DOKEZO Gharama mpya ambazo Aga Khan wanataka walipwe kwa wateja wa NHIF ni kuhujumu nchi. Haikubaliki

DOKEZO Gharama mpya ambazo Aga Khan wanataka walipwe kwa wateja wa NHIF ni kuhujumu nchi. Haikubaliki

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
NHIf na wizara wanafanya upuuzi na mwisho wa siku anaishia kupata maumivu makali ni mwananchi kwani hamna huduma toshelevu na za uhakika kwa upande wa afya nchini , hawa Agakhan wanaweza funga huduma zao nchi nzima wakabasha kituo kimoja Dar tu , sasa jiulize hizo hospitali za serikali zina uwezo wa kubeba mzigo huo uliobakia ?
Agakhan ni multinational corporation , wapo maeneo mbalimbali so kufunga hapa tz sio kwamba ndio shirika limekufa , wapo Zambia wapo South Afrika nk ,hapa ni kama branch tu .

Na hawa watoa huduma waliobakia watazidi kujiengua na kupunguza vituo na huduma kadiri siku zinavyoenda maana wengi wanadai madeni makubwa mpaka sasa NHIF na hawajalipwa halafu ndio watu akili zitawakaa vizuri na kujua spiralling effects za uongozi mbovu nchini humu
 
Agha Khan hawaitaki NHIF ,hiyo inaitwa akufukuzae....
kuna kamchezo ka kuviziana baina ya aga khan na nhif ingawa athari zake ni wanachama wa nhif wa wananchi wenye kipato kidogo.

aga khan hawana shida na nhif kwenye polyclinics zao shida ipo pale makao makuu ambapo kuna baadhi ya wanufaika wa nhif wanakwenda pale na hapa ndipo nhif nao wanatumia rungu lao kuwapiga pini aga khan (makao makuu + polyclinics)
Hiyo hospital ya Agha Khan ilijengwa Kwa ajili ya Wahindi nyie waswahili mnaoishi Manzese Kwa mfuga mbwa mnafata Nini?
ni sawa kabisa kulingana na ubora wa huduma zenye accreditation ya kimataifa, shida inakuja polyclinics zao kwa sehemu kubwa zinategemea nhif na hapo ndipo nhif wanamwaga ugali kwa kuwa aga khan kamwaga mboga makao makuu yake.
 
Najaribu kuimagine hospitali za binafsi asilimia hata 70 waache kabisa kuoperate ,aisee itakuwa ni kiama ,maana kila mtu ambaye alishakumbwa na kadhia ya kupata magonjwa serious au kuugua na kuuguzwa ataelewa hili nililoandika hapa
 
Huu muda ulotumia kuandika hapa.
Bora ungetumia kuiambia Serikali kuboresha huduma za Afya kwenye Hospital zake zote za Mikoa na Wilaya.
 
Huu muda ulotumia kuandika hapa.
Bora ungetumia kuiambia Serikali kuboresha huduma za Afya kwenye Hospital zake zote za Mikoa na Wilaya.
Aliyendandika anatibiwa India na Uingereza kwa gharama zako mvuja jasho, usimpangie cha kuandika.
 
Mbona hausemi pia wanatozwa kodi kubwa sa unataka wafanye kitu kisichowanufaisha huku ukionekana wazi kuitetea serikali mara sijui samia kanunua ct scan kwani ametoa hela zake mfukoni eeeh.
Serikali ipunguze kodi za huduma za afya na madawa wananchi tutibiwe vema na pia iwalipe wenye hospital maana watu wa bima huchelewa sn kulipa madeni yao.
Aga khan hawalipi kodi. Wana tax exemption.
 
Soda kwenye duka la mangi unainywa kwa shilingi 600, soda hiyo hiyo ukitaka kuinywa pale Samaki samaki mlimani City utainywa kwa shilingi 3000, gharama mara tano zaidi. Umeelewa nini?

Kinachoamua bei ya bidhaa au huduma ni Class ya mtoa huduma iliyolenga Class fulani ya wateja.
Mlala Hoi Haelewi Hilo Mkuu Anafikiri class ya treatment inayotolewa Aga Khan ni sawa na inayotelewa pale Temeke Hosp Shame
 
Back
Top Bottom