Geita: Afariki dunia baada ya kuchomwa kisu mara 17

Geita: Afariki dunia baada ya kuchomwa kisu mara 17

Sehemu nzuri ya kujifunzia mambo ya ndoa Ni Lindi liwale kwa wangindo, hawana stress na mapenzi, nina miaka kumi huku sijawahi sikia mme kapiga mke Wala kinyume chake, sijawahi sikia watu kuuana sababu ya mapenzi, watu wa Kanda ya ziwa mko siriazi sana na nyenge, badirikeni
Hayo mambo Mara na Mwanza. Kagera hakuna.
 
Mashaka Jeremia mkazi wa Mtaa wa Lukirini mkoani Geita anashikiliwa na Jeshi la Polisi mkoani humo kwa tuhuma za kumuua Mke wake Bi. Amina Iddy, kwa kumchoma kisu mara kumi na saba kwenye sehemu mbalimbali za mwili wake akimtuhumu kuuza shamba la familia bila ridhaa yake.

ITV
 
Hii habari ina zaidi ya week mbili mkuu.

 
Ndoa hazijawa hatari usikuze mambo huyo ujinga wake umemuuwa,hili lingeweza kutokea hata kwa kaka na dada kwanini auze kitega uchumi cha familia?

Huyo kafa kwa tamaa siyo kwa sababu ya ndoa yake.
What if Mwanaume alikuwa haudumii familia ? Wanaume wenzetu wa Geita wanatuaibisha sana,nimeishi Geita kama miezi 9 nilikuwa kila week nakutana na kesi za mwanaume kutelekeza familia au kumfukuza mke huku yupo na kichanga, kuna siku nimeenda fuel station moja akaja mwanamke amechoka akaniomba msaada wa chochote huku analia,kaachwa na mume huku ana kansa hivo amekatwa titi na yupo na mtoto mgongoni
 
Back
Top Bottom