Gerald Hando: Mbowe aachie ngazi, amekaa sana CHADEMA

Gerald Hando: Mbowe aachie ngazi, amekaa sana CHADEMA

Mkapa = Mbowe
JK = Mbowe
JPM = Mbowe
Samia = Mbowe

Bob Makani alirithi chama kwa Edwin Mtei, Makani kaoa dada wa Mtei(SHEMEJI). Freeman Mbowe karithi kwa Makani, Mbowe kaoa mtoto wa Mtei (mkwe).

Hicho ni chama cha FAMILIA, mkitaka Mbowe atoke anzisheni chama chenu
Kwa hiyo Mbowe muda wote amekuwa Rais sawa na hao uliowataja? Mandera alikaa jela na aliendelea kuwa kiongozi wa ANC, Nyerere aliongoza Taa na ikabadilika kuwa Tanu na bàadaye ccm huko hamshangai. Ccm ipo madarakani miaka 60 Toka uhuru linganisha na Singapore iliyopata uhuru 1965 mahali ilipo leo na wewe kikongwe. Unajiskia kumchoka Mbowe kuwa kiongozi wa Chadema ila unainjoi kukaa na ccm!!
Rais Samia amesema ataanza kusikiliza kero za mtu mmoja mmoja, mnashangilia, badala ya kushangaa kurudi nyuma miaka ya 1985 ambacho ndicho alichoanza Mzee Ruksa mpaka Nyerere, akamshtua nchi haiendeshwi hivyo.
Kwenye wasafi mtu akiongea angalau unaona logic ni Oscar tu, wengine labda muongelee mpira.
 

Gerald Hando akiwa katika kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM leo Machi 7, 2024 ametoa hoja ya kumtaka Mwenyekiti wa CHADEMA kuachia ngazi ya Uenyekiti wa chama hicho kwa kile alichodai amekaa sana, tazama video hapo juu.

Hoja hii inakuja siku chache baada ya kumshuhudia Zitto Kabwe akiachia nafasi ya Uongozi kwenye chama chake Cha ACT Wazalendo.

Upi mtazamo wako kuhusu hoja hii ya Hando?
Huyu ni mamluki wa ccm na hana nafasi CDM. Mbowe ndio kwanza CDM inazaliwa sasa na anahitajika kwa angalau miaka 10 ijayo.
 

Gerald Hando akiwa katika kipindi cha Good Morning cha Wasafi FM leo Machi 7, 2024 ametoa hoja ya kumtaka Mwenyekiti wa CHADEMA kuachia ngazi ya Uenyekiti wa chama hicho kwa kile alichodai amekaa sana, tazama video hapo juu.

Hoja hii inakuja siku chache baada ya kumshuhudia Zitto Kabwe akiachia nafasi ya Uongozi kwenye chama chake Cha ACT Wazalendo.

Upi mtazamo wako kuhusu hoja hii ya Hando?
Chama cha familia hicho🤣🤣🤣
 
CCM mna vichekesho Sana, sasa Zitto si anapewa ubunge Kigoma na wapemba wanachukuwa Chama chao?

Hivi unaamini Wapemba wanaoweza kuongozwa na Zitto?

Hujui kwamba ACT ni kimvuli cha CUF? Base ya ACT ni Zanzibar na lazima Chama kiwe chini ya Wazanzibar na ndicho kilichofanyika, huyo dada atakuwa kiongozi ceremonial tu kama Rais wa Ujerumani na Rais wa Israel, hapo wenye nguvu ni mwenyekiti na makamu wake Jusa.

Hayo ni maigizo ya kisiasa Zitto anarudishiwa Jimbo la Ujiji Kigoma.
Upo nje ya mada
 
Mbowe ana mapigo ya Mobutu sese seko kuku Ngbendu Wa za Banga

Kama tu kuachia kiti cha chama hataki siku akishika nchi si ndo imetoka hiyo
Huyu siku akiwa Rais tusahau hatoki hadi afe
 
Hizi radio ziache kutangaza na kusambaza habari au maoni binafsi ya watangazaji.Hili ni kosa kubwa na Chombo kinachosimamia habari kinatakiwa kiwachukulie hatua hii radio wasafi na watangazaji wake.Nahuyu Hando toka afiwe na mkewe naona ugonjwa wa afya ya akili umeongezeka
Mimi naona wewe ndio una tatizo
Maana yeye kaongea ukweli
 
Back
Top Bottom