Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Hapo ndo shida inaanza, BURE ALISHAKUFA. Vinaghalimiwa kwa %ngapi??
Hili sasa mweleweshe mtoa mada maana anachouliza ni kwamba ikiwa hizi hospitali za umma zinaendeshwa kwa kodi za wananchi iweje gharama za matibabu ziwe juu namna hiyo hata kuzidi hospitali binafsi?
 
Mnang'ang'ana kuokolewa na tawi kavu. Hakuna serikali itacover vist 100%. TUFANYE KAZI
 
Hili sasa mweleweshe mtoa mada maana anachouliza ni kwamba ikiwa hizi hospitali za umma zinaendeshwa kwa kodi za wananchi iweje gharama za matibabu ziwe juu namna hiyo hata kuzidi hospitali binafsi?
Binafsi ipi?? Ataje moja alinganishe.
 
Swala liko palepale gharama zipo juu sana, hii ndiyo hoja ya msingi na wengi wameshatoa shuhuda zao humu......
Juu what is the reference??
Unaanzia wapi? Hiyo tofauti huioni?
 
Unataka kutuaminisha reagent tunatengeneza ?
 
Juu what is the reference??
Unaanzia wapi? Hiyo tofauti huioni?
At least sasa umeanza kuelewa, kwa hiyo nendeni mkafanye review ya hizo gharama ziendane na dhana ya cost sharing siyo kuwa kichaka cha kuendelea kuwakamua watanzania maskini kwenye huduma ambayo tayari inaendeshwa kwa kodi zao wenyewe.​
 
Swala liko palepale gharama zipo juu sana, hii ndiyo hoja ya msingi na wengi wameshatoa shuhuda zao humu......
Nimetoa swali
Gharama zipo juu ukilinganisha na wapi ?
Nimewapa option ya kutaja nchi 10 afya ni Bure na nikawapa option ya surgery kubwa kama 10 Tanzania zipo juu kuliko nchi unayolinganisha

Taja ..
 
At least sasa umeanza kuelewa, kwa hiyo nendeni mkafanye review ya hizo gharama ziendane na dhana ya cost sharing siyo kuwa kichaka cha kuendelea kuwakamua watanzania maskini kwenye huduma ambayo tayari inaendeshwa kwa kodi zao wenyewe.​
Kipimo 750,000/= umeambiwa lipa 250,000/= hata hujaona sharing??

Mambo yanalipwa2/3 to 3/4?

Tufanye kazi tuache kupoteza muda.
 
Kama hutengenezi hiyo ina justify vipi bei kuwa kubwa, ni vitu vingapi hatutengenezi nchi hii!?
Sasa sema ni reagent gani tunanunua kwa bei ndogo na tunauza kwa bei kubwa
 
Nimetoa swali
Gharama zipo juu ukilinganisha na wapi ?
Nimewapa option ya kutaja nchi 10 afya ni Bure na nikawapa option ya surgery kubwa kama 10 Tanzania zipo juu kuliko nchi unayolinganisha

Taja ..
Mwenzio keshanielewa tayari wewe hapa unarudia yaleyale, nendeni mkafanye review ya hizo bei ziendane na dhana ya cost sharing.
 
Unaelewa unachosoma:
Hiyo ni bei as per MSD 2015
Umeona gharama za consumables au unarukaruka tu.

Gharama za consumables bila ya itemization ni mbuzi mwingine aliyenona kwenye gunia.

Independent audit ya watu wenye heshima zao kina CAG Assad ilikuwa muhimu na kwa dharura sana.

"Pana Pandora boxes nyingi za kufunguliwa hapa."
Kwamba average cost $176 per session.

1. Hiyo ikiwa staff list hewa yote Ile iko ndani.
2. Hakuna itemization yoyote ya consumables wala bei zake.
3. Hakuna reference yoyote lolote ya kodi zetu kwenye lolote.

Zingatia list hii ya staff hewa:

1. Manesi 20
2. Nephrologists 4
3. Registrars 8
4. Nutritionist 1
5 Biomedical engineers 2
6. Health attendants 4

Kwa kila machine 9.

Kwa hakika tumepigwa!
 
Gharama za matibabu ni kubwa sana, na hii inaweza kutokana na upungufu wa bajeti unaoelekezwa kwenye mahospitali husika; na kupelekea wagonjwa kubebeshwa gharama kubwa katika matibabu.

Mfano:-
  • Vyuo vya umma, viwe vikuu au vya kati, hulipwa mishahara na serikali, ingawa vyuo hivyo vinakusanya ada za mamilioni ambazo hutumika kama gharama za uendeshaji wa vyuo hivyo pamoja na posho mbali mbali.​
  • Tukija upande wa hospitali; serikali inawalipa mishahara, pamoja na kusambaza dawa; sijajua kama dawa hizo au kemikali hizo au vitendea kazi hivyo vinatosheleza uhitaji; na kama havitoshelezi; ni nani anatakiwa anunue; hospitali au serikali?​
  • Inawezekana gharama (ada) kuwa kubwa hospitalini ikiwa lengo ni kufidia gharama za uendeshaji au kulipana posho kutokana na ufinyu wa bajeti waliopelekewa.​
  • Kupata jibu sahihi, itatulazimu kujua; serikali inafanya majukumu gani kwa hospitali (inagharamia nini), na hospitali ina majukumu yapi katika uendeshaji. Au mapato ya hospitali yanatumika kwenye nini?​
 
At least sasa umeanza kuelewa, kwa hiyo nendeni mkafanye review ya hizo gharama ziendane na dhana ya cost sharing siyo kuwa kichaka cha kuendelea kuwakamua watanzania maskini kwenye huduma ambayo tayari inaendeshwa kwa kodi zao wenyewe.​
Watanzania wasio na ndugu ni wachache Sana na serekali inatumia Kodi kuwasaidia

Kodi haiwezi kukukipia wewe na maitaji Yako binafsi

Kodi inalipa huduma za umma

Acheni ujinga kutaka sisi tuwalipie huduma binafsi (afya ) fanyeni kazi tibuni ndugu zenu na familia zenu
 
Unaonaje badala ya kujihoji hivi kukafanyika independent audit Ili masuala mazima ya bei yakawekwa wazi?

Tungependelea bei iwe actual reflection ya gharama za consumables.

Au waona je mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…