Ukweli ni kwamba maadui wa Magufuli waliofurahia kifo chake ni wachache sana na karibuni wote hao ni wanufaika wa ufisadi kwa namna moja au nyingine. Kutaka kuwafurahisha hao hakukuongezei mtaji wa kisiasa. Wanaompenda JPM kwa dhati ni wengi mno na ukiwahuzunisha hao kwa kumkashifi JPM kama wanavyofanya wanasiasa uchwara ni kujichimbia kaburi kwenye ulingo wa siasa za Tz!! Mliokosea hapo jiandaeni kuaibika!! JPM japo hayupo lakini hakuna mwenye ubavu wa kuweza kuvunja misingi aliyoiweka!! Kwa mfano huwezi kuimba wimbo wa "Tanzania ni nchi maskini" halafu utegemee watu watakuitikia!!, Pia huwezi kuimba wimbo wa "kuwatishia watu na corona" halafu utegemee watu watakuitikia!! Huwezi kupambana na kivuli cha Magufuli na ukashinda!! Kama unabisha waulize wanaohamasisha chanjo za corona na uvaaji wa barakoa!!! Magufuli ni mwanasiasà aliyefanikiwa sana!! Huwezi kubomoa alichokijenga, na ukijaribu unajibomoa mweñyewe!!