George Simbachawene ni nani hasa?

Ukienda kibakwe baba yake anaogopeka hatari ni mtaalam maarufu sana huko
 
Kwa hiyo ni bahati tu? Huyu Elimu yake ikoje
Kama nia kubalance mbona sasa anapewa wizara nyeti?
Kwenye maisha kuna watu wana upepo tu unaweza ukafikiria ana ndumba kumbe wala hata hategemei ndumba na ndio hao ambao wanayumba yumba sana kazini.

Akipewa anafasi anakaa kwa mda flani anafitiniwa anatoka. Ila hakai sana anapata nyengine anafanya napo wakimfitini anaondolewa. Nahisi ndio aina ya personality ya Simbachawene. Unakuta hanaga noma na mtu ila wabongo wivu ukiwa na cheo ni kawaida.
 
Huyu kwao sawa ni Pwaga na Galigali pia ujombani namjua vyema akiwa kule Mbuga, Winza, Kinusi,Matonya,Ihwa,Maandazi,Ipera,Mang'alisa, Choghola, Kikuyu na Ihefu watu wa milimani mmenisoma huyu analingia uchawi wa baba yake.
Miaka yote mmekuwa mkisema hivyo anaringia uchawi wa baba yake. Baba yake alishafariki Sasa hivi huo uchawi anautoa wapi??
Simbachawene licha ya mapungufu yake lakini ana utu.
Kawasaidia vijana wengi Sana hasa kwenye kuwalipia ada na hata kuwatafutia michongo.
 
Mimi sio kiaxi kama umavyofikiria. Siwezi kutaja mtu hapa ila wapi na wanalalamika. Wakati amefiwa na mzazi wake uliudhuria kwenye msiba?
Wewe jamaa mbona kama nataka kukujua!!!!?[emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28][emoji28] Ulimsaidia kampeni baadae ukatoswa ukaanza kumpiga majungu fesibuku.
Kwenye msiba sikuhudhuria.
 
Huyu si ndiye alikuwaga anatukatisha tikiti za mabasi miaka ile huyu?.
Kwakweli huyu anaweza kuwa ni mfano wa hustlers maana tangu alivyoanza kupambana kwenye kukatisha tiketi kwenye mabasi ya Uda, kujiendeleza shule kupitia open university,kupambana na maisha Hadi kuingia kwenye siasa siyo kazi ndogo.
Jamaa amepambana Sana. Huwa ana moyo wa kumsikiliza mtu na kumsaidia lakini hapendi kupe(mtu anayemtegemea kwa kila kitu na Kila siku).
Anapenda akikusaidia uendelee na mapambano yako Sasa watu wengi wa jimboni kwake wanataka akiwasaidia Leo hili kesho akipata shida nyingine anamfikiria mheshimiwa. Jamaa anawachoka.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…