Gharama za Ujenzi kwa Nyumba za ‘Contemporary’ Vs ‘Traditional’ Roof

Gharama za Ujenzi kwa Nyumba za ‘Contemporary’ Vs ‘Traditional’ Roof

Mkuu Heri kwako ila twende mbele turudi nyuma, nyumba zile kweli za contemporary kweli ile contemporary house bongo ni chache sana,,kwa upeo wangu mdogo,mara nyingi nyumba za contemporary hutawaliwa almost 90% kwa concrete na glass,hata huko juu wabongo tunaforce kuweka bati tena kuna wengine wanajinasibu kuweka bati cheap zaidi kwa vile watu hawalioni ili kukwepa gharama,pasipo kuhusisha factors nyingine ikiwepo hali ya hewa,ubora wa matumizi ya material yenyewe kwa shughuli husika,kutu si rafiki baada ya miaka kadhaa,ukiacha swala la kuvuja pembeni,dawa ni kupiga zege tu,mwite fundi akupe makadirio na ushauri,fit kwny design yako, anza nondo mdogo mdogo,mifuko ya cement,gari kokoto,gari mchanga,pvc,mbao,hela ya fundi material ndogo ndogo,kata mzizi wa fitna ishi kweli kwny contemporary house.vinginevyo wabongo tunafake tu.[emoji3]
Hata mimi nilikuwa na wazo Hilo Hilo. Ukitumia zege umemaliza kila kitu,
 
Ahsante sana kiongozi na tumefaidika wengi na nikushukuru mno.........kwangu inaweza kuwa tabu kufanya hizo application kwani tayari nimeshaezeka na ni nyumba ya mapaa mawili yanayokutana kwenye mfereji hivyo nafasi iliyobaki sihisi kama itatosha fundi kupitisha mikono na kufanya kwa ufasaha ila ngoja nijaribu
 
Nimejenga hiyo contemporary baada ya mke na watoto kutaka mtindo huo japo niliwatahadhalisha kwa uzoefu wa kusikia uvujaji wake....nikakubaliana nao ila iwe ni ya mapaa mawili tuu na imejengwa na tukakubaliana hatuweki gypsum board mpaka msimu wa masika upite ili tuone wapi na wapi kuna vuja na nini cha kufanya kudhibiti huo uvujaji
Masika ndo hii,uvujaji kiasi (kwa matone)upo kwenye misumari km sehemu tano,fundi aliipiga kwa pembeni ya mbao,gutter (mfereji)unakuwa na unyevu kiasi kuna sehemu mpaka kunadondosha matone ya maji na kunakuwa na unyevu kwenye tofali za juu kulipochimbiwa bati (kuna sehemu humu nimesoma kuwa ni kosa kuchimbia bati)
Kwa muktadha huu naombeni ushauri wa nini cha kufanya au nani(experts)wa kuwaona sio mafundi mchundo
 
Hata mimi nilikuwa na wazo Hilo Hilo. Ukitumia zege umemaliza kila kitu,
Sure mkuu unamwita tu mtaalamu anakusaidia mahesabu kwa mzigo huo wa slab marefu na mapana kutokana na nyumba yako utahitaji nguzo ngapi nondo ngapi mm ngapi maana si ghorofa chap unasahau kbs hizi mbwembwe za slope sijui material gani na gani ni temporary tu unaweza jikuta material yote hayo plus bati mbao gati unachosevu ni kdg sana.ukiweka zege umemaliza ila huu mpango mwingine baada ya miaka kadhaa lazima uvue uvalishe tena,hili zoezi utarudia na kurudia kila baada ya muda,ukija kujumlisha cost baada ya kipindi flani unaweza ukakuta umeenda maradufu ya gharama ya awali,tukumbuke material hupanda bei kila siku pia.Leo si sawa na jana.
 
Wanakuja mkuu
 
No doubt Fundi tatizo. Wabongo tunapenda sana vitu cheap badala ya vitu affordable. Mtu anataka kujenga anaungaunga kuanzia ramani mpaka mafundi ujenzi kila kitu unataka the cheapest.

Au mtu anachorewa ramani lakini atakwambia anafundi wake, kisha anaenda kutafuta fundi wa bei nafuu bila hata kuwa na uhakika juu ya ujuzi wa fundi husika. Na tatizo ni kuwa hakuna fundi atakuambia hajui kazi
Kama vile umeyasema mawazo yangu

Sent from my SM-A015F using JamiiForums mobile app
 
Mwanzoni nilianza kuwa muumini wa contemporary roofing lakini ushuhuda nnaopata kutoka kwa walioezeka kwa style hyo unanipa mashaka makubwa na jirani yangu ameijenga nyumba inavuja kama nje ,mafundi wapo ila guarantee ya kukupaulia isivuje hana, dhumuni mama la kupaua nyumba ni kukukinga na jua na mvua na uchafu unaotoka juu, sijui mambo ya contemporary au classical roofing au msouth versatile au romantile simba dumu ni namna tu ya kutafuta mvuto ili lengo mama litimie. Lengo lisipotimia na nyumba ikaanza kuvuja hakuna maana ya kupaua .
versatile ni madoido kikubwa nyumb isivuje

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu Heri kwako ila twende mbele turudi nyuma, nyumba zile kweli za contemporary kweli ile contemporary house bongo ni chache sana,,kwa upeo wangu mdogo,mara nyingi nyumba za contemporary hutawaliwa almost 90% kwa concrete na glass,hata huko juu wabongo tunaforce kuweka bati tena kuna wengine wanajinasibu kuweka bati cheap zaidi kwa vile watu hawalioni ili kukwepa gharama,pasipo kuhusisha factors nyingine ikiwepo hali ya hewa,ubora wa matumizi ya material yenyewe kwa shughuli husika,kutu si rafiki baada ya miaka kadhaa,ukiacha swala la kuvuja pembeni,dawa ni kupiga zege tu,mwite fundi akupe makadirio na ushauri,fit kwny design yako, anza nondo mdogo mdogo,mifuko ya cement,gari kokoto,gari mchanga,pvc,mbao,hela ya fundi material ndogo ndogo,kata mzizi wa fitna ishi kweli kwny contemporary house.vinginevyo wabongo tunafake tu.[emoji3]
yan umwage slab kabisa kuua mzizi wa fitina

Sent using Jamii Forums mobile app
 
No doubt Fundi tatizo. Wabongo tunapenda sana vitu cheap badala ya vitu affordable. Mtu anataka kujenga anaungaunga kuanzia ramani mpaka mafundi ujenzi kila kitu unataka the cheapest.

Au mtu anachorewa ramani lakini atakwambia anafundi wake, kisha anaenda kutafuta fundi wa bei nafuu bila hata kuwa na uhakika juu ya ujuzi wa fundi husika. Na tatizo ni kuwa hakuna fundi atakuambia hajui kazi
Assume wewe ni mtanzania wa kawaida na unataka kujenga nyumba ya aina hiyo ungefanyeje?
 
Assume wewe ni mtanzania wa kawaida na unataka kujenga nyumba ya aina hiyo ungefanyeje?
Jiridhishe juu ya uwezo wa fundi unakabidhi kazi kabla hujaweka pesa yako. Sio tatizo kutumia fundi wa gharama nafuu kama umejiridhisha juu ya uwezo wake. Tatizo ni pale unapompa tu kazi kisa kataja gharama nafuu kuliko wengine.
 
Sure mkuu unamwita tu mtaalamu anakusaidia mahesabu kwa mzigo huo wa slab marefu na mapana kutokana na nyumba yako utahitaji nguzo ngapi nondo ngapi mm ngapi maana si ghorofa chap unasahau kbs hizi mbwembwe za slope sijui material gani na gani ni temporary tu unaweza jikuta material yote hayo plus bati mbao gati unachosevu ni kdg sana.ukiweka zege umemaliza ila huu mpango mwingine baada ya miaka kadhaa lazima uvue uvalishe tena,hili zoezi utarudia na kurudia kila baada ya muda,ukija kujumlisha cost baada ya kipindi flani unaweza ukakuta umeenda maradufu ya gharama ya awali,tukumbuke material hupanda bei kila siku pia.Leo si sawa na jana.
Haya hyo slab usipofanyia treatment inavuja vile vile!
 
Habarini wakuu,

Kuna mjadala uliletwa humu kuhusu ni nyumba zipi zina gharama nafuu kwenye ujenzi kati ya hizi za kisasa za kuficha bati (‘contempoarary) na zile za kawaida. Ambapo kwa uzoefu wangu nilijaribu kuelezea kuwa kwa kawaida tunatarajia nyumba za paa la kuficha zitatumia tofali nyingi huku bati na mbao zikitumika kidogo sana (maranyingi haizidi nusu) wakati hizi za paa la kawaida zinatumia tofali chache huku zikitumia bati na mbao nyingi zaidi.

Lakini kuna mambo ya kuzingatia
1. Ongezeko la tofali kwenye contemporary house si kubwa sana kulinganisha na utofauti wa mahitaji ya mbao na bati za kupaulia baina ya aina hizi mbili za upauaji wa nyumba.

2. Gharama za mbao na bati kwa ujumla wake zinakupa ongezeko kubwa la gharama kwa nyumba za kawaida kulinganisha na contemporary house.

3. Kuna kitu kinachoongezeka kwenye nyumba za contemporary ambacho ni ‘concrete Gutter’ (mitaro ya kukusanya maji). Ambacho kwa mtazamo wangu nili commet kuwa ndio hasa kinaweza kufanya unafuu wa contempoary uliotokana na roofing ukaja kujilipa (kwa kukalibia au hata kuzidi) kulingana na idadi na namna mitaro ya maji ilivyowekwa kwenye nyumba amabyo kwa namna flani inatokana na ‘spatial arrangement’ ya ndani na namna flani za kuboresha mvuto wa jengo (Contemporary house zinaongezeka mvuto with complexity).

Hivyo basi pendekezo langu lilikuwa ni kwamba kama unataka kujenga kwa kuficha bati na huku pia ukitaka kupunguza gharama ni muhimu kuzingatia mpangilo wa nyumba utakao kufanya uepuke kujenga mitaro mingi kwenye nyumba.

Au unaweza kuepuka kabisa ujenzi wa mitaro kwa kuacha wazi upande wa nyuma ambao ndio maji yataelekezwa huko, na hii ni nzuiri zaidi maana pia itakupunguzia idadi ya tofali ambazo zingehitajika upande wa nyuma huku pia ukiepuka materials kwaajili ya ujenzi wa gutter ambalo lingehitaji zege la nondo.

Na kwakuongeza tu namna hii ya kuacha wazi upande wa nyuma iatakusaidia kupunguza risk ya nyumba kuvuja endapo hukutumia fundi mwenye uzoefu/ujuzi wa nyumba hizi, so risk ya kuvuja itabaki kuwa kwenye maungio ya bati na ukuta (kama fundi ni kimeo).
Kwa maelekezo zaidi juu ya masuala yote yahusuyo ujenzi unaweza kutucheki whatsapp 0717682856.

Unaweza kuona mfano wa hako ka ramani hapo chini (kalichorwa kwa lengo la kusave space na gharama). Kana vyumba vitatu (1master), kiStudy room kidogo, kitchen, dining na public toilet.

View attachment 1745814

View attachment 1745815

View attachment 1745816
Fundi ana takiwa afanye nini katika upasuaji wa aina hii ili mjengo usi uje?
 
Kuna wajinga wanachimba tu ukuta anachomeka bati anapiga cement sijui na waterproof. Nyumba lazima ivuje, na pia kutu kwenye bati itakuja mapema sana. Synroof(Bitumen) bei ya ndoo moja 20kg ni 225,000 naona watu wengi wanakimbia bei au hawaijui
Sasa hapo kuna kuokoa gharama zipi? Materials ndio hayo na gharama ya ufundi ni kubwa.
 
Hapa kuna kitu naomba kujua mtu akikuchorea Ramani ni lazima afanye kazi? Na mchora Ramani kazi yake si kuchora tu au na kujenga anajenga?

Back to topic: hapo kwenye ucheap ndio penyewe sio kuwa hatupendi vitu vizuri ila mbuzi anakula urefu wa kamba.
Hii ya Mbuzi kula urefu wa kamba kumbe siku nyingi imenzaga.,[emoji1787][emoji1787]
 
Tunauza mbao kwa bei za jumla
2*4 fut 12=4400
2*4treated fut 12=4800
1*6 fut 12 = 4400
1*8 fut 12= 8500
1*8 ya fisherboard=9500
1*10=13500
1*10 ya fisherboard= 15000
2*2treated fut 12=2500
2*2 fut 12=2300
2*4treated fut 18=9500
2*6 fut 12=8500
2*6treated fut 18=16000
2*2treated fut 18=5000
2*3 fut 12=3500
1*4 fut 18=4000
1*4 fut 12=2500
Tunafanya delivery popote ulipo kwa Dar-es-salaam ,tunapatikana kwa namba hizi hapa 0759630751,
0654830416,
0687371138
vile vile huduma ya kuchana,kuranda na kusize mbao inapatikana ofisini kwetu ..
Ofisi zetu ziko Mbuyuni -Bagamoyo road
 
Shida kubwa ya contemporary House ni bati kuharibika mapema, Kwa maana bati Lina slope ndogo then linakaa na maji muda mrefu na kulifanya lioze haraka.
Shida hii haiwez onekana angalau after 6-13 yrs, Ila nawashauri wenye nyumba hizi wajipange sana
 
Back
Top Bottom