General Tyres Tanzania ilivyohamishiwa Kenya na kuitwa YANA tyres!

Ombeni SEfue aliwai sema kiwanda kitafunguliwa kabla ya mwisho wa mwaka(that was sept/oct 2015 baada ya serikali kuwa na 100% shares) ndo imebaki kesho tuu watu wa Arusha tupeni updates pls kinafanya kazi?
 
Nilinunua tairi nne za dunlop toka South africa, miezi mi4 tu zote zimevimba, hiki cha kwetu kimefika wapi?
 
Wananchi tulielezwa kwa uwazi kabisa enzi za Wahe. Kigoda (Marehemu), Mary Nagu waliokuwa Mawaziri wa Viwanda na Biashara enzi hizo kuwa Kiwanda cha General Tyre Arusha tayari Serikali inaimiliki kwa asilimia 100 na itafunguliwa katika mwaka wa fedha 2014/15 na kuanza kazi. Mpaka leo Kiwanda hakijafunguliwa na hakifanyi kazi. Tunaiomba Serikali itutake radhi kwa kutotimiza ahadi yake kama ilivyoahidi.
 
Inasikitisha mno kupeana ahadi za uongo as if sisi ni watoto, haipendezi, tuombwe radhi!
 

Na mgodi wa Phosphate wa Minjingu, Viwanda vya Chumvi, etc
 
 
General tyre ilikufa sababu ya matairi kutoka nje yalipoachiwa kuingia kwa wingi na yenye ubora sawa na General tyre.
 
"Serikali yatenga milioni 70 kwa ajili ya kufufua kiwanda cha matairi cha General tyres"

Source: Power breakfast ya clouds radio (18/05/2017)
 

Bungeni: Waziri Mpango asema Serikali imetenga bajeti 2017/18 kufufua kiwanda cha General Tyre
 
Miaka miwili ya Tanzania ya viwanda, mchakato wa hiki kiwanda umefikia wapi? naomba kujuzwa kwa mwenye taarifa
 
Ombeni SEfue aliwai sema kiwanda kitafunguliwa kabla ya mwisho wa mwaka(that was sept/oct 2015 baada ya serikali kuwa na 100% shares) ndo imebaki kesho tuu watu wa Arusha tupeni updates pls kinafanya kazi?
Huwezi amini, hii ni 2018 na hakuna dalili..!
 
Daah ni hatari..nani alietulaani jamani?kuna mchwa wameila nchi hii mpk imebaki skeleton
 
"NSSF ikatoa mkopo wa dola 10 milion Serikali ikiwa mdhamini wa mkopo huo. Badala ya kununua mitambo mipya mitambo ya zamani ikapakwa rangi na fedha zote zikatokomea. Utashangaa leo unaambiwa deni la Taifa linazidi kuongezeka ukichunguza utakuta linaongezeka kwa mambo kama haya". Wakati mwingine matatizo ya africa yanachangiwa na waafrika wenyewe na si kweli kama tulivyoaminishwa kwenye somo la historia kwamba wakoloni ndio walitifanya maskini,Mkoloni mweusi ni mbaya kuliko mkoloni mweupe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…