Gerald Hando amuuliza Januari, Dkt. Kalemani aliweza vipi umeme haukukatika?

Gerald Hando amuuliza Januari, Dkt. Kalemani aliweza vipi umeme haukukatika?

Moja ya sababu kwanini Umeme unakatika January amewadharau watu weledi katika sekta ya umeme tanesco hivyo wamemsusa kama alivyokata ulaji wao na Kuna hujuma kama zote maana huyo msambaa hana maarifa wala ujuzi wa umeme wameamuac mbwai na iwe mbwai
 
MTANGAZAJI MAHIRI nchini Tanzania, Gerald Hando amemuuliza Januari Makamba kwanini alipoingia kwenye Wizara hiyo umeme ukaanza kukatika hovyo kwanini asimuulize Kalemani aliwezaje.

"Januari Makamba tumuulize swali moja dogo sana Kalemani amekaa miaka 6 umeme haujakatika yeye ameingia tu umeme umeanza kufanya vurugu nini shida, kwanini asimuulize Kalemani alifanyaje?" amehoji Hando

"Si chama kimoja wale si wabunge wale, si Serikali moja wale kwanini asimuulize Kalemani alifanya nini, Januari Makamba amuulize Dk Kalemani ulifanyaje uliwezaje, tumekaa six years hapa hatujaona situation kama hii make wamesingizia maji sasa maji mafuriko mabomba yanapasuka" amehoji Hando
View attachment 2462435
Alikuwa hajalewa pombe? Maana huwa analewa mpaka analala kwenye meza za baa, wakati mwingine anabebwa mzegamzega kupelekwa nyumbani hajitambui
 
Kalemani umeme ulikuwa unakatika kila siku....lakini mmeshaanza kubadili facts ili agenda yenu ifanye kazi
Tuliza akili kidogo nikukumbushe,

Mlivyo pewa wizara umeme ukaanza kukatika mkasema nikwasababu mitambo ilikuwa haijafanyiwa service kwa kipindi kirefu.

Then mkasema unakatika kwa sababu ya ukame maji hamna.
Sasaivi maji yapo mnasaje!!!.

You guys are totally useless!.
 
Ila za ndani ni kuwa viwanda vingi viliumizwa kwa wakati huo maana viwanda hutumia umeme mwingi, vikikatiwa sio rahisi kupata kelele kama wananchi wakikatiwa
Huo ni uongo tungesikia malalamiko ya wafanyakazi waliocha kazi kwa sababu ya viwanda vyao kukosa umeme.. wafanyakazi ni wengi sana huwezi kuficha hiyo siri hata siku moja ingejulikana tu.
 
Akipigwa bega, mtamtetea?

....subirini, wamewezeshwa, halafu watshindwa kwa makusudi, halafu Watabinafsisha.

Waulizeni Wale Wananchi wa Nchi Wasio Wananchi Puetto Rikko kuna ya kujifunza kule
 
Who is behind Gelard hando?
watanzania wengi ni kama mataahira na mmoja wapo ni wewe,kwamba gerald hando anatumika na watu amchafue huyo waziri mpuuzi.jamaa ameshafuka kitambo tu sema system ya utawala imekaa ovyo jamaa alitakiwa awe jela sasa hivi kwa nchi zinazojitambua.maana kukata umeme makusudi ili kampuni yenu ipate wateja wa majenereta huo ni uhujumu uchumi na china walienda mbali zaidi adhabu ni kunyongwa
 
Hajui huyu hasara zilizosababishwa katika kipindi cha uwaziri wa januari, watu wamefilisika biashara zao zimekufa wauza barafu, wauza bucha za samaki, nyama, watu wa saluni za kike na za kiume, watu wa stationary, wauza juice, maji, watu wa kuchomelea mageti na vyuma mbalimbali na shughuli zote zinazotegemea umeme alafu yeye anakuja na stori nyepesi eti kuna mtu yuko nyuma ya hando?
 
Niliona mengi.
hasara zilizosababishwa katika kipindi cha uwaziri wa januari, watu wamefilisika biashara zao zimekufa wauza barafu, wauza bucha za samaki, nyama, watu wa saluni za kike na za kiume, watu wa stationary, wauza juice, maji, watu wa kuchomelea mageti na vyuma mbalimbali na shughuli zote zinazotegemea umeme alafu yeye anakuja na stori nyepesi eti kuna mtu yuko nyuma ya hando?
 
Mbona walishasema kwanini mgao haukuwepo wakati wa mwendazake. According to Makamba
1. Serikali ya Magu ililazimisha viwanda vipunguze uzalishaji ili kupunguza demand
2. Hawakufanya maintenance

Kama ni ukweli au uongo wanajua wao
 
Kama ni kweli viwanda vilipunguza uzalishaji kwanini hakukuwa na mfumko mkubwa wa bei za bidhaa kama sasa. maana ukipunguza uzalishaji bidhaa zinapungua sokoni na kusababisha ongezeko la bei
 
Kalemani umeme ulikuwa unakatika kila siku....lakini mmeshaanza kubadili facts ili agenda yenu ifanye kazi
Mkuu hilo si Kweli kwamba "umeme ulikua unakatika kila siku" Ulikuwa unakatika kwa kiwango cha kawaida, Sio kwa Mgao Rasmi kama ilivyo Sasa.

Tangu Hayati Magufuli amekuwa Rais nchi haikuwahi kuingia kwenye Mgao wa Umeme.

Huo ndio Ukweli ambao inabidi tuukiri.
 
Back
Top Bottom