Gharama za umeme: Rais Samia muwajibishe Waziri Kalemani na uongozi wote wa TANESCO

Kwanza umeme ulipaswa usambazwe bule kote nchini ili kwamba watu wote wapate huduma kisha gharama zirudi kupitia matumizi,mtoa mada elimu pekee ya kukariri darasani haitoshi kukufanya kua bright Bali ukichanganya na maarifa ndo unakua bright
 
We jamaa hata hujui ulichoandika. Nakupa mifano 3.

Kutengeneza mnara mmoja wa Simu ni zaidi ya 300,000,000 na kila baada ya km 3-15 kulingana na wingi wa. Watu makampuni ya simu wameweka mnara. Na simu kadi zinauzwa kwa tajiri au masikini kwa 1000 tu, je uliwahi kuona gaharama za mnara?

Pili wazalishaji wa bia na soda hata ukienda hapo getin kwao Bei ya soda au bia ni sawa na kule misenyi, Namtumbo, vudee au Makete. Wao wamewezaje Tanesco washindwe?

Miundombinu yote ya umeme Hadi meter ni Mali ya Tanesco, miundombinu ya mteja ni kuanzia umeme unatoka kwenye meter kuingia ndani mwako.

Swali, mteja anunua meter, nguzo, waya Kisha vyote viendelee kuwa Mali ya Tanesco. Hii ni sahihi?

Ukinunia line ya simu ni yako, simu yenyewe ni yako unachopatiwa na kampuni ya simu ni huduma ya mawasliano na sio vifaa vyao.

Hivyo hivyo kwa mashirika ya kugawa maji wanakuuzia maji tu mtandao wote ni wa kwao.
 
Daaaa tuvuteni umeme vijijini kwetu na mashambani hamani daaa safi sana
 
Bilioni 30 kilikuwa kiwanda Cha kutengeneza nuklia? Hicho kiwanda ni very simple na gharama nafuu sana hata 1 bilioni hakifiki.
Mimi nilishangaa sana. Manguzo yale ya miti hata hawa wauza mbao waliojijenga na uzoefu wa muda mrefu si wanaweza. Hata wakijenga mitambo ya kuchemsha nguzo za miti na kutia dawa, kutengeneza za simenti na za vyuma sitarajii ivuke bilioni 10 na hapo wakizalisha nyingi.
 
Hii ndo TD kila zuri ukifanya alikosi wakosoaji wenye akili zaidi
 
Politiki kitu Mbaya sana

Sent from my SM-G973U using JamiiForums mobile app
 
Mm naona yuko sawa kazi ya serikali nakugharamikia wananchi wake kwn hakuna nchi umeme unavutiwa Bure kabisa acheni propaganda. Tanesco itazidi kupata mapato kwa wingi kama watanzania wengi wakiwa na umeme. Na kuwa tajiri sio kigezo chakutoa pesa nyingi ndio upate umeme Kwan tajiri pia ni mwananchi na anahaki pia kama wengine.
 
Kuna watz wapumbavu jamani!

Kwa hiyo watu wa masaki ni kielelezo cha watz wote?
 
27,000 Bado ni nyingi,ilitakiwa umeme ufungwe Bure kabisaaaa.

Wameanza vizuri laki 5 na 20 ilikuwa pasua kichwa ila 27,000/= sio mbaya!! wananchi wengi watafunga umeme ,wengi walikuwa wanashindwa kuunganisha umeme gharama zilikuwa kubwa sana,kwa hili TANESCO wataongeza mapato sana maana wataongeza watumiaji wa umeme.
 
Tanesco makao makuu watabisha
 
Tanesco makao makuu watabisha

Hawawezi kubisha maana order imetoka juu na maazimio yalifanyika tangu may 5 na taarifa imetoka jana kichofuata ni utekelezaji tu na Tanesco wenyewe wanayo hiyo taarifa ni 27,000/= tu tanzania nzima mjini na vijini kasoro Dar City centre tu hiyo ni umeme wa single phase.
 
Na sasa anataka mtu hata aliejenga fremu 40 za biashara nae alipe elfu 27.
Au ghorofa Upanga la apartment 40 alipe elfu 27.. imagine that
1. Gharama za elfu 27 ni kwa wale wa single phase tu.

2. Gharama hizo haziwahusu watu wa Dar es salaam City centre, wao watalipa gharama za kawaida.

3. Nia ni kuhakikisha umeme unafika nchi nzima. Ili nia hiyo itimie ni vyema kupunguza gharama za kuunganisha umeme.

4. Umeme kwa sasa unazalishwa mwingi. Hakuna haja kuwa na umeme unaobaki bila matumizi wakati unaweza kuwaunganishia watu na wakalipa bill/luku shirika likapata mapato.

5. Kwa mujibu wa taarifa ya Waziri Kalemani bungeni ya bajeti ya wizara yake, alisema Tanescoa imeacha kutegemea ruzuku ya serikali kuu tangu mwaka huu wa fedha kuanza. Kwahiyo, Tanesco inajitegemea siku hizi.
 
Serikali ndio inatoa hela kuunganishia watu umeme, wewe kinachokuuma ni nini?

Kwani hapo kuna hela ya Tanesco? Si ya serikali, sasa kama serikali inataka watu wawekewe umeme hata bure as long as inaipatia tanesco gharama za kununua material wewe unaumia nini?

Tanesco haina investment cost yoyote kwani hela zinatolewa na serikali. Wewe unaumia watu kuunganishiwa kwa 27000? Ilitakiwa kua bure kabisa.
 
Haya maelezo (namba 2) umeyatoa wap? Waziri kasema sehemu zote kasoro ilala ambako hata hawahitaji kwa sasa
 
2. Gharama hizo haziwahusu watu wa Dar es salaam, wao watalipa gharama za kawaida.

Karudie kusoma vizuri tangazo ,except Dar City Centre , Je Dar city centre ni wapi? Unajua maana ya centre? Nyie ndio mnapotosha watu wa tanesco na kuwasikiliza nyie.

Mjini na vijini gharama za single phase ni 27,000/= except Dar City Center , hawakusema except Dar-es-salaam!! Maana hata Gongo la mboto mwisho wa lami ni Dar,Kongowe ni Dar,yale yale puna ni dar ,Bunju ni dar na wote hao wapo nje ya mji.
 
Tushaanza kuona madhara ya siasa kwenye huu upuuzi. Dodoma umeme ulikua haukatiki ila siku hizi kila siku..kama sasa hivi maeneo ya nkuhungu huku umekatika
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…