Gharama za Maisha Zanzibar Zipo Juu sana

Kwahiyo Qatar, Saudi, Dubai, Brunei hakuna waislam?
 
Mtoa mada yupo sahihi...

Maisha ya Zanzibar ni ghali hasa kama alivyosema kuanzia chakula hadi malazi (hotel)

Nilikula ugali makange ya Samaki Kwa elfu 24 (Samaki alikuwa mdogo) tofauti na DSM (shilingi 18k makange ya Samaki sato )

Nililala hotel sea view (pale Mazizini) shilingi 120,000/day

Bei ya tax, Umbali wa kilomita 5 tu utalipa shilingi 20,000 wakati huku Bara ningelipia 10k tu 🙌

Kwakuwa ilikuwa ni safari yangu ya mapumziko, ambayo nilishaanda bajeti yake sikuona shida sana.
Nashauri kama unaenda kwaajili ya mapumziko vyema kuandaa bajeti ya kutosha.
 
sasa wewe unaumizwa na lipi hapo? Ikiwa wenyewe wameridhia kuwatumia ndugu zao vyakula basi ni sawa, mimi na wewe tusiokuwa na ndugu wa kututumia vyakula hivyo basi tuendelee kupiga mchele wa Ifakara na nyanya za Iringa
 
Mkuu Mimi Niko Paje uku Villa Moja nalipia 90$, soon narudi Bongo
 
Kwanza unasemea zanzibar ipi pwani kwa watalii au mwanakwerekwe huko..!

Kama ni pwani kwa watalii huko sio size yako na sio size ya watanzania wengiii..

Ila sehemu nyingine zanzibar nikawaida kama sehemu nyingine Tanzania
 
Achana na ndizi kwanza, huku kinywaji Cha jero hakuna, Zanzibar nzima hukuti
 
Nimeshangaa sana kukuta ZRA na TRA huku Zanzibar, sijajua zinaoperate vipi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…