Gharama za Maisha Zanzibar Zipo Juu sana

Gharama za Maisha Zanzibar Zipo Juu sana

Wanadai ni mji wa kitalii!
Kuna jamaa alinidokeza kuwa wenye ndugu majuu huwa wanawatumia ndugu zao mchele, mafuta ya kupikia, sukari, beans, nyanya za kopo nk nk !
Nilishangaa mno! Je wenyeji wavivu? Au ndio uislamu imewadhoofisha wasilime, kufanya kazi au ?!
Very embarrassing aiseee....
Kwahiyo Qatar, Saudi, Dubai, Brunei hakuna waislam?
 
Mtoa mada yupo sahihi...

Maisha ya Zanzibar ni ghali hasa kama alivyosema kuanzia chakula hadi malazi (hotel)

Nilikula ugali makange ya Samaki Kwa elfu 24 (Samaki alikuwa mdogo) tofauti na DSM (shilingi 18k makange ya Samaki sato )

Nililala hotel sea view (pale Mazizini) shilingi 120,000/day

Bei ya tax, Umbali wa kilomita 5 tu utalipa shilingi 20,000 wakati huku Bara ningelipia 10k tu 🙌

Kwakuwa ilikuwa ni safari yangu ya mapumziko, ambayo nilishaanda bajeti yake sikuona shida sana.
Nashauri kama unaenda kwaajili ya mapumziko vyema kuandaa bajeti ya kutosha.
IMG_20240723_145758_425.jpg
 
Wanadai ni mji wa kitalii!
Kuna jamaa alinidokeza kuwa wenye ndugu majuu huwa wanawatumia ndugu zao mchele, mafuta ya kupikia, sukari, beans, nyanya za kopo nk nk !
Nilishangaa mno! Je wenyeji wavivu? Au ndio uislamu imewadhoofisha wasilime, kufanya kazi au ?!
Very embarrassing aiseee....
sasa wewe unaumizwa na lipi hapo? Ikiwa wenyewe wameridhia kuwatumia ndugu zao vyakula basi ni sawa, mimi na wewe tusiokuwa na ndugu wa kututumia vyakula hivyo basi tuendelee kupiga mchele wa Ifakara na nyanya za Iringa
 
Mtoa mada yupo sahihi...

Maisha ya Zanzibar ni ghali hasa kama alivyosema kuanzia chakula hadi malazi (hotel)

Nilikula ugali makange ya Samaki Kwa elfu 24 (Samaki alikuwa mdogo) tofauti na DSM (shilingi 18k makange ya Samaki sato )

Nililala hotel sea view (pale Mazizini) shilingi 120,000/day

Bei ya tax, Umbali wa kilomita 5 tu utalipa shilingi 20,000 wakati huku Bara ningelipia 10k tu 🙌

Kwakuwa ilikuwa ni safari yangu ya mapumziko, ambayo nilishaanda bajeti yake sikuona shida sana.
Nashauri kama unaenda kwaajili ya mapumziko vyema kuandaa bajeti ya kutosha.
View attachment 3072188
Mkuu Mimi Niko Paje uku Villa Moja nalipia 90$, soon narudi Bongo
 
Samaleko..

Kabla hujawaza kwenda Ulaya, America au Asia kula maisha jitaidi sana uanzie Zanzibar ujionee maajabu ya bei za vitu.
Kiufupi Huku Zanzibar ni sawa tu na Ughaibuni, ukiweza kumudu kula bata kwa muda wa mwezi mmoja maeneo kama Kendwa, Nungwi, Kiwengwa au Paje basi unaweza kumudu kukaa DXB ndani ya wiki mbili, Angalau Stone Town unaweza kusurvive.

Kwa experience yangu hapa Tanzania sijaona sehemu inaifikia Zanzibar kwa gharama za maisha.

All in all Karibuni Zanzibar, ni Kuzuri sana.
Kwanza unasemea zanzibar ipi pwani kwa watalii au mwanakwerekwe huko..!

Kama ni pwani kwa watalii huko sio size yako na sio size ya watanzania wengiii..

Ila sehemu nyingine zanzibar nikawaida kama sehemu nyingine Tanzania
 
Ndizi Buku Benga? Yaan ndizi 1 2000 km 2000

Ndio maana kuna mjerumani mmoja nilikutana nae huku bara akiwa kwenye hotel 1 ya nyota 3 akanunua Maji kwenye duka 1 Maji yale ya 700 mawili akapewa chenji 600 yaan mawili jumla 1400 alitoa 2000 yeye hakuelewa kingereza anajua si sana akaniomba nimuelekeze imekuaje amerudishiwa 600 sasa sikuelewa kwamba Jamaa aliona amezidishiwa Hela au amepunjwa

Ila km Zenji wanawapiga naona mjerumani yule aliona km amezidishiwa Hela ndio maana alipagawa kudadadeq leo ndio nimeelewa sasa kwanini yule mjerumani alikua amepagawa kuona ametoa Buku 2 kapewa Maji 2 ya kunywa na chenji ikarudi juu kapagawa ahamini macho yake imekuakuaje 2000 Maji makubwa 2 na chenji ikarudi mjerumani yule hakuamini naona huko Zenji alikutana na kitu kizito
Achana na ndizi kwanza, huku kinywaji Cha jero hakuna, Zanzibar nzima hukuti
 
Pesa ni ngumu sana kuipata kwa mkazi wa kawaida.
Yaani ule ni mji wa kwenda kutalii na kurudi, si mji wa kupiga kambi.
Kuna tabaka kubwa la walionazo na wenzangu na mimi.
Deal ni wale wanafamilia waliofanikiwa kutoka na kwenda ishi arabuni ndio msaada mkubwa, wanaokoteza mavitu ya mitumba na kuyatuma kisiwani. Thoo biashara imekua ngumu kwa sasa sababu target ni kuwauzia wabara.
Uwepo wa nyundo la Tra (wenyewe wanawaita kastam) umedororesha biashara hiyo. Wabara hawana mzuka tena na maelektroniki yao.
Nimeshangaa sana kukuta ZRA na TRA huku Zanzibar, sijajua zinaoperate vipi.
 
Back
Top Bottom