Mkuu, upo sahihi! Mwaka juzi, mtoto wangu alichaguliwa kwenda Mafinga JKT, nami nipo Mwanza. Kwa upande wangu, ilikuwa nafuu, kwani kuna wengine walichaguliwa kwenda Songea.
Nikatumia nauli, pamoja na baadhi ya vifaa. Kufika huko, ikabidi arudi ili aje achague vyuo, hivyo ikanibifi nimtumie nauli. Baada ya hapo, nikamrudisha huko Mafinga. Baada ya kumaliza, ikabidi nigharamie nauli.
Ile kufika tu Mwanza, akaugua na kupelekea kulazwa hospitali wiki nzima!
Kwa kweli, binafsi sioni faida yoyote ya kupeleka watoto wetu huko. Mwenda zake, alikuwa anataka kuonyesha kuwa kila kilichowashinda/kuacha wenzie, yeye alikiweza!