Kuna sababu hii 20 mkuu haikuja bure. Kuna kitu tulikisahau mpka sas kinatupiga penati watu wa pwani
Sir...
Hakikusahaulika kitu.
Mwaka wa 1962 baada ya uhuru tu palifanyika First Muslim Congress chini ya EAMWS agenda ikiwa ELIMU.
Ikaamuliwa zijengwa shue za msingi, sekondari majimbo yote kwa ili sasa Waislam wajinyanyue katika elimu ambayo ilikuwa ikitolewa kwa ubaguzi baina ya wakoloni na wamishionari.
Mwaka wa 1963 pakafanyika Second Muslim Congress na ikaamuliwa kuwa ijengwe Chuo Kikuu.
Jiwe la msingi la Chuo Kikuu likawekwa na Mwalimu Nyerere mwaka wa 1968.
Hapa ndipo matatizo yakaanza.
Waislam wakajikuta wapo katika mgogoro.
Hiki kisa ni kirefu sana na nimekieleza katika kitabu cha Abdul Sykes.
EAMWS ikavunjwa na serikali na kuunda BAKWATA na Chuo Kikuu na miradi yote ya elimu ikafa.
Pakawa pia na njama ndani ya Wizara ya Elimu ya kuhujumu nafasi za elimu ya juu kwa Waislam.
Hili ni jambo nyeti sana kwa serikali na haipo tayari kulizungumza.
Matokeo yake ndiyo haya.
Nadhani umepata kusikia matatizo ya NECTA jinsi wanavyohujumu shule zetu Waislam tunazojenga kwa jasho, vumbi na damu zetu.
Waislam waliandamana mwaka wa 2012 kueleza vipi Ndalichako ndani ya NECTA inavyohujumu mitihani ya shule za Kiislam.
Serikali ilionya Waislam kutoshiriki katika maandamano haya lakini Waislam walikaidi na Sheikh Ponda aliongoza maadamano haya kutokea Msikiti wa Kichangani hadi Kidongo Chekundu.
Ni kisa kirefu siwezi nikaeleza kila kiu hapa.
Askari hawakuwashambulia wanaandamanaji.
Akili zilirejea na serikali ilijua kuwa Waislam wanaandamana kwa jambo la haki na laiti wakiwashambulia na labda kuwaua au kuwaumiza kwa kukataa dhulma balaa laki litakuwa kubwa.
Picha hiyo hapo chini ni kabla ya maandamano baada ya kuwahutubia Waislam Sheikh Ponda aliweka ushahidi wa hujuma mbele ya Waislam na akasema lazima tuandamane.
Hotuba ilikuwa ya kusisimua sana.
Alipomaliza ndipo akageuka akaangaia kibla akamkabili Allah kuomba dua.
Umma wote msikitini walitoka kuandamana.