Gharama za Ujenzi kwa Nyumba za ‘Contemporary’ Vs ‘Traditional’ Roof

Ndugu zangu kama ni muonekano,jenga nyumba simple piga mgongo wa tembo yako kwa msouth,tengeneza mazingira vizuriyanayoizunguka nyumba yako,
Full stop itavutia tu
 
Shida kubwa ya contemporary House ni bati kuharibika mapema, Kwa maana bati Lina slope ndogo then linakaa na maji muda mrefu na kulifanya lioze haraka.
Shida hii haiwez onekana angalau after 6-13 yrs, Ila nawashauri wenye nyumba hizi wajipange sana
Sasa kama haiwezi kuonekana mapema wewe umeiona wapi? Yaani maji yatuame kwenye bati lenye slope ya degree 10? Labda hilo bati liwe limebonyea.
 
Sasa kama haiwezi kuonekana mapema wewe umeiona wapi? Yaani maji yatuame kwenye bati lenye slope ya degree 10? Labda hilo bati liwe limebonyea.
Mkuu niko na project ya contemporary na kuezeka ni mwezi wa 3 mwanzoni. Kelele za vitisho ninazopigiwa (kuhusu kuvuja) hadi nalala na hofu ama niahirishe. Lakini moyo wangu unazipenda sana hizi nyumba ni heri inifie mbeleni huko ila sio ya kuikosa katika umri huu.

Kama kuna mtu ana utaalamu wa hii kazi anicheki PM nimpe kazi ya kupaua.
 
Wapo wengi,kikubwa awe mtaalamu na usimbanie bei.

Hizo nyumba sio za njaa njaa
 
Kama nimeelewa vizuri, Cost ya Nyumba aina ya Contemporary, ikijengwa kitaalamu n bei yake inaweza kufanana na traditionnal roofing ?...
 
Tatizo lipo kwa mafundi wenyewe! Mnatoa bei za kukomoana! Nani alikuambia ww kunijengea nyumba yangu ndio unaponea kutatua matatizo yako yote? Muwe reasonable bana mfyuuuuu 😡!
Umenikumbusha kuna mtu kaniambia juzi huko mkoani kwetu viwanja vinauzwa bei kubwa kuliko hata dar. Nikamuuliza shida nini huko mpaka ardhi ifikw thamani kubwa hivyo? Akasema hawa wenzetu maisha yamewapiga sana sasa ukitaka kununua ardhi anataka matatizo yake yoote ayamalize🤣🤣🤣
 
Nyumba bwana ikichorwa hivi inapendeza mno.

Jenga sasa mpaka uifikishe mwonekano huo utachina.

Viwanja vyenyewe vya Mbezi Makabe huku Contemporary haikai🤣
 
Nyumba bwana ikichorwa hivi inapendeza mno.

Jenga sasa mpaka uifikishe mwonekano huo utachina.

Viwanja vyenyewe vya Mbezi Makabe huku Contemporary haikai🤣
Sure kwa sehemu za mabonde nyumba za namna hii labda ijengwe eneo la juu lakini ikijengwa bondeni haipendezi maana roofing yake inakua inaoneka
 
Naomba kuliza, fundi amabaye hajawahi kujenga Contemporary style anaweza kujenga foundation hari lenta?
Kama anauzoefu wa nyumba za kawaida ndio anaweza vizuri tu boss. Lakini ni vizuri ukawa na ramani (au muhimu ijulikane ‘gutter’ litapita kwenye ukuta upi wa jengo) vinginevyo inaweza kuja kusumbua kuamua sehemu ya kujengea concrete gutter au ikalazimu kuweka mengi kitu ambacho kinaongeza gharama
 
Kama nimeelewa vizuri, Cost ya Nyumba aina ya Contemporary, ikijengwa kitaalamu n bei yake inaweza kufanana na traditionnal roofing ?...
Muhimu ni ikisanifiwa (design) vizuri, kwamaana ya kwamba ikiwezekana mtaro wa maji uwe mmoja tu, au kama lengo hasa ni kupunga gharama basi usiweke kabisa mtaro (upande w nyuma uwe wazi) hapo uta save sana kuliko traditional roofing
 
Contemporary ndio nini? Kama hautaki bati lionekane kwa nini usimwage zege kabisa? Shida ya mapaa haya sio slope au ujuzi wa fundi. Shida ni mtu aliyechora. Matatizo mengi yanatokea pale ambapo bati linakutana na ukuta. Wengi wanachimbia kwenye ukuta. Hilo ni kosa kwa sababu bati na simenti na maji sio rafiki. Kinachotakiwa kufanyika ni kuchukua kipande kingine cha bati ambacho kitakunjwa kufunika hiyo joint na kuendelea juu na ukuta kama inchi 6 hafafu unaikunja tena kuiingiza kwenye ukuta. Bati hapo haliathiriki kwa sababu maji hayalifikii linaooingia kwenye ukuta. Kwa lugha ya kitaalamu kipande hiki çha bati kinaitwa "flashing".

Amandla....
 
Unamaanisha hivi?
 
Mkuu wewe ni fundi? kama Yes naomba namba yako PM au kama unaye fundi wako ni PM.
 
Ni Fundi. Lakini sio mjenzi.

Amandla...
Vp tunaweza fanya kazi ya paa kuweka hizo kitu mkuu! tumeipenda hiyo design...maana kuna nyumba ya familia inaleta shida...na fundi wa kitaaa anasema itawekwa cement haitavuja. Tunataka tumkatae, mafundi wanatofautiana na technology pia.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…