GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa

Polisi wanatakiwa wajenge mazingira ya kuaminiwa. Wasipoaminiwa, hata pale ambapo wapo sahihi, wananchi hawatawaamini, na watafanya wanachokiamini wao.

Ona sasa, vijana wawili umri mdogo kabisa wamepoteza maisha yao bila ya kuwa na hatia yoyote.

Baba wa Mbinguni tunaomba uwaonee huruma vijana hawa waliouawa katika tukio hili, uwape pumziko jema katika katika ufalme wako.
 
Taarifa inasema waliokufa ni watu wawili, mvulana 18-20 na msichana wa 4m4 naye miaka 18. Je wameuawa kwa risasi za moto au sababu nyingine? walikuwa kwenye vurugu za kituo cha polisi au nje ya kituo? Polisi na mauwaji ya raia haviendani hata kidogo.
 
Madhara ya kuleta spirit Mbaya ya kuteka watu, kupoteza watu na kuua watu ndio hayo.
Tabia hiyo inashuka hadi ngazi ya chini ya mtaani.
Nani ameanza kuleta hizo tabia ovu nchini?

Hay sina sasa taharuki kwenye jamii.
Matukio ya kuteka, kupotezwa, mauaji yanatosha mikoani mbalimbali na mijini? 🤔
 
Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita vurugu zilizoanzia katika eneo la mnada wa Lulembela baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa katika mnada huo kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambuilia, ndipo akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika kituo cha Polisi Lulembela.

Ambapo baada ya watu hao kufikishwa katika kituo cha polisi, wananchi hao walifika katika kituo hicho na kuwataka askari polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue na Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili watu hao watawanyike

"Mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, wananchi hao walichoma moto gari moja lenye namba za usajili T.440 ATW aina ya Toyota Cardina lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo hicho na katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni msichana aitwaye Teresia John mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi," imeeleza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hata hivyo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wamebeba watoto hao ni Emanuel John (33) mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba mtoto aitwaye John Emanuel mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane, Mama wa watoto hao aitwaye Rachel Luhende (22) amethibitisha kuwa watoto hao ni wakwake na walikuwa kwa wifi yake ambapo baba yao mzazi na mjomba wao walikwenda kuwachukua,".

#EastAfricaRadio
Kipindi cha kampeni wananchi wakielezwa ukweli kuhusu mfumo na utendaji wa swrikali ulivyo mbovu sidhani kama CCm itapata kura labda waibe
 
Watu wa vijijini ni wa hovyo sana na ujinga wao umesababisha kumpoteza Maisha ya watu wasio na hatia. Nakumbuka wale watumishi wa idara ya kilimo kule Dodoma waliuawa kikatili kwa kuhisiwa freemason. Halafu mamlaka zipo kimya matapeli wanaotengeneza illusion za freemason na kubandika mijini na kuweka namba zao za simu Hawa ndio huwajaza ujinga wanakijiji
 
Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita vurugu zilizoanzia katika eneo la mnada wa Lulembela baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa katika mnada huo kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambuilia, ndipo akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika kituo cha Polisi Lulembela.

Ambapo baada ya watu hao kufikishwa katika kituo cha polisi, wananchi hao walifika katika kituo hicho na kuwataka askari polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue na Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili watu hao watawanyike

"Mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, wananchi hao walichoma moto gari moja lenye namba za usajili T.440 ATW aina ya Toyota Cardina lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo hicho na katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni msichana aitwaye Teresia John mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi," imeeleza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hata hivyo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wamebeba watoto hao ni Emanuel John (33) mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba mtoto aitwaye John Emanuel mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane, Mama wa watoto hao aitwaye Rachel Luhende (22) amethibitisha kuwa watoto hao ni wakwake na walikuwa kwa wifi yake ambapo baba yao mzazi na mjomba wao walikwenda kuwachukua,".

#EastAfricaRadio
Kwanza hii idadi mmeijuaje kama ni 800 takwimu zenu Zina mashaka
 
Utakuta walikua wanawahoji kwa kilugha cha kwao baada ya kuona ni waswahili wakawageuzia kibao
Wewe unaweza kuwa sahihi. Hii hali huku ipo ukitiliwa mashaka halafu hujui kilugha ukajieleza kwa kiswahili inaweza kuwa risk, watu wanaweza kukugeuzia
 
Ndo uhalisia huyo binti alieuwawa nyumba yao ipo karibu na kituo kwahiyo probably alikua kwenye perimeter ya nyumba yao au alisogea kituoni kuona kuna nini.

Unajua sisi wananchi kuna mambo huwa hatuelewi pengine ni uelewa mdogo wa sheria, katika kujichukulia sheria mkononi kuna mazingira polisi hata akikuua hataulizwa maana kuna mazingira sheria imemruhusu polisi afanye hivyo mfano wa sheria hiyo ni Sect 21(2) CPA cap 20 RE 2022 hapo anaruhusiwa kutumia nguvu na ikiwezekana kuua kwaajili ya kutetea uhai wake au uhai wa mtu mwingine.

Sasa ni vyema tukaepuka mazingira flani flani ya sisi kuonekana ndo tulikua wahalifu, juzi tu hapa aliuwawa Mandojo kwenye hizi hizi Mob justice, leo tena mtu anataka auwawe kisa kabeba mtoto wake
Hii yote ni vile polisi hawaaminiki kwenye jamii yetu.

Watanzania ni waelewa sana tena ikitokea mtu wanaimani naye walaaa!

Utakuta kunamatuko mengi ya watoto kuibiwa au kupotea chaajabu polisi hwajafanya jitihada zozote.. unategemea nini mkuu? Kama kilichotokea.

Polisi wanashindwa kuaminika kwa sababu ya njaa leo huwezi kwenda kutoa taarifa ya waouvu maana hao waovu wanakula na polisi. Ukitoa taarifa wanakugeuka. Hawa viumbe polisi kuwatetea ni ngumu sana?

Uzuri wananchi unaweza kuwafanyia mengi maovu wakawa kama hawaoni wakipata golden chance utaona kila aina ya rangi
 
Waloua ndio wanatoa maelezo ya kutaka kueleweka kwa kosa ku wa walofanya maana ni kinyume na misingi ya haki za binadamu.
Tunahitaji kuwasikiliza wananchi waelezee ukweli wa hali halisi ilivyokuwa.
hao wataelezea ili kutafuta kueleweka jambo ambalo ni vigumu.
Gari unaweza kununua lingine binadamu je ? Utamnunua wapi?
 
Nchi hii imeridhia kuingia mikataba ya umoja wa mataifa ya kulinda, kutunza na kuhifadhi haki za binadamu.
Mojawapo ya haki ya msingi ya binadamu ni kuwa “kila binadamu anayo haki ya kuishi” na sio kudhuriwa wala kuuliwa.

kila askari Polisi anapaswa kuwa na uhahamu huo wakati wote mazingira yote anapotimiza majukumu yake.

Na hata miongoni mwa raia wote elimu hiyo inapaswa kujulikana.
 
Nchi hii imeridhia kuingia mikataba ya umoja wa mataifa ya kulinda, kutunza na kuhifadhi haki za binadamu.
Mojawapo ya haki ya msingi ya binadamu ni kuwa “kila binadamu anayo haki ya kuishi” na sio kudhuriwa wala kuuliwa.
Watu watakuwa wanatoana uhai tu

Ova
 
Watu wa vijijini ni wajinga na hatari sana. Ukiwa kijijini kaa kwa machale, kuna ujinga wa kijumuia.
Nmecheka kwenye msiba
Aisee mpaka wazo langu la kuishi vijijini limenikata.. kuna matukio ma3 yamenichosha 1. Yule mganga alokua anaua watu na wenzie wanawazika wamekaa
2. Mauaji mauaji tu yasioeleweka na uvamizi
3. La leo hili wamefata mkumbo matokeo ndo hayaa
Aisee 🤣🤣 nmecheka kama mazuri
 
Wananchi wakiona umebeba mtoto basi jiandae vitambulisho na ueleweke.

Maana Polisi na serikali zimeshindwa ulinzi.
Hao watu wawili mpaka wanavamiwa wameshindwa kujitetea kuwa hao watoto ni wakwao?
Kwenye vurugu atakusikiliza nani mkuu?? Unauwawa bila hatia
 
Back
Top Bottom