Iwapo nia ni kuunda mkoa unaosogeza huduma jirani na wananchi ni busara mkoa huu kuundwa kwa kuweka makao makuu Biharamulo.Kwa nini makao makuu yasiwe biharamulo na mkoa usiitwe biharamulo wachukue sehemu ya muleba, biharamulo,ngara,kakonko,bukombe na chato yenyew?
Sioni maana/mantiki ya wakazi wa wilaya za Ngara na Kakonko kuvuka wilaya ya Biharamulo wakienda Chato ambayo no wilaya itakayokuwa pembeni mwa mkoa huu mpya.
Mkoa huu badala ya kunufaisha wakazi wake wengi utawaumiza.
Pia sioni manufaa atakayoyapata mkazi wa Buseresere kwa kuwa ataongeza umbali wa kwenda makao makuu ya mkoa.
Hata hivyo nashauri serikali badala ya kuwaza kuongeza mikoa, ijikite kupunguza ukubwa wa vijiji na kata.
Hili liende sambamba na kuwarahisishia utendaji wa kazi zao kwa kuwapa usafiri, vifaa vya kazi kama kompyuta mpakato, simu zinazoweza kupata matukio[picha] vema.
Hapa Ngara kwenye kata ya Muganza, umbali kutoka Kitongoji cha Nyakafandi hadi makao makuu ya Kijiji chao cha Mukubu ni km.15.
Kutoka kitongoji hicho hadi makao makuu ya kata ni zaidi ya km.30.
Mtendaji wa kata na kijiji hawana usafiri wowote.
Huko hakuna umeme.
Wangeweza kusaidiwa kupewa umeme wa jua kwenye ofisi zao ili wachaji simu za ambazo zinafanya kazi za ofisi.
Wananchi hatuna hitaji la mikoa.
Tunahitaji zaidi huduma bora za vijiji na kata.
Ikumbukwe miaka michache iliyopita ukubwa wa vitongoji uliongezwa badala ya kupunguzwa.
Kuna sehemu mitaa/vitongoji vitatu viliungwa kuwa kimoja.
Mzigo uliongezeka.
Mt