Kalaga Baho Nongwa
JF-Expert Member
- Sep 27, 2020
- 9,953
- 23,150
Nakubalian na wewe mohamedi, tukirudi kuwatazama waislam kwa sasa tuliofungamana mno na upwani. Unaionaje hali hii sabbu historia ishatuachia kovu, nimebahatika kuona namna ambavyo wapwani/waislam tunasafa mno kulinganisha n wenzetu. Hii imewia ugumu hata kupata nafas kubwa katika teuzi nyingi.Sir...
Hakikusahaulika kitu.
Mwaka wa 1962 baada ya uhuru tu palifanyika First Muslim Congress chini ya EAMWS agenda ikiwa ELIMU.
Ikaamuliwa zijengwa shue za msingi, sekondari majimbo yote kwa ili sasa Waislam wajinyanyue katika elimu ambayo ilikuwa ikitolewa kwa ubaguzi baina ya wakoloni na wamishionari.
Mwaka wa 1963 pakafanyika Second Muslim Congress na ikaamuliwa kuwa ijengwe Chuo Kikuu .
Jiwe la msingi la Chuo Kikuu likawekwa na Mwalimu Nyerere mwaka wa 1968.
Hapa ndipo matatizo yakaanza.
Waislam wakajikuta wapo katika mgogoro.
Hiki kisa ni kirefu sana na nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
EAMWS ikavunjwa na serikali na chuo na miradi yote ya elimu ikafa.
Pakawa pia na njama ndani ya Wizara ya Elimu ya kuhujumu nafasi za elimu ya juu kwa Waislam.
Hili ni jambo nyeti sana kwa serikali na haipo tayari kulizungumza.
Matokeo yake ndiyo haya.
Nadhani umepata kusikia matatizo ya NECTA jinsi wanavyohujumu shule zetu Waislam tunazojenga kwa jasho, vumbi na damu zetu.
Waislam waliandamana mwaka wa 2012 kueleza vipi Ndalichako ndani ya NECTA inavyohukumu mitihani ya shule za Kiislam.
Serikali ilionya Waislam kuktoshiriki katika maandamano haya lakini Waislam walikaidi na Sheikh Ponda aliongoza maadamano haya kutokea
Binafsi nashawishika kusema kwamba jitihada hizi hata kama zilizimwa kwa kias kikubwa kwa sasa, pwani inahitaji elimu ya kuipokea elimu iliyopo. Hili suala la uchache wa ajira kwa pwani ishakuw sabbu y kuachana na mambo ya elimu
Nimeona kama si kusikia mzee wa ruksa akitupambania sana kufika sehemu walau na sisi tuwemo. Na pia maendleo ya idadi ya waislam vyuoni n taasisi kubwa nchini z kielim sio mazuri inawez kuwa 30:70 huku ndipo tatizo hili kwa sasa linapotokea