Gigy Money kafanya nini huko kwenye ziara ya Tumewasha na Tigo?

Mashabiki wa dabiliyusibii kiukweli mmeuanza mwaka vibaya mno, wapi ccm baba lao, 6 months again,πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚πŸ˜‚
 
Hii ni sawa na kuzuia mvua na kipande cha kanga, hivi vitu havizuiliki ndio dunia iliko na Tz ni sehem ya dunia, watu wana access ya vyombo vya habari vya kimataifa na huku hayo ni maisha ya kawaida sana, kwa sasa kila mtu anachagua anachotaka kuangalia, cha msingi ni kufundisha watoto kibaya na kizuri ili wakiwa wakubwa wafanye uchaguzi sahihi
 
Hakuna kazi kubwa kama kuwalea watoto katika maadili kama nyakati hizi, watoto wetu wameharibika na miondoko hii, angalau kuwe na adhabu kali isaidie kuwaweka watoto wetu mbali na mambo ya shetani
 
Hivi TCRA kabla hawajafungia kituo huwa wanatafakari Kwa kina madhara yake Kwa Uchumi Wa Jamii na nchi Kiujumla?

Binafsi pamoja na kutokuwa mdau wa Hizo Wasafi Media bado siamini kuwa hii tabia ya fungia fungia ina afya njema Kwa nchi kiujumla.
Kuna makosa ni dhahiri hayahitaji kujadili vinginevyo
 
Angalia point iliyokusudiwa katika andiko na sio kuongea maneno mengi hebu onyesha uchi katika hiyo picha.
 
Why wameifungia hali imesaidia Sana ushindi wa CCM
Fikra hizi ndio zilileta ushikaji serikali. Yaani kwa sababu walilipwa kufanya kampeni, basi hata wakifanya kosa wasi adhibiwe?

Tulilalamika kipindi cha Kikwete kuhusu ushikaji, sasa hivi tuna utaka.

Sent from my SM-G935F using JamiiForums mobile app
 
Hata sasa ushikaji ni zaidi hasa ukiwa na chapa.
Chenge, Bashite,kange,musiba,sabaya,
 
Nguo inaonyesha mifano ya utamu we unasema kuwa haina shida utamu nauona kabisa tena wameweka na vile vimavuzi we jamaa sijui unatetea nini hapa.
Siyo kwamba akili ya kikahaba imetuvaa Sana watanzania ndo maana?. Kwann huo mchoro usiuone kama ramani ya Iran?
 
Wasamehewe kwa kuwa hawakujua watendalo.
Hata hivyo vyombo vinavyohusika na maadili ya sanaa, wasanii na vituo vya TVs watoe dress codes ili pasitokee yeyote ambaye atasema hakufahamu.
Kama dress codes zipo tayari na wao wamevunja hilo ni kosa.
 
Angalia point iliyokusudiwa katika andiko na sio kuongea maneno mengi hebu onyesha uchi katika hiyo picha.
View attachment 1669598
Wewe ukiwa na Binti yako.. (would you be comfortable na uvaaji huu!?)

If not then hayo si maadili. Hiyo picha kwangu mimi sio tu mbaya ila yuko uchi kabisa... Na hiyo ni kwa watanzania asilimia 65+ tunaoishi vijijini...
 
Halafu jitu jinga kama wewe unaangalia miziki ya kina niki minaj 'na mashow yao kina beyonce 'na yanaonyeshwa kwenye tv station za kibongo 'na unashangilia kwa furaha kabisa 'na havifunguwi akifanya mbongo mnapayuka tu
Tena a naangalia akiwa na family yake
 
Lady Gaga, huyo hapo Cher.. 'na wapo wengi video zao zjnaonyeshwa ...labda niulize TUNARUHUSU HUO MNAOITA UTUPU UONYESHWE NA WASANII WA KIMATAIFA KWENYE TAIFA LETU ila wasanii wetu wavae madera vitenge 'na raba !!!??

Yaani acha tu Mkuu nilishawahi hoji ,inakuwaje Radio za TZ muziki wao wa bongo fleva wanacheza Dirty Version(Ambazo tunaelewa matusi yote) lakini Miziki ya Nje ambayo hatuielewi hata wakiimba matusi wanacheza clean version.

-Utasikia nipe hogo ,unavyokata unagusa goroli ,mara miguu iguse mabega ,mara nakupa mikito heavy na ndio zinachezwa daily!! Ni muda muhafaka sasa wa TCRA wawaambie Radio wacheze clean version kama kuna matusi matusi au lugha zisizo na stara waedit(wafute ,wascratch,mute etc),BASATA inakuwaje wanaruhusu nyimbo zenye maudhui ya matusi kuchezwa? Kuna video ya harmonize wanaonyesha demu anatingisha chura na pia wanaonyesha jamaa anapaka mkongo yupo kitandani na demu,scenes kama zile inatakiwa wazifute.

Video za Mtoni wana dirty version na clean version ,kwenye clean vesrion hauwezi kuta wanaonyesha makalio ya demu hata kama kavaa suruali.
 
Kwanini asivae nguo nyingine, hiyo nguo kwetu hapa Tanzania haina miiko ya kimaadili, ni nguo inayoleta imagination nyingi zisizo na msingi.
Kuna Miiko na maadili ya Kitanzania !!!!...

Hivi miiko ya kichaga ni sawa na ya kizaramo au ya kinyakyusa ni sawa na ya kiyao ???..

au ndio ufuska unaofanyika kila station mwenge unapolala au ni hizi twerking na kumwaga radhi kwenye singeli, vigoma na vibao kata.

Halafu unasemaje "Imaginations"..
Yaani unataka watu wawe responsible na weak minds za watu ??..

sikubaliani kiasi pengine na walichokifanya wasafi ila hii issue imekuzwa kupitilza
 
Hiyo picha iliyobandikwa ukii-zoom na kufanya tafsiri (photograph interpretation) vizuri, utapata jibu kwa nini TCRA imetoa adhabu hiyo.

Ni nguo tu .... Wabongo kujifanya watakatifu
 
Ni unafiki wa kuptiliza.Hata hao waajiriwa wa TCRA wana picha za pono katika simu zao za mkononi.Sana sana walichokifanya TCRA ni promosheni ya mambo ya ngono.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…