Hospitali zingine sio za kwenda kabisa😂Angetoka kwenye hospital ya mkoa rafiki yangu ungelipa gharama nafuu, kimara HC angeenda ngazi inayofuata hata kwa kuandikiwa tuuu tena huko ipo Hospital ya Kimkoa Ubungo, kuna ngazi za refferal rafk ndio maana wamekugonga hela ndefu. Ila mshukuru Mungu umepata watoto safi na Mungu aendelee kuwatunza na kuwapa afya njema na hekima ndani yake
Hio bima ya 50,400 ni bima gani?😆Kuchangiwa na ukoo ni fedhea.
BIMA ni 50,400 tu lakini hamtaki kukata
Mkuu, ulikuwa unajipinda tu kwa shemeji huku mnashangilia, ulitakiwa kujiandaa mapema, yaani unaona mavifaa ya kisasa yamejaaa humo yanang'weka mataa, unaware unachekelea tuWakuu Kwema? Bila shaka muko salama.
Mwezi uliopita Nilikuwa Hospitali ya Taifa ya Mloganzila, Baada ya mke wangu Kuhamishiwa hapo baaada ya Kupewa Rufaa kutoka Kituo cha Afya ambapo alienda Kujifungua. Alienda Hospitali ya kawaida baade madaktari wakashauri awahimishwe Hospitali ya Taifa Mloganzila.
Kitu ambacho Nimeona Gharama za pale ni kubwa sana ni kama Hospitali za Watu Binafsi au Taasisi za Dini n.k
Wakati anapokelewa Pale Emergence nilitakiwa Kulipia Laki moja Fedha Taslimu ambayo wanaita ni ya Accomadation na haina maelezo mengine tena unapewa Control number ulipie ndio aanze Kuhudumiwa.
Baada ya Hapo alijifungua salama watoto wawili Mapacha alikaa siku ya Ijumaa hadi Jumatatu yaani Siku tatu Tu nikapewa Bill ya 1.35 yaani (Milioni moja laki tatu na elfu thelathini na tano) Nikasita kulipa nikaenda kwa wahasibu Kugombana nao Kidogo nikitaka Ufafanuzi japo Ilishindikana.
Baadae niliuliza Nikaambiwa Ghrama ya Kulala kwa Siku ni 50,000 lakini gharama ya Kujifungua ni 750,000. Niliambiwa Hiyo ssera ya mama wajawazito wanajifungua Bure haipo ni Siasa na Propaganda Tu.
Nilipambana nikalipia kiasi nikatoka.
Lakini kwa Kifupi Gharama Za Hospitali ya Mloganzila Ni kufuru kule ndani nilikuta akina mama waliojifungua wana Daiwa Wengine Millioni tatu, tano na kuendelea wameshikiliwa wake pale hadi fedha ipatikane.
Kwa kweli jambo hili linaumiza sana watanzania wa hali ya Chini ambao Kimsingi wanaamini Hospitali za Umma zinazoendeshwa naKupata Ruzuku kutoka serikalini ambayo ni kodi za wananchi gharama zake ziwe rafiki ili kila mwananchi aweze Kumudu ila imekuwa ni Tofauti.
Soma Pia:Gharama zinazotozwa Muhimbili Hospital kuwahudumia “Watoto njiti” zinatuumiza tunaouguza
WIZARA YA Afya Aid Inatakiwa ilitazame hili na wawaweke wananchi wazi kwamba ile ni Hospitali ya Kulipia .
Ushahidi wa Nyaraka zote nianzo Mods musifute mukitaka ushahidi wa Receipt na Bill nitawapa
Bima gani hio mkuu tufahamishane😂Mchawi ni bima tu , walau gharama zinapungua
Wakiwashikilia wanawaweka wapi?🤣 Au kuna mahabusu za wazazi?Aisee nilikuta watu wengi sanawanadaiwa kule na wameshindwa kutoka wameshikiliwa zaidi ya mwezi na hili ndio linaloumiza zaidi
Hio sera ni kwa vituo vya afya😂 ila hospitali za kitaifa hazihusiki na sera hizo. Unapigwa kwenzi kama kawaida.Sera ya Afya ya 2007 inaelekeza kuwa Matibabu ya Mama Mjamzito na Watoto chini ya Miaka 5 ni bure.
Aidha Dkt. Mollel amesema kuwa anatambua kuwa zipo baadhi ya Hospitali za Umma zinazotoza wananchi fedha na kuzitaka kuacha mara moja huku Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya wakitakiwa kusimamia jambo hilo.
Dkt. Mollel hakusema kuwa hakuna Hospitali isiyotoza watu kwa ajili ya kupata huduma hiyo kama ilivyoandikwa hapo juu.
Bima ipi mnayoisemea. Hii ambayo katika dawa 5 unazoandikiwa 2 ni bure ila tatu ukanunue Pharmacy za jirani?Kabisa, ukiwa na Bima haisumbui
Huo ujinga ndio ulinifanya ni drop swala la Bima. Kimsingi Bima inatakiwa ku cover kila kitu tena upate huduma first class sababu wewe ni mteja wa Prepaid.Mchawi pesa bima hupati uduma nzuri na rafiki lakin pia bima ni usumbufu baada ya kudeal na mgojwa unawaza kuzaja makaratasi na baadhi ya dawa watakwambia hazitolewi kwa bima
So pesa Muhimu
Kibabu kinawaambia mnywe juisi ya tango na kipande cha samaki ili kuepusha ugonjwa wa moyo.Halafu Kile kibabu cha Muhimbili Janabi badala ya kufanya tafiti namna gani huduma zao ziwe za bei rafiki kwa wananchi yeye kila siku nikutaka kutrend na vitu vya hovyo hovyo...watu wa hivi enzi za u communist ilikua nikunyongaa tu.
😂😂😂😂😂😂 Amka utajikojolea mkuuMchawi bima2 kwa sasa
Kwa kuwaa umesema ullienda private hospital ghalama kuwa kubwa sio jambo la ajabu hasa kama operation zinahusika. Lakini kufika 5M ni wewe ulitengeneza mazingira hayo ingewezekana kuishia 2.5M. Kwanza kwa nini uende hospital ikutoze 2M halafu bado Daktari utafute wewe umlipe 2.5M? Ilitakiwa huyo Daktari kama anahusika na hiyo hospital ulipompa hiyo 2.5M mengine yote amalize kwenye bajeti hiyo.Mtoto wangu wa kwanza wa kike alijifungua nilitumia million 5, ilikuwa kama movie.
Hospital nilikupa 2 million private, mtoto alikuwa amekaa vibaya mno na pia kajifunga na umblical cord.
Madaktari waliangaika 4 hours kuweka sawa afya ya mama kabla hawajamfungulisha. Anesthesia alidai sijui presha imecanyaje akifanyi2a operation lazima mama aende
Nilitoka fasta baada ya kupewa akili, kumtafuta dokta bingwa gyno, naye alitaka 2.5 million ili atoke kwenye kazi yake. Analipwa kwa saa
Niliona bora nimpe tu hapo sijui kama mtoto ama mama atapona. Gyno na wenzake walifanya juhudi, operation ilikuja fanyika ndani kuna madaktari saba, gyno wawili, manesi na anesthesiologist, acha tu
Naambiwa mkeo kajifungua mtoto wa kike kwa kisu, nililia kama fala. Huwa silii na sijawahi lia hata msibani, siku anayokufa bibi kwanz usiku wake nilikul mzigo, yan kifup hata misib ikitokea nakula mzig. Inawezekana nina shida sehemu kwan hata majonzi haya yanaendelea nchin bado siku zote hizi nimekul mzigo, niombeen nina shida sehemu, thanks
Nisitoke nje ya mada, mtoto alizaliw, nilitumia gharama nyingine hapo kati. Sasa nina binti mtundu sana, mke wangu yuko salama mishono tu huwa inamuuma
Hii kulalamika ni kwa sababu hatuna hela. Gharama za kuzalisha tanzania ni nafuu compared to states. Serikaii ibireshe na indelee kupunguza jwa kulipia asilimia kubwa zaidi
Tutafute hela ndugu zangu, umaskini mbaya sana
DaaahKuchangiwa na ukoo ni fedhea.
BIMA ni 50,400 tu lakini hamtaki kukata
NHIF imekuwa kichefuchefu sana sasa hvBima ipi mnayoisemea. Hii ambayo katika dawa 5 unazoandikiwa 2 ni bure ila tatu ukanunue Pharmacy za jirani?
Tumia Jubilee Insurance. Downside ni kuna mikoa haipo zaidi ya mjini so ni changamoto ila switch huko nenda hospital za hadhi na hiyo bima halafu lete mrejesho.Huo ujinga ndio ulinifanya ni drop swala la Bima. Kimsingi Bima inatakiwa ku cover kila kitu tena upate huduma first class sababu wewe ni mteja wa Prepaid.
Ila bongo mtu wa bima unaonekana kama fala ambaye unatibiwa bure. Yani treatment ya watu wa Bima ni kama ya mbuzi na sio binadamu. Mtapangishwa foleni mistari hata mitatu na kauli za kejeli kadri wahudumu watakavyojiskia. Ila watu wa cash wao ni fasta na wanapapatikiwa 😂 kama raia wa kigeni. Bima its a No No kwangu mimi bora kutumia cash tu kwa tulipofikia.
Hamna bima mle ni kizungumkuti tuNHIF imekuwa kichefuchefu sana sasa hv
Nitaifatilia hiyo JubileeTumia Jubilee Insurance. Downside ni kuna mikoa haipo zaidi ya mjini so ni changamoto ila switch huko nenda hospital za hadhi na hiyo bima halafu lete mrejesho.
NHIF inasemekana ni wazito kulipa kwa wakati ndiyo sababu kuna kipindi baadhi ya hospital waliachana na NHIF kabisa.
Kuna baadhi ya maamuzi hufanyika wanaoumia watu wa kawaida, kuna baadhi ya vipimo na treetment lazima uchangie. Ila wao wanatibiwa kwa kodi zetu yaan ni usenge mtupuHamna bima mle ni kizungumkuti tu
Kam alisomea ualimu alipaswa kujal zaid kwakuw aliwah kuishi maish magumuShida ni waziri wa afya aliesomea ualimu kupewa asimamie sekta ya afya