mtwa mkulu
JF-Expert Member
- Sep 11, 2013
- 8,586
- 11,227
Okay katika 17 umejibu matano tena mawili hujapinga kama hilo la Riba yanabaki matatu.. unasema nimeongea uongo asilimia 80 hivi huko shule mnafunzwa ujinga? Ngoja nirudi kukujibu
1. LIBYA watu walikuwa wanalipia umeme kama kawaida kwa miaka yote
2. Libya ya dikteta Gaddafi ilikuwa ni nchi ya Kiislamu na kwenye Uislamu riba ni haramu.
3. Ni ujinga kufikiria au kuamini wazazi wake Gaddafi walikuwa wanaishi kwenye nyumba za kupanga yeye akiwa Rais
Pia Gaddafi alikuwa anapenda kuishi kwenye mahema ya kifahari, hata alipokuwa akienda nchi nyingine kama US alikuwa anaweka hema lake la Kifahari kwenye viwanja vya Trump
4. Kwa nini Kila mfanyakazi Mpya (Mwajiriwa mpya) nchini Libya alipewa Dola za kimarekani 50,000 ili aanzie maisha wakati mtu ukiajiriwa unalipwa mshahara??
5. Libya ilianza kuchimba mafuta kibiashara mwaka 1960 na miaka 9 tu baadaye Gaddafi akafanya mapinduzi, ulitegemea ndani ya miaka 8 ungeona faida zozote za uchumi wa mafuta uliokuwa unaanza kuchipuka??