Mohamed Said, hebu twende taratbu...
1. Bibi Titi Mohamed anafahamika katika historia ya Tanzania kama kiongozi wa Waislamu katika kada yoyote, au anatambulika kama mwana-siasa aliyepigania uhuru wa Tanganyika na Mwenyekiti wa UWT?
2. Huyo Gaudensia Kabaka alikuwepo kwenye sherere za kumuenzi Bibi Titi akiwa na kofia ya Utawa au akiwa na kofia ya Uenyekiti wa UWT?
3. Wale walioenda kumuona mtoto wa Bibi Titi, walikuwa ni viongozi wa Kiislamu au CCM?
4. Paliwahi kuwa na tuhuma kwamba Mwalimu Nyerere alifanya sahihi kumtia korokoroni Bibi Ti
5. Kwamba:-
Ni umoja upi huo ambao uliasisiwa na mama zenu?! Umoja wa Wanawake wa Kiislamu Tanzania, au Umoja wa Wanawake Tanzania?!
6. BInafsi, labda kwa kutokuwa na uelewa, sijapata kusikia Bibi Titi kuasisi Umoja wa Wanawake wa Kiislamu Tanzania bali nimesoma mara kadhaa kuhusu yeye na wenzake kuasisi Umoja wa Wanawake Tanzania! Sasa kama unazungumzia UWT, hivi hujisikii aibu kutoa kauli kama hiyo hapo juu?
Niwe mkweli Mzee Mohamed Said... nakuheshimu kutokana na umri wako na pia kutokana na maarifa yako lakini ukweli ni kwamba UNABOA!!!
Hivi unajisikiaje kila mada kuhusisha na udini?!
Ajabu yako sasa... mtoto wa Bibi Titi mwenyewe kafurahia ugeni lakini unakuja kuumia wewe na kuingiza udini! Ina maana unataka kusema wewe unamfahamu sana Bibi Titi, na una mahaba nae sana kuliko mtoto wake wa kumzaa?!
Badala ya mara kwa mara kuleta mada zinazoakisi udini, Hivi kama kweli una uchungu na imani yako, kwanini usitumie muda wako kuelimisha
Wazee wenu wewe na akina nani?
Mama zenu wewe na akina nani?
Kama hiyo "mama zetu" unamaanisha "mama wa Waislamu", tafadhali stop generalizing kwa sababu sio Waislamu wote wanapendezwa na huu ujinga wa mambo ya udini!!
Nilidhani ungesema hapo ndipo walipokuwa wakiimba qaswida, kusoma quran na maulidi kumuomba Mwenyezi Mungu!! Kumbe walikuwa wakiimba nyimbo za hamasa katika kupigania uhuru?!
Itoshe tu kusema kwamba, tumia elimu na maarifa yako kuhubiri umoja badala ya kuhubiri umimi na udini!! Sisi, na wengine miongoni mwetu ni Waislamu, tunamfahamu Bibi Titi kama miongoni mwa wapigani uhuru wa taifa hili!!
Tumefundishwa Bibi Titi alikuwa mwanamke shupavu katika harakati za kupigania uhuru, lakini HAKUNA popote tulipofundishwa alikuwa Mwanamke wa Kiislamu Shupavu katika kupigania Uislamu!!
And FYI, hata Madrasa nimesoma, tena Kurasini Dar es salam... mwendo mfupi tu kutoka Kariakoo lakini HATA SIKU MOJA hatukuwahi kufundishwa habari za Bibi Titi!!!
ACHA UDINI....