Gharama za Maisha Zanzibar Zipo Juu sana

Gharama za Maisha Zanzibar Zipo Juu sana

Hapo Michamvi usikose kuhudhuria swimming part kama sijakosea ni kila Jumanne usiku. Usisahau kupita na hapo chuoni kwa watasha wanaojifunza kiswahili.
Naomba location exactly ya iyo swimming party mkuu kama hutojali maana uku Usiku kuna poa sana
 
Nipo na baharia mmoja mzaliwa wa apaapa Paje ananambia hawa beach boys wa kimasai wanatumia madawa kuwarubuni hawa wadada wa kizungu na kutoka nao kimapenzi,
IMG_20240823_153052_320.jpg
vipi Kuna ukweli wowote katika ilo wadau?
 
Una ruhusiwa ila inabidi ukajenge Mashambani ukijenga mjini huta pata wateja kwasababu wenyeji wa uko siyo watumiaji wa lodge wao mfumo wao utakuta kijana Kaoa au hajaoa bado anaishi nyumbani kwa wazazi ila wanapanga chumba kwaajili ya kukutana na wapezi wao au michepuko kwa upandr wa waume za watu.
Kweli kabisa.
 
Si vyakula,si mavazi ,si usafiri,bei ni kali hasa, nimenunua parachichi bei ni elfu 3500, Mwanzo unakuona kugumu, Mwanzo nilikuwa nashangaa bei ya nyanya moja ni sh.1000,kitunguu 700 kidogo hakikidhi,,,, kwa siye tuliozoea bei chee ukija huku lazima uteseke,,,,lakini kawaida. Kwa wanaonunua kwa kimojakimoja wanateseka, Znz kitu chenye bei poa ni boflo,chocolate na mabiskut,
 
Si vyakula,si mavazi ,si usafiri,bei ni kali hasa, nimenunua parachichi bei ni elfu 3500, Mwanzo unakuona kugumu, Mwanzo nilikuwa nashangaa bei ya nyanya moja ni sh.1000,kitunguu 700 kidogo hakikidhi,,,, kwa siye tuliozoea bei chee ukija huku lazima uteseke,,,,lakini kawaida. Kwa wanaonunua kwa kimojakimoja wanateseka, Znz kitu chenye bei poa ni boflo,chocolate na mabiskut,
Vitu viko juu kweli ila kumekaa poa sana, I don't regret staying here. Pilikapilika za Dar sio kabisa
 
Ndizi Buku Benga? Yaan ndizi 1 2000 km 2000

Ndio maana kuna mjerumani mmoja nilikutana nae huku bara akiwa kwenye hotel 1 ya nyota 3 akanunua Maji kwenye duka 1 Maji yale ya 700 mawili akapewa chenji 600 yaan mawili jumla 1400 alitoa 2000 yeye hakuelewa kingereza anajua si sana akaniomba nimuelekeze imekuaje amerudishiwa 600 sasa sikuelewa kwamba Jamaa aliona amezidishiwa Hela au amepunjwa

Ila km Zenji wanawapiga naona mjerumani yule aliona km amezidishiwa Hela ndio maana alipagawa kudadadeq leo ndio nimeelewa sasa kwanini yule mjerumani alikua amepagawa kuona ametoa Buku 2 kapewa Maji 2 ya kunywa na chenji ikarudi juu kapagawa ahamini macho yake imekuakuaje 2000 Maji makubwa 2 na chenji ikarudi mjerumani yule hakuamini naona huko Zenji alikutana na kitu kizito
Hahah akina Nasoro ukijichanganya wanakupa za uso.
 
Wanadai ni mji wa kitalii!
Kuna jamaa alinidokeza kuwa wenye ndugu majuu huwa wanawatumia ndugu zao mchele, mafuta ya kupikia, sukari, beans, nyanya za kopo nk nk !
Nilishangaa mno! Je wenyeji wavivu? Au ndio uislamu imewadhoofisha wasilime, kufanya kazi au ?!
Very embarrassing aiseee....
Za kuambiwa changanya na zako.Yaani ndugu wa majuu watume mchele mafuta ya kupikia,sukari,beans na nyanya kopo?
Na wewe ukaamini kwamba ni kweli?Hao wa majuu wapo Nchi zipi,Wanapewa hizo bidhaa bure huko majuu? Gharama za usafiri huwa ni bure?
Yaani hizo bidhaa ziwe nafuu majuu kuliko Zanzibar?
Bei ya sukari Zanzibar unaijua?
Mambo mengine unapodokezwa shirikisha ubongo.
Wanatumiwa pesa inge make sense.
 
Anotaka kuja kutembea Zanzibar jamani tuwasiliane nipo hapa kijana mwenzenu tembea nami utembee ,ufurahi na kujenga urafiki wa kudumuu

Karibuni jamani
Zanzibar ni njema atakae aje
 
TRA haihusiki na mapato ya zenji..
ZRA wanakusanya trillion 1 na ushee kwa kila mwaka wa fedha. Kutoka vyanzo vyao vya Zenji.

Nimekaririshwa hivyo..ila sijiamini sana.Naruhusu kukosolewa..Maana hata Zanzibar sijawahi kufika.
Karibu zanzibar
 
Zanzibar umri wa kuishi upo chini sana kwa utafiti niliyo ufanya wazee wachache saba, kwenye familia kumi ya watoto kuanzia Miaka 30 kukuta wana wazazi wapo Hai ni familia 2 tu familia 8 hazina wazazi wamefiwa na wazazi yani kukuta kijana mkubwa mwenye miaka 45 bado wazazi wake wapo hai ni ngumu, kingine nilicho ona Wazanzibar wanawahi kuzeeka mapema na kuchoka kwa Marathi hii inasababishwa na uraji wa vyakula kutoka nje, utakuta Mzanzibar mpaka ana Zeeland hajawai kula kuku wa kienyeji wao kuku wao ni kutoka Uturuki na nchi nyinginezo na Mchele hivyo hivyo wanapenda Michele ya nje haina ubora. Ukimchukua kuja wa Tanganyika mwenye miaka 20 na kijana Wa Zanzibar mwenye miaka 20 kijana wa Zanzibar anaoneka mkubwa ana karibia miaka 27 kimuonekano.
Karibu zanzibar
 
Back
Top Bottom