Hii movement ya NRNE inakua kwa kasi kama moto wa nyikani, hawa vijana wa chuo hushawishiana nchi nzima kama nzige , muda si mrefu watachafua hali ya hewa, ni vizuri watawala sasa waliangalie hilo mapema na kupiga uturn ikibidi kubadili vifungu vichache kuua hii movement kabla ya watu kuingia road na kuvuruga amani.
Huu moto unaanza kuunguza nchi sasa, ni kitu cha kutilia maanani sana politically kuona kundi kubwa la watu walioungana wote kwa pamoja na kuzuia hotuba kwa kusema kitu kimoja tena kwa jazba, huu ni mfano wa Karl Marx anapoita "class struggle, a proletariat revolution" pale wale watu wa hali duni wasio na cha kupoteza wanaposimama pamoja kudai haki zao, huwa mwishowe wanashinda hata uwapige vipi.
Hii ya kuzomewa Mh Msigwa ni wake up call, watawala wafanye hiyo reform kinamna hata kifungu kimoja kuua so ili amani isipotee. Dalili za nchi kuharibika sasa ziko wazi, watawala wasipuuze huu moto ni mkali.
Hii clip ikifika kwa majirani tumekwisha lazima waruke nayo wiki nzima , dawa ni kuua kwa promo za derby 😜