Gerson Msigwa: Tuko mbioni kuanzisha Televisheni ya Serikali itakayorusha Habari za Maendeleo tu

Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema wizara ya habari iko mbioni kuanzisha Television ya serikali itayorusha mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali.

Television hiyo itakuwa tofauti kabisa na TBC kwani itarusha mambo ya msingi ya serikali amesema Msigwa.

Source: Clouds tv
Wakimaliza waanzishe Tv ya Rais SSH itakayokuwa inaonesha mambo ya Rais SSH tu
 
Hii nchi ni ngumu sana kuielewa!!yaani Tv ya taifa ipo na ndio mpiga debe mkuu wa serikali, kuna chaneli ten, mpiga debe wa chama, zote hizo hazitoshi?!!sasa kama ni hivyo kwanini wasiifanye TBC 2, ndio iwe na majukumu hayo?!!
Kuongeza ajira
 
huyu jamaa tangu aondolewe kule ikulu Dishi limeyumba sana naona hata afya inaanza kutetereka, vibaraka wa mwendazake hawa wamechanganyikiwa kabisaaa na bado mama samia anawakumbatia tu
 
Taifa ni nchi na watu wake

Serikali ni kikundi cha watawala!
Kwa hiyo TV ya Taifa TBC1 ni yetu sisi waTaifa (wananchi), na hiyo nyingine watakayoanzisha ya Serikali itakua ya "Watawala" !!!??

Sijui hiyo ya Watawala itakua inaonyesha nini kwetu wananchi!!?? Na bado itaendeshwa kwa kodi zetu wananchi? Au hii itatumia kodi zao watawala?
 
Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema wizara ya habari iko mbioni kuanzisha Television ya serikali itayorusha mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali.

Television hiyo itakuwa tofauti kabisa na TBC kwani itarusha mambo ya msingi ya serikali amesema Msigwa.

Chanzo: Clouds tv
Maendeleo yanaanzishiwa tv! Maendeleo si yanaonekana tu? Mtoto acha kupiga mayowe, acha watu waone wenyewe....
 
Kwa hiyo TV ya Taifa TBC1 ni yetu sisi waTaifa (wananchi), na hiyo nyingine watakayoanzisha ya Serikali itakua ya "Watawala" !!!??

Sijui hiyo ya Watawala itakua inaonyesha nini kwetu wananchi!!?? Na bado itaendeshwa kwa kodi zetu wananchi? Au hii itatumia kodi zao watawala?
Watawala wanatoza kodi hawalipi kodi!
 
Ila hii nchi, tuna viongozi wa ajabu sana.. hizi pesa si hata mgawe ajira kwa watu au atleast muwafute jasho waliounguliwa na biashara kariakoo?

Sent from my SM-J730F using JamiiForums mobile app
 
Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema wizara ya habari iko mbioni kuanzisha Television ya serikali itayorusha mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali.

Television hiyo itakuwa tofauti kabisa na TBC kwani itarusha mambo ya msingi ya serikali amesema Msigwa.

Chanzo: Clouds tv
Ianzishwe na channel ya kuonesha mapungufu ya serikali. Wananchi wana haki ya kujua mabaya na mazuri
 
Msemaji mkuu wa serikali Gerson Msigwa amesema wizara ya habari iko mbioni kuanzisha Television ya serikali itayorusha mambo ya maendeleo yanayofanywa na serikali.

Television hiyo itakuwa tofauti kabisa na TBC kwani itarusha mambo ya msingi ya serikali amesema Msigwa.

Chanzo: Clouds tv

Kabla ya kuanzisha hiyo television wangefanya hayo Maendeleo wanayotaka kurusha kwanza

Maana tuna tbc chanel10 na nyingine nyingi ambazo sasa zinatupigia tuu zinatupigia mara X SIJUI KAFANYAJE, SIJUI NYUMBA NDOGO😂😂😂😂

Au nasema uongo ndugu yangu johnthebaptist
 
Back
Top Bottom