Gaudensia Kabaka Mwenyekiti wa UWT?

Gaudensia Kabaka Mwenyekiti wa UWT?

Lombo,
Unajua mjadala huu uko hapa kwa miaka mingi sana na chanzo chake ni kutokuandikwa kwa historia ya uhuru wa Tanganyika kwa ukweli.

Unachokofanya wewe ni kuturudisha kule tulikotoka.

Kitabu cha Abdul Sykes si mzaha.

Nyaraka nilizotumia kuandika kitabu hiki ni nyaraka za akina Sykes na zinaeleza historia ya African Association kuanzia 1929 Kleist Sykes akiwa Katibu muasisi.

Baada ya kuandika kitabu hicho niliingizwa katika miradi miwili ya kuandika historia ya Afrika - wa kwanza kutoka Oxford University Press Nairobi (2007) na wa pili mradi wa Dictionary of African Biography (2011).

Kutoka hapo nimeandika vitabu 10 na nimepewa tuzo 3.

Usidhani niandikayo ni mambo ya mashkara.
Sawa ni wa miaka mingi..so what !kuendelea kuandika kuwa Nyerere sio baba waTaifa,alisaidiwa na kina Sykes,...una maanisha mini !

Uislam unakataza kusaidia watu!

Hivi ulitaka Nyerere asaidiwe na Nani ,Kama si Waislam!

Kwa Nini Historia yako ya TANU inaishia Magomeni tu!

Hujui kuwa Kuna Wazee wa TaboraMwanza,DSingda,Moshi,Moro,Dodoms nk nao wwlitoa mchango wao!

Haiwezekani mwana Historia umekomalia Jambo hilo2 miaka nenda Rudi...usipoandika kuhusu Sykes kumsaidiavNyerere ,utaanduka kumhusu Bi.Titi,au mama aliyekuwa Ana muuzia vitumbua Nyerere, !

Kuna mengi ya kuandikwa ...kwa mini usichimbue jinsi Watumishi wa Umma enzi za Ukoloni,Huko Kagera,Singida,Tabora,Mwanza ,Moshi,Mbeya nk walivokuwa wanaichsngia TANU kifichoni!

Kwa Nini usichimbue mchango wa Sera ya Kutaifisha Shule ulivosaidia Watanzsnia kuwa wa wamoja,kwa kuzibeba Jamii zilixokuwa nyuma kielimu!?

Jana nilikutokea mfamo was Temeke na Kisarawe huku uona!?
 
Hivi kama bibi titi alihusika kutaka kumpindua Nyerere angeachwa tu? Kama siyo kweli ungemtetea lakini usiseme tu ooo alikuwa na mchango mkubwa kudai uhuru hakuna anayebisha kwa hilo!

Pili una uhakika gani juu ya upendeleo wa Gaudesia Kabaka hapo chuoni je wakiristo wakifanya makosa wanatazamwa tu?

Na je kuhusu ajira umefanya utafiti ukaona waislamu na wakiristo wana uwiano tofauti gani kulingana na idadi ya wasomi na fursa au ajira zitokapo?

Ukijibu haya maswali vyema usiingize tena udini hapa siyo madrasa wala Sunday school!
 
Tatizo mzee Mudi anawadanganya au kuwapotosha Waislam wachache ...Wale wajanja siku hizi wanapeka watoto wao kusoma Shule za mrengo was Kikristo wanapiga Elimu huku wakibaki na Uislam wao!
Haya Mambo hayataki hasira!
 
Mbona unaficha ukweli kwamba huyo Bi Titi alishiriki kutaka kuipindua Serikali akakamatwa na kushtakiwa kwa kosa ya uhaini na wenzie na kufungwa kabla ya kupewa msamaha na Nyerere?
MWANZO MEDIA: MATENGENEZO YA KIPINDI MAALUM KUHUSU MAISHA YA BI. TITI MOHAMED (1926 - 2000)

Mwanzo Media wamenihoji kuhusu maisha ya Bi. Titi Mohamed.

Huu ni upepo mpya kuona kumekuwa na mwamko mpya wa kutaka kujua historia ya uhuru wa Tanganyika na mashujaa wake ambao kwa miaka mingi walikuwa wamefutwa katika kumbukumbu za TANU na historia ya uhuru wa Tanganyika.

Nimeamua kwa makusudi kabisa kuweka picha za Bi. Titi akiwa msichana mdogo wa kiasi cha miaka 26 ili msomaji wangu upate ladha ya historia hii kama ilivyokuwa katika miaka ya mwanzo ya chama cha TANU.

Angalia picha mbili za mwisho ya kwanza kulia ni Bi. Titi Mohamed, Maria Nyerere, Julius Nyerere, Rashid Kawawa, nyuma ya Nyerere ni Tewa Said Tewa.

Hii ni moja katika picha alizopiga Mohamed Shebe.

Mwangalie mama yetu Bi. Biti Mohamed na haiba yake alivyokuwa msichana.

Picha ya mwisho wa kwanza kuliani Bi. Titi Mohamed katika moja ya mikutano ya mwanzo ya TANU Viwanja Vya Mnazi Mmoja.

(Mwangalie Bi. Titi amevaa baibui la ukaya na alikuwa akihutubia mikutano akiwa ndani ya baibui).

Anaefuatia ni Clement Mtamila, Sheikh Suleiman Takadir na mwisho ni Julius Nyerere.

Nyuma kulia ni John Rupia na Rajab Diwani.

Baada ya uhuru kupatikana mwaka wa 1961 baadhi ya wazalendo hawa katika picha hizi mbili watajikuta katika hali ambayo hakuna aliyeitegemea wala kuwaza huenda ikatokea.

Hapa ndipo anapoingia Bi. Titi; kuanguka kwake na kujikuta anatumikia kifungo cha maisha na kupoteza mali zake, heshima yake na kufutwa jina lake katika historia ya uhuru wa Tanganyika.

Lakini kwa kasi ya ajabu Bi. Titi akatoka kifungoni, akarejeshewa mali zake na heshima yake.

Haya yote yakitokea bila ya kutetewa na yoyote.

Bi. Titi sasa anatajwa na kuadhimishwa kama inavyostahili.

Kipindi hiki In Shaa Allah kitakuwa hewani hivi karibuni.

Screenshot_20211025-064953_Facebook.jpg
 
Lombo,
Unajua mjadala huu uko hapa kwa miaka mingi sana na chanzo chake ni kutokuandikwa kwa historia ya uhuru wa Tanganyika kwa ukweli.

Unachokifanya wewe ni kuturudisha kule tulikotoka.

Kitabu cha Abdul Sykes si mzaha.

Nyaraka nilizotumia kuandika kitabu hiki ni nyaraka za akina Sykes na zinaeleza historia ya African Association kuanzia 1929 Kleist Sykes akiwa Katibu muasisi.

Baada ya kuandika kitabu hicho niliingizwa katika miradi miwili ya kuandika historia ya Afrika - wa kwanza kutoka Oxford University Press Nairobi (2007) na wa pili mradi wa Dictionary of African Biography mradi wa Harvard na Oxford University Press New York (2011).

Kutoka hapo nimeandika vitabu 10 na nimepewa tuzo 3.

Usidhani niandikayo ni mambo ya mashkara.
Tunashukuru sana kwa uandishi wako mzuri..lakini kwakua uandishi wako ume base upande mmoja tu kwa masalahi yako binafsi..only wajinga ndio watakao kusikiliza..Tanganyika sio pwani tu unataka kuniambia huko mbeya..Kigoma..Moshi..Mwanza..Kagera niSsykes ndio alifanya ukombozi..hutambua hata michamgo ya vyama vya wakulima na wafanyakazi ambavyo vilisimama kidete...kudai uhuru?

Naomba mzee uache kulia lia kama mtoto..hii nchi haina udini na sio chini ya dini yeyote..mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi wa hii nchi..ila kitendo cha kuleta upotoshaji kwa mlengo wa kidini mzee umepungukiwa hekima.

Ushauri tu kaa ulee wajukuu..tuzo zisikupagawishe hata wajinga hupewa tuzo pia.

#MaendeleoHayanaChama
 
Tunashukuru sana kwa uandishi wako mzuri..lakini kwakua uandishi wako ume base upande mmoja tu kwa masalahi yako binafsi..only wajinga ndio watakao kusikiliza..Tanganyika sio pwani tu unataka kuniambia huko mbeya..kigoma..moshi..mwanza..kagera ni sykes ndio alifanya ukombozi..hutambua hata michamgo ya vyama vya wakulima na wafanyakazi ambavyo vilisimama kidete...kudai uhuru?

Naomba mzee uache kulia lia kama mtoto..hii nchi haina udini na sio chini ya dini yeyote..mtu yeyote anaweza kuwa kiongozi wa hii nchi..ila kitendo cha kuleta upotoshaji kwa mlengo wa kidini mzee umepungukiwa hekima.

Ushauri tu kaa ulee wajukuu..tuzo zisikupagawishe hata wajinga hupewa tuzo pia.

#MaendeleoHayanaChama
Jiwe...
Tuzo si kitu kikubwa kama unavyodhani.

Hii ni tuzo ya tatu kwangu.

Nimetunukiwa huko nyuma vikubwa zaidi ya tuzo hizi.

Umuhimu wa historia hii ni kuwa imesahihisha historia iliyodhaniwa ndiyo kweli katika kupigania uhuru wa Tanganyika.

Bahati mbaya sana na hili sikulitegemea hata kidogo ni kuwa imechoma nafsi za watu wengi kwa kuwa tu historia ya uhuru wa Tanganyika imejaa Waislam.

Labda swali la kujiuliza ni kuwa waliofuta historia hii walisukumwa na nini na nani na kwa nia gani?
 
Usidhani kosa hutatuliwa kwa kutenda kosa lingine.

Kauli yako ina elements za ubaguzi
 
Mkuu, naomba nikuulize swali. Kabla ya Mzee Mohammed Said kuandika historia ya Wazee wake, je uliwahi kumjua Dossa Aziz Ali au kumsoma katika Historia ya nchi iliyoandikwa hapo kabla? Kama hapana, unadhani kwanini?

Wote tunaujua Mchango wa Mwalimu Nyerere katika hii nchi. Ila Mzee Mohammed Said yeye kaandika Historia ya Wazee wake ambao walikuwa pamoja na Mwalimu katika kupigania uhuru, ila mchango wao ukasahaulika au kufutwa.
Aziz Dossa alikuwa anajulikana mzee, mimi nilikuwa napajua mpaka nyumbani kweli kule maeneo ya mlandizi na alikuwa anaheshimiwa kama mmoja wa wasisi wa TANU. Wakati wa operesheni vijiji, yeye hakuhamishwa kutokana na heshima hiyo. Nyerere alimfanya mtoto wake (Hamza Aziz) kuwa mkuu wa polisi, na hata alipofanya makosa akamhamishia kwenye ubalozi wa umoja wa mataifa wala hakumtupa.
 
NAOMBA KURUDIA KUULIZA MASWALI HAYA 9 KWA MZEE MOHAMED KAMA YALIVYOULIZWA NA WADAU KAMA YERIKO NA WENZAKE MWAKA 2013. (Tunaomba ajibu kwa Facts)

1) Uliathirika vipi kwa baadhi ya wazee waliopigania uhuru wa nchi hii kutokuwemo kwao katika histori ya nchi hii kama unavyodai?

2) Taifa na waislamu waliathirika vipi kwa baadhi ya wazee unaodai wewe walipigania uhuru wa nchi hii na hawamo katika historia?

3) Ulijuaje kuwa wazee hao walipigania uhuru ilihali hawapo katika historia stahiki ya nchi hii?

4) Unaposema historia ya uhuru wa nchi hii haiwakumbuki ama haiwatambui, ulitaka wakumbukwe katika maandishi ya vitabu au katika nyaraka za serikali za historia ya uhuru wetu?

5) Unatambua kuwa historia ya nchi yoyote ile duniani huwa wapi?

6) Upeo wako umegota kwenye historia ya waislamu wa Tanganyika na Nyerere tu, au historia ya waslamu duniani kote? Kama ndivyo, je matatizo ya waislamu wa Nigeria, Somalia, Sudani, nk Nyerere ndiye kayapeleka?

7) Je ulichokiandika ni historia ya Uhuru wa Tanganyika au ni historia ya baadhi ya Waislamu wa Tanganyika na mapito yao kisiasa?

8) Kwanini unaulazimisha umma kwa maandishi yako uamini kuwa ulichoandika ndio historia sahihi ya Uhuru wa Tanganyika?

9) Je ni kweli Mohamed Said huwajui na huwatambui wale wazee 17 waliosimama kidete kudai uhuru wa nchi yetu? Je wote walikuwa wakrstu?

Kwako Mzee Mohamed.
 
Mzee wangu Mohammed Said ameandika Historia ya Wazee wake katika kupigania uhuru baada ya kuona mchango wao katika kupigania uhuru umefutwa au umesahaulika. Na hao Wazee wake walikuwa ni Waislam tena baadhi yao waliutumia ule Uislam kupambana na ukoloni.

Sasa kama wewe nawe una ndugu zako waliopigania uhuru wakasahaulika au una uwezo wa kufanya utafiti ukaandika historia za hao watu wengine waliopigania uhuru kwenye hiyo mikoa mengine kisha wakasahaulika, basi fanya hivyo wala hakuna aliyekuzuia.
Gen...
Babu yangu Salum Abdallah ni muasisi wa TANU Tabora na alikuwa akihudhuria mikutano ya siri ya mipango ya kuasisi TANU kila siku ya Jumapili pale Town School.

Alitoa fedha kumleta Germano Pacha katika mkutano wa TAA wa 1953 ulioasisi TANU.

Mwaka 1955 alikuwa Mwenyekiti muasisi wa Tanganyika Railways African Union Kassanga Tumbo akiwa Katibu muasisi.

Ana historia nzuri sana ya kupambana na ukoloni.

Aliongoza General Strike tatu dhidi ya Waingereza 1947, 1949 na 1960 wakati Tanganyika inadai uhuru.

Mgomo wa 1960 ulidumu siku 82 kuvunja rekodi ya mgomo wa Kenya wa siku 62 ulioongozwa na Makhan Singh.

Mwaka wa 1964 alikamatwa na kuwekwa kizuizini kwa tuhuma za kutaka kupindua serikali.

Hùu ulikuwa uongo ulitungwa tu kuwaweka viongozi wa vyama vya wafanyakazi kifungoni ili serikali iunde NUTA.

Ana mengi sana babu yangu toka kuundwa kwa African Association 1929 yeye akiwa anaishi Mtaa wa Kipata.
 
NAOMBA KURUDIA KUULIZA MASWALI HAYA 9 KWA MZEE MOHAMED KAMA YALIVYOULIZWA NA WADAU KAMA YERIKO NA WENZAKE MWAKA 2013. (Tunaomba ajibu kwa Facts)

1) Uliathirika vipi kwa baadhi ya wazee waliopigania uhuru wa nchi hii kutokuwemo kwao katika histori ya nchi hii kama unavyodai?

2) Taifa na waislamu waliathirika vipi kwa baadhi ya wazee unaodai wewe walipigania uhuru wa nchi hii na hawamo katika historia?

3) Ulijuaje kuwa wazee hao walipigania uhuru ilihali hawapo katika historia stahiki ya nchi hii?

4) Unaposema historia ya uhuru wa nchi hii haiwakumbuki ama haiwatambui, ulitaka wakumbukwe katika maandishi ya vitabu au katika nyaraka za serikali za historia ya uhuru wetu?

5) Unatambua kuwa historia ya nchi yoyote ile duniani huwa wapi?

6) Upeo wako umegota kwenye historia ya waislamu wa Tanganyika na Nyerere tu, au historia ya waslamu duniani kote? Kama ndivyo, je matatizo ya waislamu wa Nigeria, Somalia, Sudani, nk Nyerere ndiye kayapeleka?

7) Je ulichokiandika ni historia ya Uhuru wa Tanganyika au ni historia ya baadhi ya Waislamu wa Tanganyika na mapito yao kisiasa?

8) Kwanini unaulazimisha umma kwa maandishi yako uamini kuwa ulichoandika ndio historia sahihi ya Uhuru wa Tanganyika?

9) Je ni kweli Mohamed Said huwajui na huwatambui wale wazee 17 waliosimama kidete kudai uhuru wa nchi yetu? Je wote walikuwa wakrstu?

Kwako Mzee Mohamed.
Jones...
Soma kitabu cha Abdul Sykes au ingia na fanya search: mohamedsaidsalum.blogspot.com.
 
May Day,
Hivi unajua Nyerere kaja Dar es Salaam hana ndugu wala jamaa?

Unawajua waliompokea?

Unadhani endapo wazee wetu wamgekuwa wabaguzi wa dini au kabila Nyerere angefika hapo alipofika?

Wewe unaridhishwa na hii hali ya leo katika mgawanyo wa fursa 20:80?
Takbiiir
 
Mkuu, naomba nikuulize swali. Kabla ya Mzee Mohammed Said kuandika historia ya Wazee wake, je uliwahi kumjua Dossa Aziz Ali au kumsoma katika Historia ya nchi iliyoandikwa hapo kabla? Kama hapana, unadhani kwanini?

Wote tunaujua Mchango wa Mwalimu Nyerere katika hii nchi. Ila Mzee Mohammed Said yeye kaandika Historia ya Wazee wake ambao walikuwa pamoja na Mwalimu katika kupigania uhuru, ila mchango wao ukasahaulika au kufutwa.
Na kinaSykes je?
 
Mzee wangu Mohammed Said ameandika Historia ya Wazee wake katika kupigania uhuru baada ya kuona mchango wao katika kupigania uhuru umefutwa au umesahaulika. Na hao Wazee wake walikuwa ni Waislam tena baadhi yao waliutumia ule Uislam kupambana na ukoloni.

Sasa kama wewe nawe una ndugu zako waliopigania uhuru wakasahaulika au una uwezo wa kufanya utafiti ukaandika historia za hao watu wengine waliopigania uhuru kwenye hiyo mikoa mengine kisha wakasahaulika, basi fanya hivyo wala hakuna aliyekuzuia.
Historia haiwezi kum5aja Kila mtu ....mbona Wazee wengi was Mzizima wameandikwa na wengine Nyerere aliwataja kwa kinywa chake?
Tatizo ni Nini?
 
mambo men
Kuna mambo mengine hayataki ligi. Fika Mzumbe University, pale kuna kanisa na wamepewa mpaka eneo la kujenga shule ilhali waislamu wanaswali Mzumbe Secondary School.
Wakati mwingine waislam tunafanya mambo yanayofanya tuonekane kama tunalalamika tu...sasa hapo Mzumbe waislam waliomba eneo la kujenga msikiti wakanyimwa? kam walinyimwa na kunaushahidi kuwa waliomba ndio suala la kujadili..sio kulalamika tu!
 
Vyovyote vile naamini kuna mapungufu mengi sana katika uandishi wa historia ya nchi ya Tanganyika na baadae Tanzania, mfano mwingine mzuri, shujaa wa mapinduzi ya Zanzibar ni yule Mganda Okello lakini leo historia imejaa na kumtukuza Mzee Karume!
 
mambo men

Wakati mwingine waislam tunafanya mambo yanayofanya tuonekane kama tunalalamika tu...sasa hapo Mzumbe waislam waliomba eneo la kujenga msikiti wakanyimwa? kam walinyimwa na kunaushahidi kuwa waliomba ndio suala la kujadili..sio kulalamika tu!
Ukikaa nyuma ya keyboard unaweza kuandika mpaka yasiyoelezeka. Kama picha mnato huwezi kuisoma kikaragosi kitakutia kichaa
 
Ukikaa nyuma ya keyboard unaweza kuandika mpaka yasiyoelezeka. Kama picha mnato huwezi kuisoma kikaragosi kitakutia kichaa
..Kama ambavyo umefanya wewe..umekaa nyuma ya Keyboard na kuandika vitu visivokuwa na ushahidi mradi tu...kuchonganisha!
 
Back
Top Bottom