Genge la Kihalifu la Sabaya, ni kweli Hayati Magufuli hakulijua? OCD Hai unafanya nini kazini mpaka muda huu?

Genge la Kihalifu la Sabaya, ni kweli Hayati Magufuli hakulijua? OCD Hai unafanya nini kazini mpaka muda huu?

Ni maswali tata sana mbayo tungependa kumuuliza Shujaa. Ni kweli hakujua kuwa mteule wako anatuhumiwa na kufadhili genge la kihalifu?.
-Kama alijua basi kuna haja ya wananchi Kufungua kesi dhidi ya Rais wa JMT aliyepita kwa kubariki kufanyika uhalifu dhidi ya binadamu kwa raia alioapa kuwalinda.
-Kama si kweli basi kuna haja ya watu wanaohusika na Intelijensia kwa viongozi ya usalama na vetting kuwajibika kuanzia TISS mpaka jeshi la polisi.
-Mpaka muda huu sidhani kama OCD wa hai anapaswa kuwa ofisini kwa hili suala la mkuu na swahiba wake.
-Tume ya maadili ya watumishi wa umma mmetukosea sana watanzania, KUWAJIBIKA NI MUHIMU SANA

View attachment 1808431


Kwa upande mmoja uko sahihi kumlaumu OCD kwa mantiki ya kuwa angeweza kuwa na Moral authority kuacha kaz kipindi kile .. narudia kuacha mwenyewe kazi kuonesha uwdilifu wa kiutendaj ili kupinga. vitendo hivyo vinavyosemwa vimefanywa na sabaya.

ila kama unamlaumu na kutaka awajibishwe sababu alifumbia macho hayo mambo basi kumbuka aidha kutokana na katiba yenu au sheria zenu ambazo ni za muundo wa de facto..
basi OCD simply anachukua amri kutoka kwa mkuu wa wilaya.. infact achilia mbali OCD hata huyo IGP utashangaa anachukua amri kwa mkuu wa wilaya sasa unategemea OCD amuwajibishe vip mtu ambaye sheria inasema ni Boss wake.

mkimbiwa kuna umuhimi wa kureview hizi sheria na katiba zenu ili kuleta uwiano katika accountability maana yake ni kuepuka mambo kama haya. hebu fikiri we kesho unaweza ukawekwa DC au RC automaticaly unapokea
salute na kuongoza kamati za kiusalama huku ukitoa amri kwa mtu ambaye yuko trained kusimamia sheria. a haki miaka yake yote.

yaan automaticaly mtu wa mtaani anapewa cheo cha kisiasa anapata nafasi ya kujua siri za kiusalama wa inchi. anapata access ya silaha yeye na watu wake.. tena ndo anakuwa na mamlaka kuliko hao ambao wamedidicate maisha yao kwenye mambo ya usalama..

dah ndo maana biashara haram haziwez kuisha had siasa itenganishwe na profesional ..
 
Mtu wa Hai anaenda kusomewa mashitaka Arusha ili iweje?
Hai hamna mahakama? Na mkoa wa Kilimanjaro je?
Wameogopa mafuriko ya watu mahakamani.

Mahakamani ni sehemu ya kutoa haki kwa hiyo ni vizuri amepelekwa huko ili sasa akina Mbowe wawe wanaenda mahakamani kutoa ushahidi juu ya madai yao.
Mbowe asipoenda kutoa ushahidi mahakamani tutajua ni unafiki tu

Hata Mbowe alikaa Segerea kwa miezi nne na madawa ya kulevya yakaisha mtaani
Hayo mashitaka aliyosomewa jana ni tuhuma alizotenda akiwa arusha, bado yaliyofanyika Hai na kwingine.
 
Aliwaamini
Walijua kucheza na akili yake
Wakawa wanafanya yao

Ova
 
Tiss wataonewa sana kwenye hilo, unadhani kipindi cha mwendazake nani aliweza kumshauri?
 
wote hao utakuwa unawaonea tu..

enzi hizo za mwendazake, yy ndiye sheria, yy ndiye katiba na vettung yy ndio anaifanya hata kama uliowataja walimwambia hafai

nao wanafamilia zinawasubiri, wapingane naye ile kwao?
hata ww ungeweza?
Naam. Mwendazake alikuwa ni kama Mfalme Louis XVI wa Ufaransa enzi za 1780s..."I am the State, the State it is me"
 
Huyo mama nae alipokuwa RC pale Kilimajaro alikuwa very weak ndio maana hakuwa na impact; hasa kwa Wilaya ya Hai, alipelekewa malalamiko mengi dhidi ya afisa Ardhi wa Hai kuwa corrupt lakini alishindwa kumchukulia hatua ingawa alikuwa anajua ukweli wa mashitaka hayo!
Utamuonea tu, mbele ya mwendazake?
 
Mtu wa Hai anaenda kusomewa mashitaka Arusha ili iweje?
Hai hamna mahakama? Na mkoa wa Kilimanjaro je?
Wameogopa mafuriko ya watu mahakamani.

Mahakamani ni sehemu ya kutoa haki kwa hiyo ni vizuri amepelekwa huko ili sasa akina Mbowe wawe wanaenda mahakamani kutoa ushahidi juu ya madai yao.
Mbowe asipoenda kutoa ushahidi mahakamani tutajua ni unafiki tu

Hata Mbowe alikaa Segerea kwa miezi nne na madawa ya kulevya yakaisha mtaani
Hujiulizi kwanini DC wa Hai Kilimanjaro aende kufanya uharamia mkoa mwingine? Kosa limefanyika Arusha halafu unataka kesi ipelekwe Hai kwa sababu ipi?

By the way Mbowe anaenda kutoa ushahidi kwa kosa lipi?
 
Kwa hili nawaza sana kuhusu Hayati JPM, aliwezaje kuona na kujua kwamba chanjo za COVID, BARAKOA ni hatari kwa Watanzania ila asijue uhalifu wa huyu Jambazi, JPM alikuwa anaipeleka hii Nchi kubaya sana, nina uhakika Mungu wa mbinguni aliona hili akaamua kutuepusha na shari mapema.
Mungu wa mbinguni hashindwi jambo. Kama alivyowatoa wana wa Israel kule Misri kwenye makucha ya Farao ndivyo alivyotutoa watanzania kwenye makucha ya uharamia wa awamu ya tano.

Tunashukuru kutuletea Mama mwenye huruma
 
Hujiulizi kwanini DC wa Hai Kilimanjaro aende kufanya uharamia mkoa mwingine? Kosa limefanyika Arusha halafu unataka kesi ipelekwe Hai kwa sababu ipi?

By the way Mbowe anaenda kutoa ushahidi kwa kosa lipi?
Nilivyoelewa kesi ya jana ni matukio ya Arusha, ya Hai hayajatajwa kabisa
 
Ilikuwa ni utawala muovu kupata kutokea
 
Walikuwa chini ya mwenyekiti wao wa kamati ya Ulinzi na Usalama wa Hai Sabaya
Kamati ya Ulinzi na Usalama wilaya ya Hai ina maswali ya kujibu.
Walikuwa wapi wakati uharamia wote ukifanyika?
 
Back
Top Bottom