Geita isipojihadhari, itakuja kuachwa mbali sana na Njombe

Geita isipojihadhari, itakuja kuachwa mbali sana na Njombe

Hujui Geita wewe

Geita watu wana hela kuanzia mjini hadi visiting

Geita vijijini kuna dhahabu migodi midogo iko kibao Sio tu hiyo mikubwa.Watu wana hela vijijini Geita Acha

Pili wasukuma wale ni wafugaji .Wana ng'ombe sio utani

Tatu wana zao la biashara la pamba wanauza nje

Nne ziwa lipo wanavua samaki hizi sato na sandala kwa wingi sana

Vijijini wana mapato mazuri ya uhakika kuliko wanavijiji wa njombe

Mjini ndio kabisa biashara ziko juu sana zikitegemea wanavijiji wenye pesa ,wafanyabiashara na wakazi wa mjini wafanyakazi wa migodi na pale kuna soko la madini kwa kanda ya ziwa madini hadi toka Congo yanauzwa Geita ushuru na kodi inayopatokana huwezi linganisha na kodi za hayo maparachichi na mbao
Pesa haipendi utetezi. Inaongea yenyewe.
 
Mkuu, umeshafika Njombe?

Nimekaa Geita zaidi ya mwaka mmoja. Hapa Njombe sina hata mwezi mmoja. Nimeona utofauti mkubwa sana.

Siwasifii, ila naona kama kiwango cha uelewa wa watu wa huku ni mkubwa pia. Ni watu "wanaojielewa". Wana miili ya kawaida na akili "kubwa"
🙄😳🤔
 
Mleta Uzi weka data-
1.GDP latest
2.Per capita income latest
Haya mengine ni mbwembwe Tu.Tunapima maendeleo Kwa watu,Siyo stand za bus,mabarabara au Viwanda.Pwani Wana Viwanda vingi lakini ndiyo Mkoa maskini.
 
IMG-20250214-WA0019.jpg
 
BALOZI WA URUSI: PARACHICHI ZA TANZANIA ZITAPATA SOKO RAHISI NCHINI URUSI

Balozi wa Shirikisho la Urusi nchini Tanzania, Mhe. Andrey Avetisyan, amewasili mkoani Njombe kwa ziara rasmi, ambapo alipokelewa katika eneo la Makambako na Mkuu wa Wilaya ya Njombe, Mhe. Juma Sweda, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Njombe, Mhe. Anthony Mtaka. Mapokezi hayo yamefanyika asubuhi ya leo, huku viongozi mbalimbali wa serikali na sekta binafsi wakishiriki katika kumpokea mgeni huyo muhimu.

Baada ya mapokezi, Mhe. Balozi Avetisyan alielekea kwenye kiwanda cha AVO Afrika, ambacho kinasindika na kukamua mafuta ya parachichi. Ziara hiyo inalenga kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Urusi, hususan katika sekta ya kilimo na viwanda. Akizungumza wakati wa ziara hiyo, Mhe. Balozi amesema kuwa Mkoa wa Njombe ni miongoni mwa mikoa mikubwa inayozalisha parachichi kwa wingi nchini Tanzania, na akasisitiza kuwa parachichi za Tanzania hazitakumbwa na pingamizi lolote kuingia nchini Urusi.

"Njombe is one of the largest avocado-producing regions in Tanzania, and I can confidently say that Tanzanian avocados will face no obstacles in entering the Russian market. As the Russian Ambassador, I am now ready to bring Russian investors to Njombe to explore and invest, particularly in the areas of industrial development and modern agriculture," alisema Mhe. Balozi Avetisyan.

"Njombe ni moja ya mikoa mikubwa inayozalisha parachichi nchini Tanzania, na nina uhakika kwamba parachichi za Tanzania hazitakumbwa na vikwazo vyovyote kuingia katika soko la Urusi. Kama Balozi wa Urusi, sasa niko tayari kuwaleta wawekezaji wa Kirusi kuja Njombe kutazama fursa zilizopo na kuwekeza, hususan katika eneo la ujenzi wa viwanda na kilimo cha kisasa," alisema Mhe. Balozi Avetisyan.
 
Mkuu, umeshafika Njombe?

Nimekaa Geita zaidi ya mwaka mmoja. Hapa Njombe sina hata mwezi mmoja. Nimeona utofauti mkubwa sana.

Siwasifii, ila naona kama kiwango cha uelewa wa watu wa huku ni mkubwa pia. Ni watu "wanaojielewa". Wana miili ya kawaida na akili "kubwa"
Ukweli ndio huo, mkoa wa Njombe una utofauti wa kipekee. Mimi pia nilishangaa kuona hakuna nyumba za nyasi wala vyoo vibaya vya ovyo.
 
Dhahabu NI hot keki inafuatwa na yeyote mwenye nguvu na mwenye pupa...wajanja na werevu sana... Alafu wanatapua NI non renuwable aset ikiisha imeisha...kwa hio hawafikirii kuwekeza sana zaidi ya kuioata hio dhahabu..
 
Back
Top Bottom