Gazeti la The Economist: Rais Magufuli na CCM kuendelea kushika madaraka baada ya Uchaguzi Mkuu

Kabendera angekuwa nje,angeandika ccm itaanguka
Hao viongozi waende tu,lakini wajue kuna sheria ya utakatishaji pesa
 
Kama ishu ya lowasa katika uchaguzi mkuu hujui basi ww ni mgeni wa siasa au ni kijana mdogo ambae unaleta ubishi usio na msingi
Wewe ndiye unaleta hoja za hisia zako lakini bila kujua kuwa hoja zako zinakinzana!
 
Kumbuka uchaguzi wa mfumo wa vyama vingi umeanza mwaka 1995.

Tumefanya chaguzi kuu 5 mpaka sasa.

Leo ndio mmejua kuwa tume niya CCM?
 
Si gazeti la mabeberu au.
Mkuu;
Sielewi hoja yako ya msingi ni nini?

Kama mabeberu yamefikia hitimisho na kusema CCM/Rais Magufuli watashinda basi itakuwa yamefanya kila njia kuhakikisha hawashindi lakini imeshindikana!
 
Baada ya uchaguzi wa 2015 nchi hii haijaongozwa tena na ccm bali na "kitchen cabinet". Chama kimetumika tu kama hirizi ya kisiasa na kupiga muhuri mawazo binafsi ya baadhi ya watu.
Wewe ulitaka iongozwe na CCM?
 
Umeusema ukweli ambao wapinzani hawataki kuusikia au kuuelewa!
 
Baada ya chaguzi kuu 5 kwa muda wa miaka 25 kwa sasa ndio mmejua kuwa Mwenyekiti wa Tume na Mkurugenzi wanachaguliwa na Rais?
 
Tena nimewahi kusema mara nyingi sana humu jamvini kwamba HAKUNA MTU MNAFIKI KAMA ZITTO KABWE, NI OPPORTUNIST WA HALI YA JUU SANA ! Wamarekani na ujanja wao wasipo kua makini atawapiga hela ndefu japokua wanaweza mtemesha vile vile.
Pesa ya Wamarekani huwa haiendi bure!

Juzi tu Wairaq na viongozi wao wamesema hawawataki Wamarekani ndani ya nchi yao lakini Rais wa Marekani akawaambia hawawezi kuondoka nchini humo mpaka wawalipe pesa yao waliyotumia katika kuwalinda!
 
Siasa ni mapambano kati ya vyama vya siasa lakini kikubwa zaidi, Siasa zetu zimejengeka katika msingi wa ''Mshindi huchukua vyote''.

Kuna uwezekano mkubwa mshindi wa 2020 akachukua vyote!
 
Tangu uchaguzi umeanza je kura za upinzani zinapishana kwa ukubwa gani?
Unaweza kupitia LINK HII>>>
 
..binafsi sijamsikia Dr.Slaa akikanusha madai yake kuwa aliibiwa kura na ushindi mwaka 2010.
Kama una macho na yanaona, huhitaji kusikia anachokisema wakati matendo yake unayaona!
 
P, dunia yenyewe ina mwisho, ccm inatawalaje milele; au una maana gani unapotumia hilo neno “milele”!




Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…