Gharama za Ujenzi kwa Nyumba za ‘Contemporary’ Vs ‘Traditional’ Roof

Hata mimi nilikuwa na wazo Hilo Hilo. Ukitumia zege umemaliza kila kitu,
 
Ahsante sana kiongozi na tumefaidika wengi na nikushukuru mno.........kwangu inaweza kuwa tabu kufanya hizo application kwani tayari nimeshaezeka na ni nyumba ya mapaa mawili yanayokutana kwenye mfereji hivyo nafasi iliyobaki sihisi kama itatosha fundi kupitisha mikono na kufanya kwa ufasaha ila ngoja nijaribu
 
Nimejenga hiyo contemporary baada ya mke na watoto kutaka mtindo huo japo niliwatahadhalisha kwa uzoefu wa kusikia uvujaji wake....nikakubaliana nao ila iwe ni ya mapaa mawili tuu na imejengwa na tukakubaliana hatuweki gypsum board mpaka msimu wa masika upite ili tuone wapi na wapi kuna vuja na nini cha kufanya kudhibiti huo uvujaji
Masika ndo hii,uvujaji kiasi (kwa matone)upo kwenye misumari km sehemu tano,fundi aliipiga kwa pembeni ya mbao,gutter (mfereji)unakuwa na unyevu kiasi kuna sehemu mpaka kunadondosha matone ya maji na kunakuwa na unyevu kwenye tofali za juu kulipochimbiwa bati (kuna sehemu humu nimesoma kuwa ni kosa kuchimbia bati)
Kwa muktadha huu naombeni ushauri wa nini cha kufanya au nani(experts)wa kuwaona sio mafundi mchundo
 
Hata mimi nilikuwa na wazo Hilo Hilo. Ukitumia zege umemaliza kila kitu,
Sure mkuu unamwita tu mtaalamu anakusaidia mahesabu kwa mzigo huo wa slab marefu na mapana kutokana na nyumba yako utahitaji nguzo ngapi nondo ngapi mm ngapi maana si ghorofa chap unasahau kbs hizi mbwembwe za slope sijui material gani na gani ni temporary tu unaweza jikuta material yote hayo plus bati mbao gati unachosevu ni kdg sana.ukiweka zege umemaliza ila huu mpango mwingine baada ya miaka kadhaa lazima uvue uvalishe tena,hili zoezi utarudia na kurudia kila baada ya muda,ukija kujumlisha cost baada ya kipindi flani unaweza ukakuta umeenda maradufu ya gharama ya awali,tukumbuke material hupanda bei kila siku pia.Leo si sawa na jana.
 
Wanakuja mkuu
 
Kama vile umeyasema mawazo yangu

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
versatile ni madoido kikubwa nyumb isivuje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
yan umwage slab kabisa kuua mzizi wa fitina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Assume wewe ni mtanzania wa kawaida na unataka kujenga nyumba ya aina hiyo ungefanyeje?
 
Assume wewe ni mtanzania wa kawaida na unataka kujenga nyumba ya aina hiyo ungefanyeje?
Jiridhishe juu ya uwezo wa fundi unakabidhi kazi kabla hujaweka pesa yako. Sio tatizo kutumia fundi wa gharama nafuu kama umejiridhisha juu ya uwezo wake. Tatizo ni pale unapompa tu kazi kisa kataja gharama nafuu kuliko wengine.
 
Haya hyo slab usipofanyia treatment inavuja vile vile!
 
Fundi ana takiwa afanye nini katika upasuaji wa aina hii ili mjengo usi uje?
 
Kuna wajinga wanachimba tu ukuta anachomeka bati anapiga cement sijui na waterproof. Nyumba lazima ivuje, na pia kutu kwenye bati itakuja mapema sana. Synroof(Bitumen) bei ya ndoo moja 20kg ni 225,000 naona watu wengi wanakimbia bei au hawaijui
Sasa hapo kuna kuokoa gharama zipi? Materials ndio hayo na gharama ya ufundi ni kubwa.
 
Hii ya Mbuzi kula urefu wa kamba kumbe siku nyingi imenzaga.,[emoji1787][emoji1787]
 
Tunauza mbao kwa bei za jumla
2*4 fut 12=4400
2*4treated fut 12=4800
1*6 fut 12 = 4400
1*8 fut 12= 8500
1*8 ya fisherboard=9500
1*10=13500
1*10 ya fisherboard= 15000
2*2treated fut 12=2500
2*2 fut 12=2300
2*4treated fut 18=9500
2*6 fut 12=8500
2*6treated fut 18=16000
2*2treated fut 18=5000
2*3 fut 12=3500
1*4 fut 18=4000
1*4 fut 12=2500
Tunafanya delivery popote ulipo kwa Dar-es-salaam ,tunapatikana kwa namba hizi hapa 0759630751,
0654830416,
0687371138
vile vile huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu ..
Ofisi zetu ziko Mbuyuni -Bagamoyo road
 
Shida kubwa ya contemporary House ni bati kuharibika mapema, Kwa maana bati Lina slope ndogo then linakaa na maji muda mrefu na kulifanya lioze haraka.
Shida hii haiwez onekana angalau after 6-13 yrs, Ila nawashauri wenye nyumba hizi wajipange sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…