Billgate,
Hakika ni udini mtupu.
Nakuunga mkono mia kwa mia.
Inawezekana vipi Chuo Cha Kivukoni CCM iandike historia ya TANU isiwataje katika kitabu hicho viongozi wa TAA na waasisi wa TANU waliokuwa mstari wa mbele katika harakati za uhuru.
Hebu angalia maajabu haya.
Mwaka wa 1953 mwezi Aprili tarehe kumi na 17 ulifanyika uchaguzi wa mwaka kuchagua Rais wa TAA.
Wagombea ni Abdul Sykes aliyekuwa Kaimu Rais na Katibu wa TAA na Julius Nyerere.
(Kisa cha uchaguzi huu nimekieleza mara nyingi hapa).
Nyerere akachaguliwa kuwa Rais na Abdul Sykes Makamu wa Rais.
1954 TANU inaundwa.
Mipango yote ya kuunda TANU inafanyika nyumbani kwa Abdul Sykes.
Kadi za TANU mnunuzi wa kadi 1000 za mwanzo ni Ally Sykes kutoka mfukoni kwake.
1955 Nyerere anakwenda UNO na mipango yote ya safari inafanyika nyumbani kwa Abdul Sykes na mksanyaji fedha za safari ni Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na wakati huo huo Mweka Hazina wa TANU.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Sheikh Suleiman Takadir.
Viongozi wa akina mama katika harakati hizi ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee kwa kuwataja wachache.
Mwaka wa 1955 Nyerere anaacha kazi na anaishi na Abdul Sykes nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Tusimame hapa.
Historia ya TANU inaandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni mwaka wa 1981.
Hawa wote hawamo ndani ya kitabu hicho.
Nauliza vipi historia hii naambiwa na wapashaji habari wangu kuwa historia ya uhuru imejaa Waislam hili halitakiwi na wenye madaraka.
Ndipo hapa nakuunga mkono kuwa ni udini mtupu.