Gerald Hando: Mbowe aachie ngazi, amekaa sana CHADEMA

Malengo ya Wazanzibar NI kuchukuwa Dola ya Zanzibar hawana mpango na Tanganyika wala hakuna fund wataleta Tanganyika.

Zitto NI mwanasiasa opportunist tayari amehakikishiwa ubunge kwahiyo akili yake na nguvu zake NI Kigoma, hataki madaraka yatakayomlazimu kuzunguka nchi nazima wakati Chama chenyewe kipo Zanzibar na Kigoma tu.
 
Ccm wamemlipa sh. ngapi kwenye hii project?
Ccm wamemlipa sh. ngapi kwenye hii project?
 
Maalim Seif alinunua ACT Wazalendo kwa ajili ya Ukombozi wa Zanzibar

Usisahau hilo
 
Na uzuri ni mlevi mwenzetu wa bia, sasa hivi tunakula bia mpaka kwenye maandamano.
Bia, konyagi, hivi ni viburudisho tu, alimradi kazi ifanyike, watanzania wanahitaji demokrasia safi, "Huwezi kuwa mpenda haki na ukalichukia neno demokrasia ukiona una lichukia tu ujue haupo sahihi, demokrasia huanzia maungoni, na si neno la kutamka bila vitendo, kama afanyavyo Bw. Mbowe, anaitamka, lakini ndani mwake haipo""
 
"Mbowe aachie ngazi amekaa sana Chadema"

Nimeitazama hiyo kauli nimeiona imekaa kidikteta, na sio hiyo kauli ya Hando pekee, wote wanaomtaka Mbowe aachie ngazi nao wamekaa kidikteta hurudia kauli hiyo hiyo wakijidai kutaka demokrasia ifuatwe, hii demokrasia yao ni ya ajabu sana.

Hawa viumbe wanajiona wao ndio wapo juu ya maamuzi ya wengine, hawajui demokrasia inasema wengi wape wachache wasikilizwe, sasa kama wengi wameamua kumpa Mbowe, hawa viumbe wengine wachache kwanini wanateseka?!

Halafu wanaposhangaza zaidi, wanamtaka Mbowe afuate mfano wa Zitto, ni kama vile wanataka kulazimisha Zitto aondoke na Mbowe, sijui wanataka iwe hivyo kwa lengo gani..

Hawajui hata huyo Zitto wanaemuona ameondoka uongozini ACT, anaenda kuwa "mshauri mkuu wa chama" chake kulingana na Katiba yao, hawajui huyu ni sawa na ametoka kwa mlango wa mbele, lakini anarudi ndani kwa mlango wa nyuma, sijui huu ujinga ndio wanataka Mbowe nae aufuate?!.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Ukweli mchungu huu
 
Mhh!
 
Na mafanikio pekee ya Zitto kwenye ACT ni kuachia madaraka.
Wewe chama kinafanya kazi Pemba, Tunduru, Kigoma na Magomeni kuna haja gani ya kukaa muda mrefu ?
Chaggadema inafanya kazi zaidi ya kanda ya kaskazini?
 
Wajumbe wa Kamati Kuu ya Chadema ndio wenye maamuzi ya mwisho juu ya Mbowe ikiwa kama atagombea uenyekiti wa chama chao, wakiamua kumpa watampa, wakiona hafai watamnyima, wale ni watu wazima wenye akili zao na maamuzi yao, hizi kelele nyingine nje ya hao wenye maamuzi yao ni sawa na za walevi bar.

Sent from my SM-G900H using JamiiForums mobile app
 
Hivi kati ya mbowe ,pr lipumba na cheyo nani kakaa sana kwenye uwenyekiti?
 
Hando ni mtangazaji kwa hali hiyo habari zake zitaegemea upande mmoja na zitakuwa hasi kwa Chadema. Vipi na yeye bosi wake ameshikilia kiti kwa miaka mingapi? Aanze naye aondoke.
 
huyu ni nani na anafafanya nini? ana elimu gani? huwezi ku- argue technical issues na na std seven failure.
 
Akili kubwa sana hii, angeanzia kwa CCM itoke madarakani "imekaa sana zaidi ya miaka 60"
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…