Gerald Hando amuuliza Januari, Dkt. Kalemani aliweza vipi umeme haukukatika?

Gerald Hando amuuliza Januari, Dkt. Kalemani aliweza vipi umeme haukukatika?

Nashangaa sana kuna mlevi mmoja wa mataputapu hapa kilabuni kango ameropoka wazuri hawafi nimeshangaa January si mzuri lakini hafi nilipompigia simu Izraili akaniambia Mh February ana bonus ya twenty something years
 
Kalemani umeme ulikuwa unakatika kila siku....lakini mmeshaanza kubadili facts ili agenda yenu ifanye kazi
Ulikuwa unakatika na Tanesco hawakudhubutu kusema ni mgao au nini. Ilikuwa kimya tu. WaTz wasaulifu sana.

Kelemani ndo alikuwa anasema connection ya umeme ni 27k kila sehemu Tz, wakati Tanesco wana taratibu tofauti kabisa, ilikuwa usumbufu sana kwa watu.
 
Kama ni kweli viwanda vilipunguza uzalishaji kwanini hakukuwa na mfumko mkubwa wa bei za bidhaa kama sasa. maana ukipunguza uzalishaji bidhaa zinapungua sokoni na kusababisha ongezeko la bei
Nimeripoti kama alivyosema
 
Ulikuwa unakatika na Tanesco hawakudhubutu kusema ni mgao au nini. Ilikuwa kimya tu. WaTz wasaulifu sana.

Kelemani ndo alikuwa anasema connection ya umeme ni 27k kila sehemu Tz, wakati Tanesco wana taratibu tofauti kabisa, ilikuwa usumbufu sana kwa watu.
Ulipokua unakatika walikua wanatoa taarifa kwani tanesco wameanza kipindi gani kuwa na emergency service 24 hrs si kipindi cha kale tanesco wameanza kuwa na whatsapp groups za info si kipindi cha kale kwenye ukweli tuseme tu ila now makamba ni miyeyusho mitupu umeme unakatika hata kama wanatoa taarifa ila dah haikupaswa iwe hivi
 
Ni kweli kabisa kuwa kipindi Kalemani ni waziri huo umeme haukuwa shida? Haukuwahi kukatika?
Umeme ulikatika lakini haikuwa mara kwa mara lama sasahivi! Shida na hawa wanacho haribu visingizio ni vingi! Kipindi kile walituambia mitambo haikufanyiwa ukarabati sababu watu waliogopwa kufukuzwa kazi, ikaja story ya maji! Makamba akachukua chopa mpaka Mtera ila meneja wa Mtera alipiga nyundo ambayo uenda anajilaumu kwann hakumuweka pemben kabla ajaenda! Maana Meneja alimueleza wazi kuwa bado wanaweza kuzalisha MW 80 kama kawaida mpaka miezi 7 mbele atakama mvua hazitanyesha!

Sasa hizi issue ndo zinazaa maswali kwa Makamba!
 
MTANGAZAJI MAHIRI nchini Tanzania, Gerald Hando amemuuliza Januari Makamba kwanini alipoingia kwenye Wizara hiyo umeme ukaanza kukatika hovyo kwanini asimuulize Kalemani aliwezaje.

"Januari Makamba tumuulize swali moja dogo sana Kalemani amekaa miaka 6 umeme haujakatika yeye ameingia tu umeme umeanza kufanya vurugu nini shida, kwanini asimuulize Kalemani alifanyaje?" amehoji Hando

"Si chama kimoja wale si wabunge wale, si Serikali moja wale kwanini asimuulize Kalemani alifanya nini, Januari Makamba amuulize Dk Kalemani ulifanyaje uliwezaje, tumekaa six years hapa hatujaona situation kama hii make wamesingizia maji sasa maji mafuriko mabomba yanapasuka" amehoji Hando
View attachment 2462435
Huku ni kumnanga tuu bure JM, hili la kukatika kwa umeme, kwanza sii kweli kuwa umeme haukukatika kabisa enzi za Kalemani.

Pili JM amelifafanua vizuri sana tuu!.
Kilichofanya umeme haukukatika katika enzi za Kalemani na sasa unakatika katika ni kitu kinachoitwa peak demand
Hii peak demand imeongezeka sasa kuliko enzi za Kalemani!.

P
 
Alikuwa hajalewa pombe? Maana huwa analewa mpaka analala kwenye meza za baa, wakati mwingine anabebwa mzegamzega kupelekwa nyumbani hajitambui
Haiwezekani, ubebwe mzegamzega halafu saa kumi na moja asubuhi uwe kazini!
 
Mbona walishasema kwanini mgao haukuwepo wakati wa mwendazake. According to Makamba
1. Serikali ya Magu ililazimisha viwanda vipunguze uzalishaji ili kupunguza demand
2. Hawakufanya maintenance

Kama ni ukweli au uongo wanajua wao
Duu hili likitokea hukai hata mwezi utasikia vilio kila kona.
 
Ila za ndani ni kuwa viwanda vingi viliumizwa kwa wakati huo maana viwanda hutumia umeme mwingi, vikikatiwa sio rahisi kupata kelele kama wananchi wakikatiwa
Hii ni uongo maana ukienda kwenye data zao utakuta umeme unaoitajika nchini ni MW 1500 wakati uzalishaji ni MW 1850! Ukataka viwandani kwanini?
 
Ulikuwa unakatika na Tanesco hawakudhubutu kusema ni mgao au nini. Ilikuwa kimya tu. WaTz wasaulifu sana.

Kelemani ndo alikuwa anasema connection ya umeme ni 27k kila sehemu Tz, wakati Tanesco wana taratibu tofauti kabisa, ilikuwa usumbufu sana kwa watu.
Kuhusu swali la 27000 ni sera tu! Maana ile ni huduma na lengo lilikuwa watu wengi waunganishiwe umeme then Tanesco ipate mapato yake kupitia ununuaji wa Luku!
 
Ni kweli kabisa kuwa kipindi Kalemani ni waziri huo umeme haukuwa shida? Haukuwahi kukatika?
Haukuwa unakatwa ieleweke umeme haukatiki ila unakatwa kusudi ili watu flani wanaufaike na upungufu au mgao wa umeme.

Toka huyu beloved son akae kwenye wizara umeme umekatwa mara nyingi kuliko kawaida.
 
Wamenunua generator ya MW 20, hawasemi kwa bei gani na kama ni mtumba au mpya. Inasemekana wananunua umeme toka generator la Beatrice Lema wa Aqua Company la MW 45 lililokuwa lipigwe mnada wa hadhara kwa sababu ya madeni huko Mtwara kwa Dangote. Hawasemi umeme huo wanaununua kwa bei gani na ni kwa nini wasingainunua moja kwa moja hiyo generator ya Lema. Lakini yote hayo na mengine mengi bado umeme unakatika. Wananchi wakilalamika Januari anawaita ni wapuuzi tu na kwamba kama hawampendi basi wakamuue!! Yaani dhihaka tupu, masikio yamezidi kichwa.
 
Gerald Hando...paid journalist...wanarudia zoezi lile lile yeye na Kipanya walivyofanya kazi maalum Kwa Dr Idrisa..haadi akatolewa...wakaingia watu wa Ngeleha zikapigwa bilioni 500...

Nchi hii usipoelewa operations za wajanja, unaweza kupotezwa
 
Gerald Hando...paid journalist...wanarudia zoezi lile lile yeye na Kipanya walivyofanya kazi maalum Kwa Dr Idrisa..haadi akatolewa...wakaingia watu wa Ngeleha zikapigwa bilioni 500...
Mmmh
 
Gerald Hando...paid journalist...wanarudia zoezi lile lile yeye na Kipanya walivyofanya kazi maalum Kwa Dr Idrisa..haadi akatolewa...wakaingia watu wa Ngeleha zikapigwa bilioni 500...
La si kweli mvua zimenyesha mito imefurika sasa huo uhaba wa maji kuendeshea mitambo umetokea wapi tena?

Kwa hili hamna utetezi, kutakuwa na uwalakini mkubwa sana kwenye uongozi wake!! Anastahili kuuliza nni mwenzake alikuwa anafanya umeme usikatike katika rate iliyopo kwa sasa!! Its too much bro, hata mjinga huwezi kumdanganya tena!!
 
Kalemani umeme ulikuwa unakatika kila siku....lakini mmeshaanza kubadili facts ili agenda yenu ifanye kazi
Kwa hili siyo kweli labda kama hukuwa unaishi Tanzania!! Penye ukweli usemwe!!
 
Back
Top Bottom