Generation "Z" Wanajipa Umuhimu Wasiokuwa Nao..."Stay Humble Guys"

Ndicho hasa nilichoandika. Muhimu waache kudharau vizazi vilivyowatangulia na kujiona kama wao ndo wanaanzisha dunia. Dunia ipo na waliikuta, wasione vizazi vilivyopita ni Washamba!
Labda wanaona vizazi vilivyo tangulia avifanyi maisha vile inavyo takiwa
 
Dah kulalek
Mimi ni wa kuwekwa grup moja na vitoto vya elfu mbili na kumi na mbili kweli? 🥲

Cc BICHWA KOMWE - , Maghayo, litutumbwe
 
Sio kilakitu cha kujifanya mjuaji mzee huna hoja ya maana katika hili.
Nimeandika hoja zangu, nimeweka mpaka link inayoelezea Generations hizi na historia zake, Kimarekani.

Hujatoa hoja yoyote ya kupinga hoja zangu nilizozitoa.

Hata sielewi unapinga nini, kwa sababu gani.

Unapinga ovyo ovyo tu.

Yani hata siwezi kukujibu kwa hoja.

Kwa sababu hujatoa hoja.

Imwtoa tu ad hominem logical fallacy.

Wewe ndiye huna hoja hapa.

Ila nyani haoni kundule.
 
Kumbe mimi ni Alpha! mungu yuko nami.
 
Kwa maelezo haya, kila nchi inaweza kucategorize hivyo vizazi kulingana na historia yake.

Hata hii Gen Z yenyewe kibongobongo haijakamilika, mpaka leo kuna vijiji umeme hamna, kule kwa babu tale mpaka mwaka jana kulikua hamna mtandao wa simu sijui kama uliwekwa.

Labda hivyo vizazi waviweke kimjinimjini tu hasa daslam.
 

Kuna Watanzania wengi wanapenda kuigaiga vitu hata bila ya kuvielewa.

Kuna mtu kasema GenZ zinafanana kwa fourth industrial revolution, mambo ya internet na artificial intelligence.

Nikamwambia huko Malampaka hakuna hizo habari za fourth industrial revolution wala artificial intelligence.
 
Hatuendani nao kabisa hao watu.
Basi tu ni kwakua tunaiga.

Na kwenye hiyo article uliyoweka hapa, Gen Z wako aware na mambo mengi kuhusu tech na mambo ya siasa, sasa hapa kwetu nani aliezaliwa miaka ya 2000 anafatilia siasa??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…