GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa

Vyombo vya dola vijitafakari na vijisafishe. Wakati watu wanaripoti watoto kupotea hawakuonesha juhudi zozote za kukabiliana na wimbi hilo. Sasa ndio hayo ya kujichukulia sheria mkononi ambayo haifai. Something must be done.
 
Kanda ya ziwa,hali sio shwari.
Jawaelewi bibi yule anafanya nini!
Hali sio
 
Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita vurugu zilizoanzia katika eneo la mnada wa Lulembela baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa katika mnada huo kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambuilia, ndipo akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika kituo cha Polisi Lulembela.

Ambapo baada ya watu hao kufikishwa katika kituo cha polisi, wananchi hao walifika katika kituo hicho na kuwataka askari polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue na Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili watu hao watawanyike

"Mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, wananchi hao walichoma moto gari moja lenye namba za usajili T.440 ATW aina ya Toyota Cardina lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo hicho na katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni msichana aitwaye Teresia John mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi," imeeleza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hata hivyo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wamebeba watoto hao ni Emanuel John (33) mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba mtoto aitwaye John Emanuel mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane, Mama wa watoto hao aitwaye Rachel Luhende (22) amethibitisha kuwa watoto hao ni wakwake na walikuwa kwa wifi yake ambapo baba yao mzazi na mjomba wao walikwenda kuwachukua,".

#EastAfricaRadio
Wananchi waanze kupambana pia na wasiojulikana.

Akija bila utambulisho basi iwe halali ya jamii
 
Taarifa ya Polisi inaonyesha hao ni wazazi, je ni kweli au si kweli?
Kuhusu watu wangapi katika matukio hayo wengi huwa wanaenda na upepo tu pasipo kuujua ukweli.
Wanaweza wakaanzisha wawili lakini mamia wakafuata mkumbo. Kwani wezi anavyopigwa mitaani watu wote huwa wanajua hata kilichoibwa au aliyeibiwa? Si hufuata tu zile kelele za tuhuma
Umenikumbusha Temeke Sandali aliwahi uliwa mtu akidhaniwa mwizi na hakuwa mwizi.
 
Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao
Wao polisi hawachukui sheria mkononi?
Tangu lini polisi akaaa na busara ya kusema hayo?
 
Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita vurugu zilizoanzia katika eneo la mnada wa Lulembela baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa katika mnada huo kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambuilia, ndipo akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika kituo cha Polisi Lulembela.

Ambapo baada ya watu hao kufikishwa katika kituo cha polisi, wananchi hao walifika katika kituo hicho na kuwataka askari polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue na Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili watu hao watawanyike

"Mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, wananchi hao walichoma moto gari moja lenye namba za usajili T.440 ATW aina ya Toyota Cardina lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo hicho na katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni msichana aitwaye Teresia John mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi," imeeleza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hata hivyo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wamebeba watoto hao ni Emanuel John (33) mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba mtoto aitwaye John Emanuel mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane, Mama wa watoto hao aitwaye Rachel Luhende (22) amethibitisha kuwa watoto hao ni wakwake na walikuwa kwa wifi yake ambapo baba yao mzazi na mjomba wao walikwenda kuwachukua,".

#EastAfricaRadio
Huo ukanda wagombea wa ccm ni wachawi na waganga bila kafara uchaguzi 2025 hawatoboi.
 
Tanzania wapumbavu tuko wengi, kuna watu wana walaumu polisi sasa unajiuliza kosa la polisi ni lipi hapo

kuwahifadhi watuhumiwa ambao wametuhumiwa kwa hisia tu
 
Wewe ndio hurlrwi na ni mpumbavu zaidi.

Hapa point sio tukio la leo bali matukio yaliyotangulia ndio yamepelekea tukio la leo na ndio msingi wa majadiliano haya.
 
Kadri kunavyozidi kupambazuka giza linaongezeka ila lazima pakuche tu
 
Taarifa ya Polisi inaonyesha hao ni wazazi, je ni kweli au si kweli?
Kuhusu watu wangapi katika matukio hayo wengi huwa wanaenda na upepo tu pasipo kuujua ukweli.
Wanaweza wakaanzisha wawili lakini mamia wakafuata mkumbo. Kwani wezi anavyopigwa mitaani watu wote huwa wanajua hata kilichoibwa au aliyeibiwa? Si hufuata tu zile kelele za tuhuma
Uko sawa lkn jeshi letu lilipifikia Hadi Sasa kuaminika vigumu mno hata alikuambia Sasa Hivi ni saa7 usiku Toka Nje kwanza ukashuhudie ndivho kinachofanyika Sasa Hivi ha waaminiki.

Watu wanahimidhana akija police kukuchukua usiende heri akuulie hapo hapo familia inaona. Kwa Hali hii ni kiasi Gani jeshi haliaminiki Tena?
 
Back
Top Bottom