Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,967
- 32,074
- Thread starter
-
- #141
Generation...Shukran mkuu, ila kiukweli Mimi Dossa nimemjulia kupitia akina Mzee Mohammed Said.
Halafu rekebisha kidogo hapo mkuu, nadhani Hamza Azizi Ali sio mtoto wa Dossa Aziz Ali, hao ni Brothers.
Kilembwe,Vyovyote vile naamini kuna mapungufu mengi sana katika uandishi wa historia ya nchi ya Tanganyika na baadae Tanzania, mfano mwingine mzuri, shujaa wa mapinduzi ya Zanzibar ni yule Mganda Okello lakini leo historia imejaa na kumtukuza Mzee Karume!
Billgate,udini mtupu 😕
Ruta...Mimi natoa mchango wangu kama mtu neutral. Na declare interest japo nimezaliwa kwenye moja ya dini hizi mbili kubwa, lakini mpaka hivi leo bado nina mashaka ya imani za dini. Tunajikuta tupo kwenye hizi dini si kwa choice bali kwa kukuta tumezaliwa na wazazi wenye dini moja au mbili ya kati ya dini hizi 2 kubwa.
Binafsi, kuna mambo naafikiana juu ya uduni na upotofu wa Historia yetu kabla ya Uhuru na hata baada. Kwangu mimi Nyerere was smart, lakini alikosa uvumilivu wa kisiasa kwa watu aliopishana nao mawazo na impact yake ilikua kuwaweka vizuizini, kuwafunga, kuwamaliza, kuwatesa na hata kuwachafua mbele ya jamii na kutokana na kuminya taarifa na mfumo wa ujamaa jamii ikaamini.
Na mpaka hivi leo athari zake zinaishi.
Moja ya watu wa nyumbani nayemfahamu ni mhanga wa utawala wake ni Mzee Ludovic Mwijage na kuna kitabu chake pia. Kwa sasa anaishi Denmark.
Kuna hoja juu ya malalamiko ya waislamu kipindi cha utawala wake. Lakini hiyo ni zamani vipi kuhusu sasa?
Niseme tu bado waislam wa nchi hii hasa Ukanda wa Pwani na Visiwani, mwamko wa uwekezaji kwenye elimu ni mdogo. Vijana hawataki kusoma, wazazi hawaipi elimu kipaumbele. Elimu ni bidhaa aghali. Lakini, si kwa jamii ya Pwani ambayo ni muslim majority. Bado waislam - hasa wale fanatics elimu kwao ni kama kitu cha ziada na si lazima. Walau waislam wa bara, wanasoma na wanaipa elimu kipaumbele, japo vilevile ukikuta wale fanatics ni tatizo kwenye kufanya uwekezaji wa elimu.
Nimeishi sana na jamii ya watu wa Pwani (ambayo kimsingi ni muslim majority) inashangaza mzazi ana ardhi ya kutosha, inatokea anauza ardhi kwa pesa ya kutosha, lakini anaona si sahihi kuwekeza kwenye elimu ya watoto wake. Matokeo yake jamii ya watu wengi wa Pwani ni mzigo tu. Nilikua nawaelimisha kwa kuwa kama watanzania wenzangu natamani kuona ustawi kwenye jamii yao. Lakini wapi!!!
Siafiki ujenzi wa misikti na makanisa kwenye taasisi za umma unless zile za kidini.
Muone huyu nae,ulikuwepo?Soma history vizuri..
Hawakutaka kupindua serikali ..
Walibambikiziwa kesi kwa kutofautiana na Nyerere....
Bibi Titi alipachikwa tu kwa kesi ambayo hata haijui..
1. Mzee Mohamed wapashaji habari wako ni wakina nani? Na kwanini huwa siku zote unatulazimisha kuwaamini hao wapasha Habari wako bila reference za kutosha??Billgate,
Hakika ni udini mtupu.
Nakuunga mkono mia kwa mia.
Inawezekana vipi Chuo Cha Kivukoni CCM iandike historia ya TANU isiwataje katika kitabu hicho viongozi wa TAA na waasisi wa TANU waliokuwa mstari wa mbele katika harakati za uhuru.
Hebu angalia maajabu haya.
Mwaka wa 1953 mwezi Aprili tarehe kumi na 17 ulifanyika uchaguzi wa mwaka kuchagua Rais wa TAA.
Wagombea ni Abdul Sykes aliyekuwa Kaimu Rais na Katibu wa TAA na Julius Nyerere.
(Kisa cha uchaguzi huu nimekieleza mara nyingi hapa).
Nyerere akachaguliwa kuwa Rais na Abdul Sykes Makamu wa Rais.
1954 TANU inaundwa.
Mipango yote ya kuunda TANU inafanyika nyumbani kwa Abdul Sykes.
Kadi za TANU mnunuzi wa kadi 1000 za mwanzo ni Ally Sykes kutoka mfukoni kwake.
1955 Nyerere anakwenda UNO na mipango yote ya safari inafanyika nyumbani kwa Abdul Sykes na mksanyaji fedha za safari ni Iddi Faiz Mafungo Mweka Hazina wa Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika na wakati huo huo Mweka Hazina wa TANU.
Mwenyekiti wa Baraza la Wazee Sheikh Suleiman Takadir.
Viongozi wa akina mama katika harakati hizi ni Bi. Chiku bint Said Kisusa, Bi. Titi Mohamed na Bi. Tatu bint Mzee kwa kuwataja wachache.
Mwaka wa 1955 Nyerere anaacha kazi na anaishi na Abdul Sykes nyumbani kwake Mtaa wa Stanley na Sikukuu.
Tusimame hapa.
Historia ya TANU inaandikwa na Chuo Cha CCM Kivukoni mwaka wa 1981.
Hawa wote hawamo ndani ya kitabu hicho.
Nauliza vipi historia hii naambiwa na wapashaji habari wangu kuwa historia ya uhuru imejaa Waislam hili halitakiwi na wenye madaraka.
Ndipo hapa nakuunga mkono kuwa ni udini mtupu.
Jones,1. Mzee Mohamed wapashaji habari wako ni wakina nani? Na kwanini huwa siku zote unatulazimisha kuwaamini hao wapasha Habari wako bila reference za kutosha??
2. Kwanini usianishe mambo yote unayoita ni dhuluma kwa "watu wako" ili wote tuyafahamu badala ya kuandika kwa mafumbo mafumbo?
3. Hivi tangu kipindi hicho ndani ya serikali hakukuwa na waislam? Hawakuyaona haya unayoita dhuluma?
4. Ni kweli unaamini wakristo ndio wamesababisha matitizo kwa waislamu? Unaweza kufafanua kivip??
5. Je matatizo yaliyo kwenye nchi zinazoongozwa kiislam tangu kipindi hicho nayo yamesababishwa na wakristo??
NB: Uwe unajibu maswali kwa fact na reference Mzee Mohamed tafadhali sana, vinginevyo tutaendelea kuamini maandiko yako unayatoa kwenye vijiwe au barza za ghahawa.
Nashukuru nitaisoma.Ruta...
Bahati mbaya hujui historia ya Waislam na juhudi zao katika elimu ndiyo maana unasema Waislam hatuthamini elimu.
Ni paper ndefu inataka ustahamilivu lakini ikiwa unataka kujua ukweli soma yote:
Ruta...Nashukuru nitaisoma.
Mie najua wewe muislam wa bara. Shule umekwenda na unajua umuhimu wake. Nasemea ndugu zetu wa Pwani na hii inajionyesha wazi. Tusiendelee kulialia kwa mambo ya nyakati zilizopita. Tujipanguse na kuangalia hatma ya mbele.
Nashukuru kwa kiungo nitaisoma.
Nilidhani utajibu hoja zilizo mezani naona unakwepa maswali.Jones,
Sikulazimishi kuniamini.
Hili lisikupe tabu.
Watu waliamini historia ya Kivukoni kwa miaka mingi.
Cha ajabu kipi ukikataa kuwa TANU Nyerere kaikuta nyumbani kwa Abdul Sykes?
Cha ajabu kipi ukikataa kuwa African Association iliasisiwa na Kleist Sykes 1929?
Walioniamini walinialika kuzungumza katika kumbi za vyuo vyao.
Jones...Nilidhani utajibu hoja zilizo mezani naona unakwepa maswali.
Anyway sidhani kama kuna dhuluma yeyote una mislead watu kitu ambacho sio afya taifa. Taifa lina amani tele wakristo kwa waislam wanazikana, wanasherekea Sikukuu zote kwa pamoja, wanasoma kwa pamoja kwa furaha kabisa hao unasema wanadhulumiwa Kuna baadhi hata hapa jukwaani wanashangaa.
Na tunashangazwa na chuki unaiotoa wapi mzee wangu
Nina kipi nijuacho??Jones...
Huyajui.
Mimi nikwepe swali gani kwako?
Una kipi ukijuacho?
Tatizo lako Mohamed unajinasibisha Na historia ya Tanzania kwa Ujumla wakati so kila kitu unakijua japo nakupongeza kwa kujua angalau 30% ya history lakini so 100% hivo wenye mawazo mbadala usuwabezeJones...
Huyajui.
Mimi nikwepe swali gani kwako?
Una kipi ukijuacho?
"Na zaidi ni kuwa safari ya kwanza ya Mwalimu Nyerere ya kwenda UNO 05/03/1955 , Kanisa Katoliki lilitoa msaada kwa chama cha TANU wa tiketi ya ndege ya kwenda na kurudi, lilifanya hivyo kupitia shirika lake la Maryknoll Sisters la New York Marekani,Jones...
Huyajui.
Mimi nikwepe swali gani kwako?
Una kipi ukijuacho?
Jones,Nina kipi nijuacho??
Kama unachojua wewe watu wanakitilia shaka una ithibati gani ya kuniambia mimi nina kipi nijuacho??