GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa

GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa

Maskini na wapumbavu 800 wakijikusanya na kuamua lazima walete uharibifu. Katika hao washenzi 800 walioleta vurugu kuna ambao watakiona cha moto.
Haohao masikini na wapumbavu,kwa kadiri ya ufinyu wa akili zako,wakiamua ulale umevaa kama unaenda kusali hawashindwi.Kama unabisha,waulize wanajeshi hodari wa Misri kilichowakuta hadi wakakimbia na kuvua magwanda huku wanapiga yowe.🤔
 
Hapa Kuna maswali mengi kuliko majibu!! Watu 800+ wasingizie watu wawili kweli?
Kwahiyo hao watu 800 ndio wanawajua zaidi hao watoto kuliko wazazi wao ambao wamethibitisha kua hao watoto ni wao? punguza mihemko mkuu,just use a simple logic to understand it,

Wrong is wrong even if everyone is doing,and right is right even no one is doing it.
 
Haohao masikini na wapumbavu,kwa kadiri ya ufinyu wa akili zako,wakiamua ulale umevaa kama unaenda kusali hawashindwi.Kama unabisha,waulize wanajeshi hodari wa Misri kilichowakuta hadi wakakimbia na kuvua magwanda huku wanapiga yowe.🤔
Hamia Misri
 
Duh,Watu wamechafukwa kweli kweli.Sipati picha kama hali ikiwa hivyo kwenye kila eneo ambalo inaonekana haki haitendeki
 
Hizi ni salamu kuwa inawezekana.
Acheni kulishana ujinga mtaendela kuliwa kama kuku.

Si ni juzi tu apa aliuliwa raia ktk mazingira kama ayo ya kituo cha polisi!
Ni hatua gani raia mlichukua baada ya polisi kukatisha maisha ya hao raia ?

Si kila mmoja yupo kwake ameufyata mkia kmya huku mkiaziacha familia za wafiwa na majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao ?

Ni afadhali mgekinukisha basi kuwa hatua zichukuliwe kwa hao askar
ila ivo mnavyofanya vurugu mkiuliwa wawili watatu mnaishia kuufyata mkia sio poa.
 
Acheni kulishana ujinga mtaendela kuliwa kama kuku.

Si ni juzi tu apa aliuliwa raia ktk mazingira kama ayo ya kituo cha polisi?
Ni hatua gani raia mlichukua baada ya polisi kukatisha maisha ya hao raia ?

Si kila mmoja yupo kwake ameufyata mkia kmya huku mkiaziacha familia za wafiwa na majonzi ya kuondokewa na mpendwa wao ?

Ni afadhali mgekinukisha basi kuwa hatua zichukuliwe kwa hao askar
ila ivo mnavyofanya vurugu mkiuliwa wawili watatu mnaishia kuufyata mkia sio poa.
Acha akili zako za ajabu.Watauawa wote?Unawajua waru wakichukia na kuhamasishana wafanye jambo?Wewe baki nyumbani tu unachambua maharage mabovu.
 
Nimeuliza hii habari kutoka kwa bamdogo ambae yupo huko geita karibu na lilipotokea tukio kanambia ni kweli limetokea ila jamani kuna watu wajinga kupita kiasi sasa ndo nini hiki walichofanya
 
Sasa hapo kosa ni la police kweli?
Unataka kuvamia kituo Chenye silaha na mahabusu halafu uachwe?
 
Acha akili zako za ajabu.Watauawa wote?Unawajua waru wakichukia na kuhamasishana wafanye jambo?Wewe baki nyumbani tu unachambua maharage mabovu.
Hawauwawi wote ila ni faida gani wamepta baada ya kufanya izo vurugu zao apo kituo cha polisi?
 
Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita vurugu zilizoanzia katika eneo la mnada wa Lulembela baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa katika mnada huo kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambuilia, ndipo akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika kituo cha Polisi Lulembela.

Ambapo baada ya watu hao kufikishwa katika kituo cha polisi, wananchi hao walifika katika kituo hicho na kuwataka askari polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue na Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili watu hao watawanyike

"Mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, wananchi hao walichoma moto gari moja lenye namba za usajili T.440 ATW aina ya Toyota Cardina lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo hicho na katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni msichana aitwaye Teresia John mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi," imeeleza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hata hivyo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wamebeba watoto hao ni Emanuel John (33) mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba mtoto aitwaye John Emanuel mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane, Mama wa watoto hao aitwaye Rachel Luhende (22) amethibitisha kuwa watoto hao ni wakwake na walikuwa kwa wifi yake ambapo baba yao mzazi na mjomba wao walikwenda kuwachukua,".

#EastAfricaRadio

View attachment 3093573
Mambo haya yamelelewa na serikali ya Chifu Hangaya hadi imefika wakati sasa binadamu hatuaminiani. Mtendaji wa Kata ashukuriwe sana kwa kuokoa roho za wananchi hawa, vinginevyo wangeuawa.
 
Kuna wapuuzi walichoma moto vijana wa watu kisa ishu hizi hizi za kukurupuka. Wabongo kuna muda kama makondoo yakiona mwenzao kaanzisha yanafata tu bila kuhoji.

Aiseeee dooooh!
 
Back
Top Bottom