GEITA: Wananchi wavamia kituo Cha Polisi, wawili wauawa

Hilo tukio wamelitengeneza maksudi kutuamisha akili katika mauaji ya ndugu yetu mpendwa Ally Kibao. Tumeshawashtukizia.

Hata wakifanikisha mpango wao wa kumtumia mwijaku akirekodiwa anatatuliwa rinda na kunya hadharani bado tuu hatutakubali.
Tupate watu wa Geita wathibitishe maana unaweza kuta walikuwa ni wafungwa wametegeshwa ili kutuhamisha
 
Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita vurugu zilizoanzia katika eneo la mnada wa Lulembela baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa katika mnada huo kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambuilia, ndipo akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika kituo cha Polisi Lulembela.

Ambapo baada ya watu hao kufikishwa katika kituo cha polisi, wananchi hao walifika katika kituo hicho na kuwataka askari polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue na Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili watu hao watawanyike

"Mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, wananchi hao walichoma moto gari moja lenye namba za usajili T.440 ATW aina ya Toyota Cardina lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo hicho na katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni msichana aitwaye Teresia John mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi," imeeleza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hata hivyo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wamebeba watoto hao ni Emanuel John (33) mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba mtoto aitwaye John Emanuel mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane, Mama wa watoto hao aitwaye Rachel Luhende (22) amethibitisha kuwa watoto hao ni wakwake na walikuwa kwa wifi yake ambapo baba yao mzazi na mjomba wao walikwenda kuwachukua,".

#EastAfricaRadio

View attachment 3093573

Wangeuwa zaidi wawili hawatoshi
 
Kama Jambo halikuhusu kaa kimya. Unaongea kwa dharau bila kujua kilichotokea kwenye field. Usifanye dhihaka na damu za watu.
Damu za watu zipi wakati upumbavu wao umepelekea vijana kufa! Yani Mimi nibebe mtoto wangu unisuspect na utake kuniua, kwanini usinihoji kwanza!? Haya wamevamia kituo na watu wamekufa what's next?
 
hofu kila Kina kona watu hawaaminiani na polisi hawaaminiki kwa sabab ya matendo yao. Ona sasa hata mtu akimbeba mwanae anahisiwa na mtekaji au mwizi
 
Damu za watu zipi wakati upumbavu wao umepelekea vijana kufa! Yani Mimi nibebe mtoto wangu unisuspect na utake kuniua, kwanini usinihoji kwanza!? Haya wamevamia kituo na watu wamekufa what's next?
Shida ilipoanzia unajua?!!
 
Vijana wawili wamefariki dunia hii leo Septemba 11, 2024 baada ya wananchi 800 kuvamia na kufanya vurugu katika kituo cha polisi Lulembela wilayani Mbogwe mkoani Geita vurugu zilizoanzia katika eneo la mnada wa Lulembela baada ya watu wawili kuonekana wakiwa wamebeba watoto wawili na wananchi waliokuwa katika mnada huo kuwahisi kuwa ni wezi wa watoto na kuanza kuwashambuilia, ndipo akatokea Mtendaji wa Kata akawabeba kwenye pikipiki na kuwakimbiza katika kituo cha Polisi Lulembela.

Ambapo baada ya watu hao kufikishwa katika kituo cha polisi, wananchi hao walifika katika kituo hicho na kuwataka askari polisi wawakabidhi watuhumiwa hao ili wawaue na Askari walijaribu kuwaelimisha na kuwaeleza ni kosa na si vizuri kujichukulia sheria mkononi lakini walikaidi na baada ya askari kuona hali hiyo ya kuhatarisha maisha ya watu na mali za serikali walitumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya watu hao na iliposhindikana walitumia silaha za moto kwa kupiga risasi juu ili watu hao watawanyike

"Mbali na kushambulia kituo hicho kwa mawe na kutaka kuingia kwa nguvu ndani ya kituo hicho, wananchi hao walichoma moto gari moja lenye namba za usajili T.440 ATW aina ya Toyota Cardina lililokuwa limeegeshwa nje ya kituo hicho na katika vurugu hizo watu wawili wamepoteza maisha, mmoja ni mwanaume anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka 18 hadi 20 na wa pili ni msichana aitwaye Teresia John mwenye umri wa miaka 18, mwanafunzi wa kidato cha nne Shule ya Sekondari Lulembela ambaye nyumba yao inatazamana na kituo hicho cha Polisi," imeeleza taarifa ya Msemaji wa Jeshi la Polisi nchini

Aidha taarifa hiyo imeongeza kuwa, "Hata hivyo, ilibainika kuwa watu waliokuwa wamebeba watoto hao ni Emanuel John (33) mkazi wa Kigamboni Lulembela ambaye alikuwa amembeba mtoto wake aitwaye Ikram Emanuel mwenye umri wa mwaka mmoja na miezi kumi na moja na wa pili anaitwa Ng'amba Leonard (24) ambaye alikuwa amembeba mtoto aitwaye John Emanuel mwenye umri wa miaka miwili na miezi nane, Mama wa watoto hao aitwaye Rachel Luhende (22) amethibitisha kuwa watoto hao ni wakwake na walikuwa kwa wifi yake ambapo baba yao mzazi na mjomba wao walikwenda kuwachukua,".

#EastAfricaRadio

View attachment 3093573

Wasukuma shida Sanaa yaan Kuna muda wanakuaga too emotional

Enzi zile za MANYONYA DAMU huko usukumani walikua wakiona LAND CRUISER linapita shuleni au barabarani wanakimbia au kufuata watoto wao shuleni.

Shida Sana hao WATU wasukuma ILLITERATE ni wazito Sana KUELEWA
 
Watu 800 hawawezi kukosea
Huwajui wabongo kwa kufata mkumbo wewe.
Hata watu 10,000 wanaweza kukosea tu, wangapi wanauawa kwa kuitiwa kelele za mwizi hadi kuuawa na kumbe sio wezi??

Hii tabia ya kupigia watu kelele na kuwashutumu ni wahalifu halafu mnawaua bila uthibitisho wowote ni mbaya sana hii, wengi wasio na hatia wanauawa kwa dizaini hii.

Hao wenyewe wamethibitishwa sio wezi mmoja ni baba wa mtoto, mwingine ni mjomba wa mtoto. Labda kisa hawafahamiki mtaa huo na watoto wanafahamika tayari washaitiwa ni wezi wa watoto.

Ujinga mtupu.
 
Wasukuma shida Sanaa yaan Kuna muda wanakuaga too emotional

Enzi zile za MANYONYA DAMU huko usukumani walikua wakiona LAND CRUISER linapita shuleni au barabarani wanakimbia au kufuata watoto wao shuleni.

Shida Sana hao WATU wasukuma ILLITERATE ni wazito Sana KUELEWA
Hii inaleta hofu kwa wageni wanaotaka kwenda huko, na mbaya zaidi ni kua mtu huwezi kujitetea wakishakuhusi na huo mtaa hufahamiki.

Utaulizwa maswali mfululizo na kutopewa nafasi ya kujibu zaidi ya kipigo tu.
 
Shida inaanzia hapo yaan unauwawa huku unajiona ni pakwenda na tahadhari kubwa au uwe na mwenyeji wa hapo anae fahamika otherwise unaumia kweupee
 
Kazi kweli. Inakuwaje unaona watu wamebeba watoto mnawavamia na kuanza kuwapiga. Hii mihemuko ya makundi itatupeleka pabaya.
 
Mob justice inaanza tuliyasema humu.
Mob justice ipo sana Tanzania, lakini unakuta wengi waliouawa hawana hatia , ni mihemuko tu. Mfano kwa mwaka jana zaidi ya watu 500 wameuwawa sababu hiyo (LHRC report). Watanzania hawawezi kuandamana hata bei ya mafuta au sukari au wizi wa mabilioni inayofanywa na baadhi ya watumishi wa serikali ambavyo kwa asilimia kubwa vinaathiri maisha yao na kupelekea mwananchi kuwa maskini na kuendelea kuwa wajinga.
 
Back
Top Bottom