Gerald Hando hata Wewe?

Gerald Hando hata Wewe?

Mkuu, hao unaojibizana nao hawawezi kukuelewa hata mara moja. Yani mtu ukisoma kile ulichoandika vs kile wanachoandika unaona uwezo wa ufahamu wenu uko mbali kama mashariki na magharibi.
Na hili ndilo tatizo kubwa Mkuu wangu. Yani kuna vitu inapaswa vijibiwe tuelewe. Lakin mtu anakuambia eti tunaichukia DPW sababu ni waarabu (au waislam).

Au kama kuna mikataba mingine inayoonyesha vitu kama ukomo wa mkataba, mgawanyo wa mapato/faida, vipengele vya kuvunja mkataba basi tuambiwe pia.

Maana yake inawezekana tukawa tunapinga kumbe kilichoonekana ni makubaliano tu lakini vipengele vinavyopigiwa kelele viko kwenye mkataba mwengine.

Sio mtu unasoma Mkataba unakuta umeandikwa eti sijui MAKUBALIANO YATAKUA HAI MPAKA PALE AMBAPO SHUGHULI ZA MIRADI ZITASITISHWA, lini? Haijulikani
 
Hoja kuu zinazohitaji majibu ni hizi hapa

1.) Tofauti ya ‘Makubaliano’ na ‘Mkataba’ ni ipi hasa kiasi mseme ule sio mkataba, kwamba ni makubaliano tu ya awali, na je Mkataba huo (makubaliano hayo) ni wa miaka mingapi? (UKOMO)

2.) Ni kwa faida ya nani kwamba DPW anapewa haki ya bandari zote za Tanganyika, kwamba hakuna mwekezaji mwingine yeyote anaweza kuja kufanya uwekezaji kwenye bandari za Tanganyika bila udalali wa DPW, je, ukiritimba huu ni kwa faida ya nani?

3.) Ni kwa faida ya nani, DPW apewe haki ya kudai kipande chochote cha ardhi yenye ukubwa wowote anaoutaka yeye ndani ya ‘Territory’ ya Tanganyika na sisi tumpe ardhi hiyo kwa kuondoa watu na miradi yote ndani ya eneo alilolitaka, na tumpatie bire kabisa kwa gharama zetu sisi, hata fidia tulipe sisi ili kuondoa watu kumpisha, huu uwendawazimu ni kwa faida ya nani?

4.) Ni kwa faida ya nani, kwamba sisi tuliowekeza matrillion ya mikopo kuendeleza bandari na tukiwa kama wamiliki wa rasimali ya bandari, tupate 0% ya faida itakayotokana na uendeshaji wa huduma za kibandari, yaani ni kana kwamba yeye kawekeza 100% na hivyo achukue 100%? Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

5.) Ni kwa faida ya nani, kwamba mkataba unahusisha bandari za Tanganyika tu na sio za Zanzibar, ilihali bandari ni suala la Muungano? Je, Zanzibar haitaki kunufaika au yenyewe haitaki matunda ya mkataba huu? Ukizingatia walioongia huu mkataba wote ni waZanzibari, kuanzia Samiah Suluhu Hassan, Makame Mbarawah, Hamza Johari na wenzao, kwamba hawataki Zanzibar yao ipate matunda mazuri ya mkataba huu?!

6.) Ni kwa faida ya nani kusema kwamba, hata DPW akavunja mkataba na kukiuka kanuni na taratibu zote zinazotambulika kimataifa, bado hatutaweza kuvunja , kuusema vibaya au kujitoa kwenye mkataba, milele! Uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?

7.) Ni kwa faida ya nani kwamba pamoja na kuwa DPW watachukua 100% ya faida, bado tena faida hiyo watapewa Msamaha wa kodi kwa 100%, yaani hata hicho wanachovuna nacho hatuchukui kodi, na wakti huo huo tunakamuliwa kodi za miamala, uwendawazimu huu ni kwa faida ya nani?
Hoja km hv tulizitegemea si kwa hando tu hata kwa waandishi nguli wa magazeti
 
Kila Nikiwaza kuandika huu uzi nilikua najishauri sana, mwishowe nimeona tu bora niandike ili dukuduku langu liishe.

Hivi karibuni watangazaji wakituo cha Wasafi FM Gerald Handom Maulid Kitenge na Zembwela walienda mpaka ziliko ofisi za DP Word kwenda kudanya mahojiano na wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo juu ya utendaji wao katika masuala mbalimbali ya bandari.

Kwangu ziara hiyo haikua na maana sana sababu kinachopingwa na watanzania wengi sio utendaji wa hao jamaa, hakuna anaepinga kua jamaa wako vizuri. Ila kinachopingwa ni aina ya mkataba. Sasa katika watangazaji hawa ningeweza kuelewa kama Maulid Kitenge na Zembwela wakifanya ushabiki wa haya masuala sababu upeo wao wa kuchambua mambo kama haya sio mkubwa kama Gerald.

Maulid Kitenge hua anaropokaga tu anadhani akiongea kwa sauti na ushabiki mkubwa ndio watu wataelewa. Sio mjenga hoja kwenye issues nyeti za msingi. Zembwela anaweza kua anajua kujenga hoja lakin maranzingio huonekana kwenye vipindi ambavyo sio serious sana hivyo uwezo wake unaweza ukawa unafichwa na hilo.

Lakin Gerald Hando wewe toka ukiwa Clouds FM msimamo wako ulikua ni wa kutetea wanyonge. Wewe ulikua hutetereki kuongea ukweli. Ulikua huogopi kabisa na kipindi hicho uko clouds ulikua hot kweli kaka. Kipindi chako cha Power Breakfast kilikua ho sana kwenye ile segment ambayo ulikua ukizungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu jamii. Umejadili mengi sana na kwa weledi sana kwenye hicho kipindi cha PB. Nadhan hata leo hii kama bado ungekua pale ungepinga hili.

Hata ulipoingia EFM bado ulikua hujaacha kuongelea mambo mbalimbali yanazohusu jamii. Nakumbuka ulisimamishwa hata EFM sababu ulikua ukitetea juu ya nchi kukopa kulikopitiliza. EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi.

Sasa Gerald Hando wa sasa umekuaje? NIni kimekubadilisha msimamo? Ni wewe kweli unaungana na Mtu roporopo kama Maulid Kitenge kutetea kitu ambacho unajua sio sahihi? Najua mtakua mmelipwa ili mtetee ulaji lakini roho yako kweli haikusuti kwa usaliti unaoufanya? Au kuna mahali umebanwa kifedha ukaona ufate msemo wa "mtumikie kafiri upate utajiri"??

Ukweli sijaamini na sintoamini kama kweli eti wewe Gerald Hando unaamini kua ule mkataba wa DP World na Serikali hauna dosari yoyote ile,
Masikini hana kiapo
 
Mmhhhh,
Nilikua sijaona hii Mkuu. Kwamba mapato yote anachukua yeye? Sidhan kama hili ni kweli sababu mojawapo y sababu ya kuipigia chapuo hii kampuni ni kwamba mapato atakayotupatia yataweza ku finance budget yetu Kwa zaidi ya 40%, sasa ingekua anayachukua yote yey wasingesema hivi.
 
Kuna watu hawajawahi kufika hata bandarini na kujionea Rushwa inavyopigwa pale, tunahitaji mwekezaji ili kutengeneza mapato yatakayo leta faida kwa watanzania wote, wapo watanzania wenzetu pale TPA lkn wanakunyanyasa utafikir wewe sio binadamu, wamejenga majumba ya kifahari kwa pesa za Rushwa ya bandari, Kuna mfanyakazi mmoja Enzi za Magufuli alikutwa na pesa trion 3 za kitanzania mfanyakazi tu wa kawaida, kwangu mimi Naona tunahitaji mwekezaji lkn kwa upande wa serikali waweke mkataba wenye ukomo basi
 
Hicho cha kuongeza mapato kipo kwenye makubaliano/mkataba?
 
Mmhhhh,
Nilikua sijaona hii Mkuu. Kwamba mapato yote anachukua yeye? Sidhan kama hili ni kweli sababu mojawapo y sababu ya kuipigia chapuo hii kampuni ni kwamba mapato atakayotupatia yataweza ku finance budget yetu Kwa zaidi ya 40%, sasa ingekua anayachukua yote yey wasingesema hivi.
Mapato wanayozungumzia ni kupitia kudhibiti magendo katika ulipaji kodi, na sio ile faida ya shughuli za huduma za kibandari..
 
Kuna watu hawajawahi kufika hata bandarini na kujionea Rushwa inavyopigwa pale, tunahitaji mwekezaji ili kutengeneza mapato yatakayo leta faida kwa watanzania wote, wapo watanzania wenzetu pale TPA lkn wanakunyanyasa utafikir wewe sio binadamu, wamejenga majumba ya kifahari kwa pesa za Rushwa ya bandari, Kuna mfanyakazi mmoja Enzi za Magufuli alikutwa na pesa trion 3 za kitanzania mfanyakazi tu wa kawaida, kwangu mimi Naona tunahitaji mwekezaji lkn kwa upande wa serikali waweke mkataba wenye ukomo basi
Kama tumeshindwa kupambana na rushwa za watu wa ndani, je kukitokea rushwa za watu wa nje tutaweza kupambana nayo?
 
Kila Nikiwaza kuandika huu uzi nilikua najishauri sana, mwishowe nimeona tu bora niandike ili dukuduku langu liishe.

Hivi karibuni watangazaji wakituo cha Wasafi FM Gerald Handom Maulid Kitenge na Zembwela walienda mpaka ziliko ofisi za DP Word kwenda kudanya mahojiano na wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo juu ya utendaji wao katika masuala mbalimbali ya bandari.

Kwangu ziara hiyo haikua na maana sana sababu kinachopingwa na watanzania wengi sio utendaji wa hao jamaa, hakuna anaepinga kua jamaa wako vizuri. Ila kinachopingwa ni aina ya mkataba. Sasa katika watangazaji hawa ningeweza kuelewa kama Maulid Kitenge na Zembwela wakifanya ushabiki wa haya masuala sababu upeo wao wa kuchambua mambo kama haya sio mkubwa kama Gerald.

Maulid Kitenge hua anaropokaga tu anadhani akiongea kwa sauti na ushabiki mkubwa ndio watu wataelewa. Sio mjenga hoja kwenye issues nyeti za msingi. Zembwela anaweza kua anajua kujenga hoja lakin maranzingio huonekana kwenye vipindi ambavyo sio serious sana hivyo uwezo wake unaweza ukawa unafichwa na hilo.

Lakin Gerald Hando wewe toka ukiwa Clouds FM msimamo wako ulikua ni wa kutetea wanyonge. Wewe ulikua hutetereki kuongea ukweli. Ulikua huogopi kabisa na kipindi hicho uko clouds ulikua hot kweli kaka. Kipindi chako cha Power Breakfast kilikua ho sana kwenye ile segment ambayo ulikua ukizungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu jamii. Umejadili mengi sana na kwa weledi sana kwenye hicho kipindi cha PB. Nadhan hata leo hii kama bado ungekua pale ungepinga hili.

Hata ulipoingia EFM bado ulikua hujaacha kuongelea mambo mbalimbali yanazohusu jamii. Nakumbuka ulisimamishwa hata EFM sababu ulikua ukitetea juu ya nchi kukopa kulikopitiliza. EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi.

Sasa Gerald Hando wa sasa umekuaje? NIni kimekubadilisha msimamo? Ni wewe kweli unaungana na Mtu roporopo kama Maulid Kitenge kutetea kitu ambacho unajua sio sahihi? Najua mtakua mmelipwa ili mtetee ulaji lakini roho yako kweli haikusuti kwa usaliti unaoufanya? Au kuna mahali umebanwa kifedha ukaona ufate msemo wa "mtumikie kafiri upate utajiri"??

Ukweli sijaamini na sintoamini kama kweli eti wewe Gerald Hando unaamini kua ule mkataba wa DP World na Serikali hauna dosari yoyote ile,
NJAAAAAAAAAAAAA
 
Nafikiri tukubali kuwa majira yanabadilika jameni, hata dunia yenyewe huzunguka! Hahaa
 
Serikali ya awamu ya 6 inakwenda kuukata huo mzizi wa fitina
emoji120.png
Nafikiri mleta mada na wengine hatujakataa kuwa kuna dosari kubwa bandarini, ila tu makubaliano ya kisheria yasiegemee upande moja.
 
Kila Nikiwaza kuandika huu uzi nilikuwa najishauri sana, mwishowe nimeona tu bora niandike ili dukuduku langu liishe.

Hivi karibuni watangazaji wakituo cha Wasafi FM Gerald Handom Maulid Kitenge na Zembwela walienda mpaka ziliko ofisi za DP Word kwenda kudanya mahojiano na wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo juu ya utendaji wao katika masuala mbalimbali ya bandari.

Kwangu ziara hiyo haikua na maana sana sababu kinachopingwa na watanzania wengi sio utendaji wa hao jamaa, hakuna anaepinga kua jamaa wako vizuri. Ila kinachopingwa ni aina ya mkataba. Sasa katika watangazaji hawa ningeweza kuelewa kama Maulid Kitenge na Zembwela wakifanya ushabiki wa haya masuala sababu upeo wao wa kuchambua mambo kama haya sio mkubwa kama Gerald.

Maulid Kitenge hua anaropokaga tu anadhani akiongea kwa sauti na ushabiki mkubwa ndio watu wataelewa. Sio mjenga hoja kwenye issues nyeti za msingi. Zembwela anaweza kua anajua kujenga hoja lakin maranzingio huonekana kwenye vipindi ambavyo sio serious sana hivyo uwezo wake unaweza ukawa unafichwa na hilo.

Lakin Gerald Hando wewe toka ukiwa Clouds FM msimamo wako ulikua ni wa kutetea wanyonge. Wewe ulikua hutetereki kuongea ukweli. Ulikua huogopi kabisa na kipindi hicho uko clouds ulikua hot kweli kaka. Kipindi chako cha Power Breakfast kilikua ho sana kwenye ile segment ambayo ulikua ukizungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu jamii. Umejadili mengi sana na kwa weledi sana kwenye hicho kipindi cha PB. Nadhan hata leo hii kama bado ungekua pale ungepinga hili.

Hata ulipoingia EFM bado ulikua hujaacha kuongelea mambo mbalimbali yanazohusu jamii. Nakumbuka ulisimamishwa hata EFM sababu ulikua ukitetea juu ya nchi kukopa kulikopitiliza. EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi.

Sasa Gerald Hando wa sasa umekuaje? NIni kimekubadilisha msimamo? Ni wewe kweli unaungana na Mtu roporopo kama Maulid Kitenge kutetea kitu ambacho unajua sio sahihi? Najua mtakua mmelipwa ili mtetee ulaji lakini roho yako kweli haikusuti kwa usaliti unaoufanya? Au kuna mahali umebanwa kifedha ukaona ufate msemo wa "mtumikie kafiri upate utajiri"??

Ukweli sijaamini na sintoamini kama kweli eti wewe Gerald Hando unaamini kua ule mkataba wa DP World na Serikali hauna dosari yoyote ile,
Unataka Gerald Hando afanye utakavyo yakimtokea ya Azory Gwanda au Christopher Mtikila utakuwa tayari kuipa Matunzo Familia yake?

Na kwa Kukusaidia tu baada ya Kukichafua kule EFM na Kupigwa chini kwa Amri kutoka Chalinze na Magogoni alipokea Simu asizozijua huku akipigwa Biti na sasa anafuatiliwa na anaowajua na asiowajua ili akirudia tu Ukipendacho Wewe na Unachokililia hapa wenye Kazi yao Maalum wamalize Shughuli na awe Historia Kwenu na Tanzania.

Acheni kumponza Mwenzenu yamkute.
 
Awatete wakati hamjitetei? Hando pigania ugali wa wanako kiongozi. Hakuna hata mmoja utakuletea mchele, unga sembe,mchichi.
 
Mkuu kuna ufanisi gani pale bandari ya malindi?
Bandari ya Zanzibar tumeona ufanisinwa Mwekezaji mpaka Sasa. Ni zamu yenu huko Tanganyika
Mfano huu, kuna meli ina week ya tatu pale inapakua makontena, hili ndilo tatizo kubwa kwenye ufanisi unaopigiwa kelele sana.
 
Ni neema tupu....

Mkataba wetu na DPW unakwenda kuuondoa urasimu na "status quo" iliyoko bandarini.... haiwezekani bandari za nchi jirani ,Lamu na Mombasa ziwe na ubora wa kupakia na kupakua mizigo ndani ya siku 3 ,zetu ziwachukulie wafanyabiashara siku 7 ,siku 14 hadi mwezi na nusu....AIBU HII ...

Tunapoteza mapato kiasi gani....

Tunawaumiza wafanyabiashara kiasi gani....

Turidhie kukimbiwa na wafanyabiashara wa hizi nchi 8 zinazotuzunguka?!!!

Serikali ya awamu ya 6 inakwenda kuukata huo mzizi wa fitina[emoji120]

Kongole kwake mh.Rais SSH[emoji120]

#SiempreJMT[emoji120]
Huyo unaemmwagia sifa ameshindwa vipi kuondoa urasimu, na kuweka mifumo thabiti ya kudhibiti upigaji na rushwa ili bandari yetu itunufaishe, na kwamba wageni ndio watakuja wakuboreshee bandari yako na kukuchumia faida bwerere, kwa mikataba ipi? Yuko wapi mwenye uwezo wa kushinikiza mikataba yenye win-win situation? Nchi imejaa majuha wengi kweli hii..!
 
Kila Nikiwaza kuandika huu uzi nilikuwa najishauri sana, mwishowe nimeona tu bora niandike ili dukuduku langu liishe.

Hivi karibuni watangazaji wakituo cha Wasafi FM Gerald Handom Maulid Kitenge na Zembwela walienda mpaka ziliko ofisi za DP Word kwenda kudanya mahojiano na wafanyakazi mbalimbali wa kampuni hiyo juu ya utendaji wao katika masuala mbalimbali ya bandari.

Kwangu ziara hiyo haikua na maana sana sababu kinachopingwa na watanzania wengi sio utendaji wa hao jamaa, hakuna anaepinga kua jamaa wako vizuri. Ila kinachopingwa ni aina ya mkataba. Sasa katika watangazaji hawa ningeweza kuelewa kama Maulid Kitenge na Zembwela wakifanya ushabiki wa haya masuala sababu upeo wao wa kuchambua mambo kama haya sio mkubwa kama Gerald.

Maulid Kitenge hua anaropokaga tu anadhani akiongea kwa sauti na ushabiki mkubwa ndio watu wataelewa. Sio mjenga hoja kwenye issues nyeti za msingi. Zembwela anaweza kua anajua kujenga hoja lakin maranzingio huonekana kwenye vipindi ambavyo sio serious sana hivyo uwezo wake unaweza ukawa unafichwa na hilo.

Lakin Gerald Hando wewe toka ukiwa Clouds FM msimamo wako ulikua ni wa kutetea wanyonge. Wewe ulikua hutetereki kuongea ukweli. Ulikua huogopi kabisa na kipindi hicho uko clouds ulikua hot kweli kaka. Kipindi chako cha Power Breakfast kilikua ho sana kwenye ile segment ambayo ulikua ukizungumzia mambo mbalimbali yanayoihusu jamii. Umejadili mengi sana na kwa weledi sana kwenye hicho kipindi cha PB. Nadhan hata leo hii kama bado ungekua pale ungepinga hili.

Hata ulipoingia EFM bado ulikua hujaacha kuongelea mambo mbalimbali yanazohusu jamii. Nakumbuka ulisimamishwa hata EFM sababu ulikua ukitetea juu ya nchi kukopa kulikopitiliza. EFM yatangaza kumchukulia hatua Hando, yadai maoni yake kuhusu Serikali kukopa si msimamo wa taasisi.

Sasa Gerald Hando wa sasa umekuaje? NIni kimekubadilisha msimamo? Ni wewe kweli unaungana na Mtu roporopo kama Maulid Kitenge kutetea kitu ambacho unajua sio sahihi? Najua mtakua mmelipwa ili mtetee ulaji lakini roho yako kweli haikusuti kwa usaliti unaoufanya? Au kuna mahali umebanwa kifedha ukaona ufate msemo wa "mtumikie kafiri upate utajiri"??

Ukweli sijaamini na sintoamini kama kweli eti wewe Gerald Hando unaamini kua ule mkataba wa DP World na Serikali hauna dosari yoyote ile,
Njaa mbaya, Esau aliuza ulaziwa wake wa kwanza kwa sababu ya njaa.
 
Back
Top Bottom