Geita isipojihadhari, itakuja kuachwa mbali sana na Njombe

Mwanza ni ndoto ya kila zilizokua wilaya zake zikapanda hadhi au kuchomolewa,wakipata tu pesa wapo town mwanza. Huko pengine sijui sababu ni zipi.
Swali Kwa nini wasijenge Geita badala yake wakawekeze Mwanza na Kahama? Mbona Njombe haijamezwa na Iringa,Songea au Mbeya?
 
Hujamuelewa mleta mada.
Hajasema Njombe inaizid Geita Kwa wingi wa fursa na rasilimali isipokuwa amesema Njombe inaizid au itaizid Geita maendeleo.

The late JPM amewah shangazwa na ujenzi wa nyumba bora uliopo Njombe
 
Njombe mkoa mzima unawatu laki nane sawa na jimbo la busanda! Geita aka gold region usiilinganishe na maparachichi na ngwengwe region!

Mkoa wa geita Ina miji ya geita, katoro, ushirombo, runzewe na masumbwe.
Lakini watu 800k Wana Uchumi mkubwa na maisha Bora kushinda Geita yenye watu over 3M.

Maparachichi yanaitwa green gold 💚💚💚💚 ni uhakika wa pesa.

Njombe ni Mkoa wa kimkakati wa Serikali Kwa sababu zifuatazo.
1.Mji wa Makambako unatengenezwa kuwa Industrial zone
2.Mkoa wa Njombe una mito mikubwa 3 ambayo itajengwa mabwawa makubwa ya Kuzalisha umeme-Ruhudji,Rumakali na Ruhuhu.
4.Njombe ni Mkoa umeteuliwa maalumu Kuwa.kitovu Cha kuzlisha ngano ya ukanda wa Juu(Baridi) Tanzania
5.Wakati Geita mnalingia Dhahabu ya mzungu,Njombe ndio Mkoa pekee ambao una Madini ya Chuma(Liganga&Mchuchuma ) Tanznaia nzima.
6.Mkoa wa Njombe ni Mkoa maalumu wa Kilimo kikubwa Cha Chai,Pareto na Horticulture eg parachichi,nk.
7.Mkoa wa Njombe ni Shamba la Kilimo Cha miti kibiashara
8.Njombe ni Mkoa uliopo junction na unapakana na Mikoa mingine ya wachapakazi eg Mbeya,Ruvuma, Morogoro na Iringa.
9.Njombe ni Mkoa wenye vivutio vya Utalii eg Hifadhi ya Taifa Kitulo,Milima ya Mpanga-Kipengele,Safi za Milima ya Livingstone na Lake Nyasa.
10.Njombe ni Mkoa wenye makabila ya wachapa kazi eg Wakinga,wabena ,Wopangwa.Hao ni Hustlers yaani huko Kwenye migodi Geita wapo maana Mwenyekiti wa wachimbaji wadogo Tanzania ni Mkinga wa Njombe.

Sasa Kwa nondo hizi saa ngapi Geita italingana na Njombe?
 
Ukitoa mgodi wa huyo mzungu wa GGM ,Geita ni zero kabisa.

Hata hivyo Geita ni Moja ya Mikoa top 10 yenye GDP kubwa hapa Tanzania eti Iko Juu ya Dodoma 😁😁
Sio kwa sababu ya Geita Mine kuwa top 10 ni sababu ya local business zinazolipa kodi VAT na Income Tax local Geita ziko vizuri
Makampuni ya kigeni hulipa income tax kwao wanakouza hayo madhahabu soko lingekuwa Tanzania wangelipa income Tax na VAT hapa.

Ni sawa na wewe uwe na soko la Njegere Ulaya VAT na income Tax utalipa ulaya sio Tanzania sawa na mtu exporter wa magari ya Japan mwenye kampuni hapa na mauzo yanafanyika hapa atalipa income tax hapa na VAT

Soko la dhahabu nyingi haipo Tanzania wala Geita Hatulipwi VAT au income tax tunalipwa mrahaba tu na local tax za local content hizo ni sheria za kimataifa za kodi

Madini tunapata mrahaba tu sababu hayo matani na matani ya dhahabu soko hapa hatuna wanauza kwao kwenye nchi zao ambako kampuni zao zinatoka na zina makao makuu kule kama local resident companies

Geita ikiongoza Mapato TRA jua ni local business ziko vizuri kulipa TRA sio foreign business
 
Mwanza ni ndoto ya kila zilizokua wilaya zake zikapanda hadhi au kuchomolewa,wakipata tu pesa wapo town mwanza. Huko pengine sijui sababu ni zipi.
Jibu ni Moja,Mikoa mingi sana hapa Tanzania kama sio yote,Maisha ya mawilayani ni hovyo na hakuna fursa tofauti na Wilaya za Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini ambako kila Wilaya imechangamka.

Sasa nani anataka kuishi Ngudu,Buchosa, Sengerema,Ukerewe nk? Afadhari na Misungwi na Magu ziko pembezoni mwa Mji.

Hii ni tofauti sana na Wilaya za Mkoa mfano wa Mbeya Chunya, Mbarali,Kyela,Rungwe ambako kote ni kizuri na kuko liveable likewise case ya Njombe na Geita.
 
Acha porojo zisizokuwa na msingi basi.Mwaka huu GGM imepata cheti Cha mlipaji Kodi mkubwa na TRA wewe unaleta stori za local businesses zipi hizo? 😁😁

Pia mgodi unaoongoza kuingiza Mapato hapa Tanzania ni GGM ,harafu wewe unaleta hadithi za mchana.

Geita ni Moja ya Mikoa yenye idadi kubwa sana ya watu na Ina Kasi kubwa mno ya kuzaliana sijajua ni Kwa nini lakini inaonesha chakula kipo na mvua Huwa inanyesha vizuri japo sijafanya utafiti.
 
Hata Mererani (Bunguni) Manyara (zamani arusha) hali ni hiyo. Ni eneo linalotajirisha wengine na kukuza miji mingine kama Arusha, Moshi, Nairobi na Kigali lakini lenyewe limebakiwa kuwa duni mnoo.

Ni kama laana vile.
 
Mkuu, kama si typing error, basi utakuwa na "bifu" na watu wa Njombe.

Mjinga hawezi kuwa Mwenyekiti.
 
in short kodi hizo ni za local content kama PAYE ya kodi za mishahara na posho za wafanyakazi wa mgodini kama wanalipa mikubwa na local suppliers local content wana supply bidhaa nk wanatakiwa wawakatwe VAT nk na kuwakilisha TRA anyway niwapongeze kwa hilo kuwa wako vizuri local content inayoingiza kodi kubwa iwe PAYE ya wafanyakazi au VAT ya manunuzi local content malipa VAT etc nawapongeza kwa hilo kwa kweli hongera zao makampuni mengine yawaige ya nje
 
HHap
Hapo umewafafanua Kila kitu mkuu
 
Toka lin wafuga n'gombe wakawa na hela
Na hao wachimbaj wanahela za bia tu sio za kufanyia maendeleo
 
Njombe ilijikita zaidi kwenye Kilimo na biashara kwa Sasa tayari wameanza kutoa na madini mfano makaa ya mawe na chuma na tayari kongani ya viwanda vya chuma inajengwa makambako wameteua mji wa makambako uwe wa biashara na viwanda
 
usiringanishe njombe na vitu vya kijinga
 
Kwani zipo kwenye ligi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…