GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa

GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa

Kwenye vurugu atakusikiliza nani mkuu?? Unauwawa bila hatia
Unajua mambo huwa yanaanza Taratibu.....unaulizwa mwanzoni na watu wachache hao watoto unawapeleka wapi? Unaanza ujeuri wa kujibu unavyotaka.

.sasa mimi watoto wakiwa wangu natoa majinu yaloyonyooka na wala sihitaji kugombana na watu...unakumbuka yule RC aliyeulizwa alete Vyeti vyake vya Form Four?

Badala ya kuweka mezani hata kama vina Division 4 akaansa kugombana na kila mtu. Wakati jibu moja tu lingemaliza majadala.
 
Unajua mambo huwa yanaanza Taratibu.....unaulizwa mwanzoni na watu wachache hao watoto unawapeleka wapi? Unaanza ujeuri wa kujibu unavyotaka...
HIi taarifa nilichogundua ni wananchi kuna muda hawana uelewa mzuri wa mambo.. Tuna mihemko mnoo kuna kaka angu alizushiwa mwizi wa pikipiki sekunde kadhaa watu wakamvamia et kisa kijana mmoja amesema yule jamaa ndo aliniibia pikipiki!

Watu wakaanza vurugu kwakua Siku zake hazikufika difenda la polisi likawa around wakamkamata kumtia kituoni wananchi wakajaa nje mtoeni mtoeni rusha maweee! Na hio sio mkoa ni hapa Dar tena katikati ya mji...

Ikabi mambo ya reinforcement polisi wa Central kariakoo wakaja wako full kumhamisha ndo ikawa pona yake , akakaa central uchunguzi ukafanyika na yule kijana aliemnyooshea kidole kuwa mwizi hakuonekana tena baada ya kitambo fulani akaachiwa mana walifatilia kila mahala akawa clean! Sasa imagine angekua mkoa?

Sehemu ambayo hakuna reinforecemnt wale polisi wangepigwa wameuwawa na mtuhumiwa! Hii dhana ya sheria mkononi sio njema!

Polisi hawana wema ila kuna mambo wananchi tujitafakari!

Nchi imekua kama taifa stars haina muunganiko
 
#HABARI Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita vurugu zilizoanzia katika eneo la mnada wa Lulembela baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa katika mnada huo kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambuilia, ndipo akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika kituo cha Polisi Lulembela.

Ambapo baada ya watu hao kufikishwa katika kituo cha polisi, wananchi hao walifika katika kituo hicho na kuwataka askari polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue na Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili watu hao watawanyike

"Mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, wananchi hao walichoma moto gari moja lenye namba za usajili T.440 ATW aina ya Toyota Cardina lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo hicho na katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni msichana aitwaye Teresia John mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi," imeeleza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hata hivyo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wamebeba watoto hao ni Emanuel John (33) mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba mtoto aitwaye John Emanuel mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane, Mama wa watoto hao aitwaye Rachel Luhende (22) mkazi wa Kigamboni Lulembela amethibitisha kuwa watoto hao ni wakwake na walikuwa kwa wifi yake ambapo baba yao mzazi na mjomba wao walikwenda kuwachukua,".

#EastAfricaTV
FB_IMG_1726088111438.jpg
 
Hilo tukio wamelitengeneza maksudi kutuamisha akili katika mauaji ya ndugu yetu mpendwa Ally Kibao. Tumeshawashtukizia.

Hata wakifanikisha mpango wao wa kumtumia mwijaku akirekodiwa anatatuliwa rinda na kunya hadharani bado tuu hatutakubali.
 
Nmecheka kwenye msiba
Aisee mpaka wazo langu la kuishi vijijini limenikata.. kuna matukio ma3 yamenichosha 1. Yule mganga alokua anaua watu na wenzie wanawazika wamekaa
2. Mauaji mauaji tu yasioeleweka na uvamizi
3. La leo hili wamefata mkumbo matokeo ndo hayaa
Aisee 🤣🤣 nmecheka kama mazuri
Wanachosha sana. Kuna wengine kule Mara waliandamana kung'oa ile miti ya ngazi ngazi inaitwa panga uzazi. Eti ina mikosi na inasababisha watu kufa!!
 
Maumivu ya kichwa huanza taratiibu..tutafika tu pale watawala wanataka tufike..haya mambo yanakolezwa na kukosekana kwa imani kwenye vyombo vyetu vya dola..Mimi hao.wananchi hata siwalaumu
 
Hilo tukio wamelitengeneza maksudi kutuamisha akili katika mauaji ya ndugu yetu mpendwa Ally Kibao. Tumeshawashtukizia.

Hata wakifanikisha mpango wao wa kumtumia mwijaku akirekodiwa anatatuliwa rinda na kunya hadharani bado tuu hatutakubali.
Njombe kuna gari limekamatws na wahamiaji wawili wakiwa wanamfatilia mfanyabiashara wamuibie polisi imewanasa.🤣
Taarifa zitakua nyingi sana
 
Katika vitu vya ovyo wabongo hujaribu kufanya ni kuvamia vituo vya polisi vyenye mamia ya silaha na kujaribu kuiba na kuchoma chochote mle.

Silaha zikiibwa hapo kituoni mji hautakalika ujambazi , unyang,anyi , wizi Kwa silaha utaongezeka.

NB
Ni vyema wananchi wakaachana na mipango hii ya kuvamia vituo
 
Kuna kesi nyingi sana hapo waliokamatwa wajipange unaweza kujikuta unakula maisha yaliyobaki jela
 
Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani...
Vyombo vya usalama Hali hii mnaistawisha kwa kas nyie wenyewe
Absolutely.

Wananchi wanapopoteza imani dhidi ya vyombo vya dola na Serikali, matokeo yake huwa ndio haya.
 
Back
Top Bottom