Gerald Hando amuuliza Januari, Dkt. Kalemani aliweza vipi umeme haukukatika?

Gerald Hando amuuliza Januari, Dkt. Kalemani aliweza vipi umeme haukukatika?

Alikuwa hajalewa pombe? Maana huwa analewa mpaka analala kwenye meza za baa, wakati mwingine anabebwa mzegamzega kupelekwa nyumbani hajitambui
Duh kumbe huyu ngiri ni chapii hivyo basi watakua wanamtafuna kama analewa hadi anazima
 
"It no longer matters what is true or false – what matters is who controls the discourse" - Yaun Peng

Welcome to 1984, Orwellian Ministry of Truth.
 
MTANGAZAJI MAHIRI nchini Tanzania, Gerald Hando amemuuliza Januari Makamba kwanini alipoingia kwenye Wizara hiyo umeme ukaanza kukatika hovyo kwanini asimuulize Kalemani aliwezaje.

"Januari Makamba tumuulize swali moja dogo sana Kalemani amekaa miaka 6 umeme haujakatika yeye ameingia tu umeme umeanza kufanya vurugu nini shida, kwanini asimuulize Kalemani alifanyaje?" amehoji Hando

"Si chama kimoja wale si wabunge wale, si Serikali moja wale kwanini asimuulize Kalemani alifanya nini, Januari Makamba amuulize Dk Kalemani ulifanyaje uliwezaje, tumekaa six years hapa hatujaona situation kama hii make wamesingizia maji sasa maji mafuriko mabomba yanapasuka" amehoji Hando.


View attachment 2462435
Hando hivi ni Nani haswaaa??!
 
Hakukuwa na mgao kipindi cha Magu kila mtu anajua huu ukweli kasoro wewe tu. Ila umeme kukatika kama nilivyosema awali ulikuwa unakatika.

Elewa nilichoongea...kila mwaka kuna mgao kipindi cha ukame...wakati wa Magu walikuwa hawatangazi mgao...wanatangaza kuna matengenezo...elewa hiko nilicho ongea ...na mgao haukuwa mkali kama wa mwaka huu...so unaweza sema wakati wa Magu hakukutangazwa mgao...lakini usiseme haukuwepo ulikuwepo...zipo hata threads humu watu wanauliza kuna mgao WA kiimya kimyaa wakati wa Magu...labda Chige akupe link
 
Gerald Hando...paid journalist...wanarudia zoezi lile lile yeye na Kipanya walivyofanya kazi maalum Kwa Dr Idrisa..haadi akatolewa...wakaingia watu wa Ngeleha zikapigwa bilioni 500...

Kwani kitu wanachohoji ni cha kweli au wanamsingizia?
 
Hajui huyu hasara zilizosababishwa katika kipindi cha uwaziri wa januari, watu wamefilisika biashara zao zimekufa wauza barafu, wauza bucha za samaki, nyama, watu wa saluni za kike na za kiume, watu wa stationary, wauza juice, maji, watu wa kuchomelea mageti na vyuma mbalimbali na shughuli zote zinazotegemea umeme alafu yeye anakuja na stori nyepesi eti kuna mtu yuko nyuma ya hando?
Tutajie wafanyabiashara 5 tu na biashara zao mahali zilipo na TIN no zao ambao wamefilisika ?

Huo uwongo na kutunga mambo ya hovyo vinawasaidia nini?
 
Back
Top Bottom