To be honest wababa wengi ni ile mnajua mtoto amekula, ameenda shule, anavaa vizuri, anatibiwa, the rest ni kazi ya mama yake. Baba muda wote anawaza madeal, mtu hawazi hata kuna family time, mkae mzungumze mcheze, muwafundishe watoto wenu etc. Baba kila siku anarudi watoto wameshalala mmh. Sasa ndo ukute mama naye ana mambo mengi, basi mlezi mkuu anakuwa house gal. Sad
Mtu umeoa lakini still unataka kubehave as a bachelor. Ndo hayo "ooh nikirudi mapema washkaji watanionaje". Ujinga tu na kushikiwa akili, usioe basi uendelee kuwaplease washkaji
Wewe usicheke bana, juzi mtu anaongea wanaume wengi mnajisahau kwenye ndoa zenu, wake zenu wanahitaji sana attention yenu , mtu kajibu "baba ako alikuwa anakupa attention" mweee