Gharama kufuru za matibabu hospitali za umma ni kwa uhalali upi?

Bei hizo hutokana na matibabu makubwa ya kibingwa ambayo gharama na teknolojia yake ni kubwa saana ,tena kwa hizi hospital za umma gharama hizo ni nafuu saana ililinganishwa na hospitali za binafsi au nje ya nchi ,ili kuweza kuendesha huduma hizo kwa wananchi kwa wakati wote Mwananchi anapaswa kuchangia gharama kidogo ,suluhu ya kudumu ya jambo hili ndio huu mpango wa Bima ya Afya kwa wote ambayo itamhakikishia Mwananchi wa hali yeyote kupata huduma za matibabu makubwa na madogo kwa nyakati zote ,BIMA YA AFYA KWA WOTE ITATUONDOLEA ADHA HIZI KWA KUTUHAKIKISHIA HUDUMA BORA KWA NYAKATI ZOTEEE ,bima ni muhimu saana .
 
Ndio mana kuna ishu ya bima ya Afya ambayo malipo yake ni kidogo lakini ita cover haya mambo yote, leo mtu anapinga 340,000 km malipo ya bima ya Afya Kisha akipewa gharama halisi qnalalaika inakuwaje? Tujifunze
 
wanapanga bei kwa watu binafsi sio vya kwao...tunatakiwa kufanya kama watanzania ni kuiondoa ccm madarakani, ccm ina nguvu sana sasa ,wanafanya chochote kile hakuna wakuwafanya chochote, wenyewe wanasema hata hili litapita.....we unafikili pesa za uchaguzi wanatoa wapi?
 
Tunajua kuwa amekaa hospitali kwa kipindi gani? Zimetumika gharama kiasi gani za ununuzi wa dawa na baadhi ya matibabu yamekwendaje? Yawezekana kwa kiasi hicho cha pesa angekwendq India ingekuwa zaidi ya milioni hamsini huko, lazima tulinganishe huduma na gharama za matibabu mana serikali ikiboresha huduma gharama nazo lazima ziongezeke hata kwa kiasi fulani
 
Huduma siyo anasa. Hospitali inalipa umeme, maji, wataalamu ,matengenezo ,madawa na uchunguzi na vitu vingine vingi . Ni muhimu sana kuchangia matibabu ili kuwa na uhakika wa uendeleevu wa utoaji huduma katika vituo vyetu vya afya. Hili linawezekana tu pale kila mtu atakapokuwa na bima. Nguvu yetu iende huko ,tusipolipa kesho tutashindwa kutoa huduma kwa watanzania wengine .Bima inaweza onekana haina umuhimu ila ukikata bima inaweza kuokoa mamilioni ya fedha ,UGONJWA HAUPIGI HODI
 
Tupunguze Double standard tunapojadili mambo yenye maslahi kwa umma. Hospitali hazijiendeshi for free hivyo hizi charges zinazowekwa ambazo hata sio nyingi ni kwa ajili ya kugharamia mambo muhimu ili huduma zipatikane kiurahisi
 

Kwamba ni gharama za kibingwa? Hii si ni Ile ya Bashe na wakulima?

Hizi gharama za kibingwa zinafikiwa je? Majengo ya umma? Vifaa vya umma? Mabingwa wanesomeshwa na umma? Wanalipwa na umma? Nk nk.

Kwamba kama vipi Kila mtu akawe bingwa?

Kwa bei hIzi hakuna mfuko wa bima au mtu utaweza kumudu.

Si waseme tu kama nia yao ni pesa kama vipi watu tufanye maamuzi magumu?

Ninakazia:

Tunakoelekea siyo kwenyewe.
 
Kuiondoa ccm madarakani sio solution. Solution hapa ni Mfumo wa Bima ya Afya kwa wote ambao utakua mfumo rfiki wa kuhakikisha Matibabu kwa wote yanakua sawa
 
Basi na serikali iache kutenga bajeti kwa wizara ya afya!
Ikiacha kutenga Bajeti Wananchi mtaweza kuchagia ili kulipa mishahara ya Madaktari na wahudumu wa afya? na kununua Vifaa Tiba? pamoja na kujenga Majengo ya kutolea Huduma?
 
Hayupo anayekataa cost sharing ila break down ya gharama ni vyema vikajulikana, nani anaweka bei na vigezo gani.

Vinginevyo hapa ni ujanja ujanja tu.
Umefuatilia breakdown ya gharama na ukakosa!?..juzi hapa nilisikia mjadala wa Bei ya kumuona daktari,uliufuatilia..au umebakiza lawama tu
 
Mkuu unajua dialyser moja ina cost kiasi gani?
Zile chemical je ? Ujuuzi na utaalamu wa wafanyakazi wa hospital husika, fee ya consultations?
Usiseme unapigwa , kimahesabu hospital nyingi bado zinarun kwa hasara

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Tarizo si kuchangia. Tatizo ni huyu mbuzi kwenye gunia.

Mgonjwa kafa anadaiwa 10m/- plus. Pesa hizi ni kwa kigezo kipi?

Ujuzi, umeme, machela, vifaa, dawa, maji, au majengo?

Mfuko gani utahimili malipo ya namna hii hospitali zinazopata bajeti tokea tunakokamuliwa sisi kodi na tozo zisizokuwa kifani?
 
Hayupo anayekataa cost sharing ila break down ya gharama ni vyema vikajulikana, nani anaweka bei na vigezo gani.

Vinginevyo hapa ni ujanja ujanja tu.
Kelele zote hizi ni kukosekana kwa Mfumo mzuri wa Bima ya Afya. tutakapoona umuhimu wa Bima ya afya kwa wote nadhani hizi ngonjera za kulilia gharma za matibabu hatutazisikia kwani Bima ya afya kwa wote inaenda kuwa mwarubaini wa changamoto hizi
 
Bingwa gani kasomeshwa na umma ? Si tunalipa kodi? Vifaa kuwa vya umma havihalalishi kutolipiwa mkuu , Mwendokasi ni ya Umma ila tunalipa

Usilete siasa hapo mkuu

Sent from my 220333QAG using JamiiForums mobile app
 
Kwa sasa hv jitahd ukate BIMA ya Afya , bila BIMA ya Afya hutoboi labda uwe fisadi , hata level ya dispensary tuu bila BIMA ya Afya utapata taabu Sana
 
hapa tatizo sio bima, jamaa anauliza gharama za matibabu zinalinga na gharama za huduma?
Kwa mfano dawa x hospitali ya serikali ni sh mia ukienda famasi au binafsi ni sh 50, hii ni kwa nini ? Wakati majengo , madawa ,madocta nk vyote vina pata pesa kutoa kwa watanzania
 
Mtoa mada ungekuwa na bima ya afya usinge lalamika , kata bima ya afya

Serekali Ina tumia Kodi kujenga ,kulipa mishahara na huduma za Bure kama HIV , TB ,Watoto , RCH , maternity n.k

Running cost zote zinakuhusu ,

Siwezi kubali Kodi yangu itumike kukutibia badala wewe ufanye kazi ujitibu wewe na familia Yako , Kodi yangu itakusaidia Kuweka miundo mbinu na vitendea kazi

Serekali imemlipa mfanyalazi unataka na vifaa tiba ikulipie?
 
Kwamba ujuzi na utaalamu siyo? Namwona Bashe kazini akiwachuuza wakulima.

Hapa ilikuwa muafaka kila mtu akishika chake:

1. Mtaalamu ashike utaalamu na ujuzi wake.
2. Mkulima akamate chakula chake
3. Mwenye Kodi na tozo azing'ng'anie.
4. Mwanajeshi akamate makombora yake.
5. Kila mtu na lwake.

Hawa watu wapo kwenye majengo ya umma, dawa za umma, mashine za umma, wanalipwa na umma, nk nk.

Tunakijua kweli tunachokisema?

Kwani hata pesa hizi zinaishia wapi? Kwani wanalipwa wao?
 
Ni mambo ya ubinafsi mtupu. Vigogo wanabinafsisha huduma serikali imewekeza. Wakichunguza watu waadilifu watakuta fedha nyingi wanajilipa watumishi kwa kupeana marupurupu makubwa au wizi wa moja kwa moja.
Ni jambo la kusikitisha kuona eti sera ya kuchangia matibabu imeishia kukandamizwa raia kwa gharama kubwa kiasi hiki.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…