaswali Mzumbe Secondary School.
 
Did...
Ikiwa wamefukuzwa kwa ajili ya kukosa sifa hapo hakuna tatizo lakini hebu tuwekee hapa ili ukwelii ujulikane na ubishi umalizike.

Hili la wao kufukuzwa na msikiti kuvunywa nalo vipi?
Ule msingi ulikuwa chini ya viwango?
 
Did...
Ikiwa wamefukuzwa kwa ajili ya kukosa sifa hapo hakuna tatizo lakini hebu tuwekee hapa ili ukwelii ujulikane na ubishi umalizike.

Hili la wao kufukuzwa na msikiti kuvunywa nalo vipi?
Ule msingi ulikuwa chini ya viwango?
Niweke mimi, au waweke waliolalamika sifa walizonazo na kwamba walionewa.
 
Niweke mimi, au waweke waliolalamika sifa walizonazo na kwamba walionewa.
Did...
Kwa kuwa wewe umeeleza vyema hili tatizo hapa niliamini kuwa unazo taarifa.
La huna hizo taarifa si kitu na kwa kuwa hao uliowasema hawako hapa JF hakuna shida.
 
Mzee Mohamed;
Yupo Rais wa Nchi,Muislamu,Yupo Waziri mkuu,Muislamu,Ipo serikali ya ZNZ full waislamu.Sijajua ubaguzi unaolalamikia na upi kama sio frustration zako tu za kutokukubali kwamba kuna wakati waislamu wanachanganya ajenda za maendeleo ya kitaifa na ajenda za kidini ambapo matokeo yake huwa ni mabaya kwa uislamu na kwa nchi.

Hata katika ukristo pia wakichanganya mafaili huwa wanaisoma namba.

Binafsi nataka nikukumbuke kama mwanahistoria mahiri lakini naona sasa unatamani kuitwa mchochezi ingawa kwa maandiko yako naona bado hujapata ujasiri wala uwezo wa kuwa mchochezi.Zaidi unaonekana kutotaka kuwatendea haki waislamu wenzako.
 
Saidi
Shikamoo!

Huo msikiti ulikua unajengwa na Udom ama nani? Nieleweshe mzee.

Ninavofahamu kiiwanja cha Udom ni cha Serikali na Serikali ndiye aliyejenga Udom kwenye kiwanja chake na viunga vyote vile vimejengwa na Serikali, waislam walitaka Serikali iwajengee msikiti ama? Nieleweshe mzee wangu.
 
Mzee wetu kubali kuwa hapa umekosea. Wewe ni binadamu, na kukosea ni kawaida. Ila uungwana ni kukiri kuwa umeteleza. Kwa umri wako hukutakiwa kuendekeza kauli za ubaguzi na uchochezi wa kidini namna hii.
Umefeli sana hapa mzee wetu
Lib...
Kukosea kunawezekana vipi nami nina vitabu na papers nyingi hii pamoja na kitabu ambacho kimesahihisha historia ya uhuru wa Tanganyika?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…